Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri
Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista
Mhagama akimkabidhi zawadi aliyekuwa Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo (Bunge na
Waziri Mkuu) Bi. Maimuna Tarishi wakati wahafla fupi ya kumuaga
iliyoandaliwa na ofisi yake.
Katibu Mkuu Msaafu wacOfisi ya
Waziri Mkuu (Bunge na Waziri Mkuu) Bi. Maimuna Tarishi akieleza historia
yake katika utumishi wa umma (Miaka 34) kwa timu ya menejimenti ya
ofisi hiyo wakati wa hafla fupi ya kumuaga iliyoongozwa na Waziri wa
Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Wenye
Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama katika Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi hiyo
Jijini Dodoma.
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Uwekezaji) Bi.Dorothy Mwaluko akizungumza wakati wa halfa hiyo.
Katibu
Mkuu Mstaafu wa Ofisi ya Waziri Mkuu (Bunge na Waziri Mkuu) hiyo Bi.
Maimuna akizungumza na timu ya Menejimenti ya ofisi hiyo wakati wa hafla
fupi ya kumuaga kwa kustaafu utumishi wa umma kwa mujibu wa sheria za
utumishi.
Mhasibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Bw.Anthony Chayeka akichangia jambo wakati wa kikao hicho.
********************************
NA.MWANDISHI WETU
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri
Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu
Mhe. Jenista Mhagama amempongeza aliyekuwa Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo
Bi.Maimuna Tarishi kwa utendaji wenye weledi kwa kipindi cha miaka 34
alichotumikia katika utumishi wa umma.
Ametoa pongezi hizo wakati wa
hafla fupi ya kumuaga na kumpongeza katibu mkuu huyo aliyestaafu
utumishi wake wa umma kwa mujibu wa sheria za utumishi nchini mapema
mwanzoni mwa mwezi Septemba Jijini Dodoma.
“Kwa dhati nachukua nafasi hii
kumpongeza Bi. Tarishi kwa namna alivyotumikia Taifa hususani akiwa
katika Ofisi hii ya Waziri Mkuu, amefanya vizuri na alijitahidi sana
kusimamia vyema ofisi kuhakikisha ofisi inaenda vizuri na hakika
unastahiri pongezi kwa kuzingatia ulivyotekeleza majukumu yako kwa
busara na weledi wa hali juu,”
Waziri aliongezea kuwa, mchango wa
Katibu mkuu huyo ni mkubwa kwa kuzingatia namna alivyotumika kwa miaka
mitatu katika ofisi hiyo kwa kuhudumia Ofisi binafsi ya Mhe.Waziri Mkuu
pamoja na Uratibu wa Shughuli zote za Bunge.
“Umekuwa ni kiungo muhimu katika
kuhakikisha shughuli za Mhe.Waziri Mkuu pamoja na bunge zinatekelezwa
katika viwango vya hali ya juu kwa kusimamia vyema hivyo tutakumbuka
mchango wako kwa kipindi chote ulichokuwa nasi,”alisema Waziri Mhagama
Aidha Waziri alipongeza timu ya
menejimenti ya ofisi hiyo na kukiri kuridhishwa na utendaji wao wenye
ufanisi na weledi wa hali ya juu kwa kuzingatia misingi, kanuni na
sheria za utumishi wa umma.
“Kipekee ninawapongeza timu ya
menejimenti kwa usimamizi wenu mzuri wa ofisi hii hivyo niwatie moyo
muendelee kutekeleza majukumu yenu ili kuzaa matunda yanayoonekana kwa
kuzingatia ofisi hii ni mratibu wa shughuli zote za
serikali,”Alisisitiza Waziri Mhagama
Kwa upande wake aliyekuwa Katibu
Mkuu wa Ofisi hiyo Bi.Maimuna Tarishi alishukuru Ofisi ya Waziri mkuu
kwa namna walivyochangia katika utekelezaji wake wa majukumu kwa muda
aliotumikia katika ofisi hiyo toka tarehe 4 Aprili 2017 alipoteuliwa
kusimamia shughuli za Bunge na Waziri Mkuu.
Aidha Tarishi aliiasa timu ya
menejimenti kuendelea kuwatumia watumishi vijana katika kutekeleza
majukumu kwa kuzingatia uwezo waliona katika kufiri, kutenda na kujituma
kwa dhati.
“Nishauri Watendaji mnaobaki
wekezeni kwa vijana kwa kuzingatia wanauwezo mkubwa wa kufikiri kwa
haraka, wepesi kutenda na wakiaminiwa wanatekeleza kwa juhudi ili
kuthibitisha uwezo wao hivyo muwatumie kwa tija na maendeleo ya nchi
yetu’”alisema Tarishi
Aidha aliongezea kuwa, uwepo wa
vijana katika ofisi za umma unamchango mkubwa kwa kuzingatia uwezo
walionao wa kubuni mbinu mbalimbali zinazorahisisha utendaji kazi kwa
kuzingatia ukuaji wa sayansi na teknolojia hivyo wekezeni nguvu kwa
kundi hilo.
“Chukue fursa ya ukuaji wa sayansi
na teknolojia katika kuboresha ufanishi na ubunifu katika kutekeleza
majukumu yenu ya kila siku kwa kuwekeza kwa vijana, kwa kuwatia moyo na
kuwaelekeza pindi inapobidi ili kuleta matokeo chanya katika kutekeleza
majukumu ya kila siku,”alisisitiza Tarishi.
No comments:
Post a Comment