Infinix, baada ya kuliteka soko
na toleo pendwa la Infinix S4, Infinix imezindua rasmi Infinix S5,
kinamara wa toleo la S series kwa sasa ikiwa na Infinity-O Display na
32MP. Ujio wa Infinix S5 umeambatana msimu wa sikukuu za Christmas na
Mwaka mpya hivyo Infinix kusheherekea msimu huu kwa kuzindua rasmi
promotion itayoanza rasmi tarehe 25/11/2019 na zawadi mbalimbali kama
vile Vacuum Cleaner, Deep Flyer, Subwoofer Radio.
Akizungumza na vyombo vya habari
wakati wa uzinduzi wa Infinix S5, Afisa wa mahusino wa kampuni ya
Infinix, Aisha Karupa alisema, “Infinix ikiwa ni kampuni yenye ushawishi
mkubwa katika mfumo wa kidigitali tunawahakikishia wateja wetu bidhaa
zenye teknolojia ya hali ya juu kwa bei Rafiki”,
Vile vile Aisha aligusia kuhusiana
na sifa za simu hiyo kwa kusema, “na pamoja ya kuwa na selfie kali
yenye 32MP lakini pia inasifa lukuki kama vile teknolojia ya Artifficial
Intelligence kwenye kamera 4 za nyuma ambazo ni 16MP+5MP+2MP+AI Lens,
lakini pia Infinix S5 ina memory card ya ukubwa wa GB 4 kwa GB64 yenye
uwezo wa kutunza kumbukumbu nyingi pasipo huitaji ya memory card ya
ziada na kwa upande wa design Infinix S5 imekuja katika muonekano wa
kitofauti wenye kuvutia kutokana na namna kamera ya mbele ilivyopachikwa
ndani ya Display kwa jina la kitaalamu Infinity-O Display na kwa wale
wenye matumizi mengi Infinix S4 inauwezo wa kukaa na chaji kwa muda
mrefu kutokana na ujazo mkubwa wa Battery wenye mAh40,000”.
Pia Infinix wametumia nafasi hiyo
kutambulisha rasmi promotion ya msimu wa sikukuu inayoenda sambamba na
uzinduzi wa Infinix S5. Akizungumza meneja wa mauzo wa Infinix Bwana
Fredy Kadilana alisema kwamba, katika msimu huu wa sikukuu za Christmas
na mwaka mpya Infinix imezindua rasmi promotion itakayompa nafasi mteja
wa Infinix S5 au mteja wa simu yoyote ya Infinix kujishindia zawadi
mbalimbali kama vile Vacuum Cleaner, Deep Flyer, Subwoofer Radio na
nyengine nyingi lakini pia Infinix haijasahau wadau wake wa
wanaotembelea kurasa @infinixmobiletz kwa kuitambulisha challenge ya
#S5showitoff itayoanza rasmi mwishoni mwa wiki hii”.
Kwa maelezo zaidi tembelea
No comments:
Post a Comment