Waziri
wa Nishati, Dkt Medard Kalemani akizungumza katika kikao chake na Wafanyakazi, Menejimenti na
Bodi ya Wakala wa Nishati Vijijini (REA). Wengine katika picha Kaimu Katibu
Mkuu, Wizara ya Nishati, Raphael Nombo (kulia kwa Waziri), Kamishna wa Umeme na
Nishati Jadidifu, Mhandisi Leonard Masanja (wa kwanza kushoto), Mjumbe wa Bodi
ya REA, Dailin Mgweno na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa REA, Mhandisi Amos Maganga.
Baadhi
ya Wafanyakazi na Menejimenti ya Wakala
wa Nishati Vijijini (REA) wakiwa katika kikao chao na Waziri wa Nishati, Dkt
Medard Kalemani kilichofanyika jijini Dodoma.
Kamishna
wa Umeme na Nishati Jadidifu, Mhandisi Leonard Masanja akiwasalimia Wafanyakazi
na Menejimenti na Bodi ya Wakala wa Nishati Vijijini (REA) wakati wa kikao chao
na Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani kilichofanyika jijini Dodoma. Kulia
kwake ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa REA, Mhandisi Amos Maganga na kushoto kwake
ni Mjumbe wa Bodi ya REA, Dkt Andrew Komba.
Baadhi
ya Wafanyakazi na Menejimenti ya Wakala
wa Nishati Vijijini (REA) wakiwa katika kikao chao na Waziri wa Nishati, Dkt
Medard Kalemani kilichofanyika jijini Dodoma.
Kaimu
Katibu Mkuu Wizara ya Nishati, Raphael Nombo, akizungumza na Wafanyakazi, Menejimenti na Bodi ya Wakala wa
Nishati Vijijini (REA) wakati wa kikao chao na Waziri wa Nishati, Dkt Medard
Kalemani (kushoto) kilichofanyika jijini
Dodoma.
....................................
Na Teresia Mhagama, Dodoma
Waziri
wa Nishati, Dkt Medard Kalemani, ameagiza kuwa wakandarasi wa umeme vijijini
wenye mikataba wahakikishe kuwa wanamaliza kazi za usambazaji umeme vijijini ifikapo
tarehe 31 Disemba mwaka huu.
Dkt
Medard Kalemani aliyasema hayo hivi karibuni wakati wa kikao chake na
Wafanyakazi, Menejimenti na Bodi ya Wakala wa Nishati Vijijini (REA).
Kikao hicho kilifanyika jijini Dodoma na
kuhudhuriwa na Viongozi mbalimbali wa Wizara ya Nishati, akiwemo Kaimu Katibu
Mkuu, Raphael Nombo, Kamishna wa Umeme na Nishati Jadidifu, Mhandisi Leonard
Masanja na Kamishna Msaidizi wa Maendeleo ya Nishati, Mhandisi Juma Mkobya.
“Kila
mtumishi anayehusika na suala hili, ahakikishe kuwa anasimamia ipasavyo kazi
yake ili lengo litimie, iwe ni mtu wa fedha, mhandisi, mtu wa manunuzi, lengo
ni kupeleka umeme vijijini kwa muda uliopangwa na kwa ufanisi.” Alisema Dkt
Kalemani.
Kufuatia agizo hilo, Dkt Kalemani aliwataka
watumishi wa REA kuanza maandalizi ya utekelezaji wa mradi wa umeme vijijini wa
Awamu ya Tatu mzunguko wa pili (REA III, Round II) ili ifikapo tarehe 31,
Januari 2020, utekelezaji wake uanze.
“ Bado kuna muda wa kutosha wa maandalizi,
hivyo kama kuna sheria, kanuni na taratibu zinazopaswa kufuatwa, zizingatiwe na
masuala yote yafanyike ndani ya muda, ili utekelezaji uanze, lengo letu sote ni
kufikisha umeme kwenye vijiji vyote ifikapo mwaka 2021.” Alisema Dkt Kalemani.
Waziri
wa Nishati pia aliagiza kuwa, Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) na REA
washirikiane katika kusimamia utekelezaji wa miradi ya umeme vijijini na
kuwachukulia hatua wakandarasi wazembe.
Aidha alitoa agizo kuwa, wakandarasi wote wa
umeme vijijini mara wanapomaliza kazi waliyopangiwa na Serikali, wanapaswa kufanya
makabidhiano na TANESCO au REA badala ya kuondoka kiholela katika maeneo
waliyopangiwa kusambaza umeme ili kujirisha na masuala mbalimbali ikiwemo kama
kazi husika imezingatia ubora na wigo.
Vilevile, aliendelea kusisitiza kuhusu suala
la wasimamizi wa miradi ya umeme vijijini, kufuatilia kwa karibu kazi
zinazoendelea za usambazaji umeme vijijini badala ya kutumia muda mwingi kuwa
maofisini.
Waziri
wa Nishati na Kaimu Katibu Mkuu, pia walizungumza na watumishi wa REA kuhusu
masuala kiutumishi ambayo yatapelekea utatuzi wa changamoto mbalimbali na
kuongeza morali ya kazi kwa watumishi hao.
Kwa
upande wake, Kamishna wa Umeme na Nishati Jadidifu, Mhandisi Leonard Masanja
alisisitiza kuhusu suala la kufuata haki na sheria wakati wa mchakato wa kupata
wakandarasi wa umeme vijijini ili kuepuka migogoro itakayochelewesha
utekelezaji wa miradi.
Aidha,
alisema kuwa agizo la Waziri, kuhusu wasimamizi wa miradi ya umeme vijijini
kwenda katika maeneo ya kazi ili kusimamia kazi hizo kwa karibu halina budi
kutekelezwa kwani ni jukumu la Taasisi kusimamia miradi hiyo.
Kwa
upande wake, Kaimu Mwenyekiti wa Bodi ya REA, Dkt Andrew Komba alimshukuru
Waziri wa Nishati kwa kufanya kikao na Bodi, Menejimenti na Wafanyakazi wa REA
na kueleza kuwa vikao vya aina hiyo, vinasaidia kutoa mwelekeo wa Serikali
inakotaka kwenda na kufanya utatuzi wa changamoto mbalimbali.
Dkt
Komba pamoja kueleza masuala mbalimbali ambayo yamefanyiwa kazi na Bodi hiyo
ili kuboresha masuala la kiutumishi na kazi za usambazaji umeme vijijini,
aliahidi kuwa Bodi hiyo itayazingatia maagizo yaliyotolewa na Waziri wa
Nishati.
No comments:
Post a Comment