Naibu Spika wa Bunge la Tanzania Dkt. Tulia Ackson akimkaribisha Spika wa Bunge la Jimbo la Shanghai nchini China Bi. Yin Yicui.
Naibu Spika wa Bunge la Tanzania
Dkt. Tulia Ackson akimkaribisha akieleza jambo katika mazungumzo na
Spika wa Bunge la Jimbo la Shanghai nchini China Bi. Yin Yicui
yaliyofanyika katika ofisi ndogo za Bunge Jijini Dar es salaam.
Naibu Spika wa Bunge la Tanzania
Dkt. Tulia Ackson akipokea zawadi kutoka kwa Spika wa Bunge la Jimbo la
Shanghai nchini China Bi. Yin Yicui baada ya mazungumzo yaliyofanyika
katika ofisi ndogo za Bunge Jijini Dar es salaam.
Naibu Spika wa Bunge la Tanzania
Dkt. Tulia Ackson na Spika wa Bunge la Jimbo la Shanghai nchini China
Bi. Yin Yicui wakiwa katika picha ya pamoja na Ujumbe wa Wabunge kutoka
Jimbo la Shanghai China.
………………
Na. Dianarose Shirima- Maelezo
Spika wa bunge la Shengai Yin
Yicui,yuko nchini na wajumbe kumi na mbili wa bunge hilo ambapo jiji
Dar es Salaam wamekutana na Naibu Spika wa Bunge Dkt. Tulia Akson
Mwansasu kwa lengo la kubadilishana uzoefu mbalimbali kwa pande zote
mbili. Spika Yin Yicui na wenzake wamefurahishwa na mapokezi na kusema
kuwa baada ya kupokea mwaliko kutoka kwa Spika wa Tanzania wakati
alipotembelea Shengai, walifurahia kupata mwaliko huo na kuahidi kuja
Tanzania.
Spika huyo aliongeza kuwa
Tanzania pamoja na jimbo hilo la Shengai limekuwa na uhusiano mzuri toka
huko nyuma na kulenga kuendeleza maslahi mapana ya maendeleo ya
Tanzania pamoja na jimbo hilo la Shengai.
Katika mazungumzo yao wamejikita
zaidi kuona jinsi wanavyoweza kushirikiana katika sekta ya
elimu,mazingira na utunzaji wa maliasili na wanyamapori, ambapo
watashirikiana katika hatua za utekelezaji.
Kwa upande wa mazingira, Bunge la
Shengai linaangalia namna linavyoweza kusaidia uboreshaji wa mazingira,
ambapowalipongeza serikali ya Tanzania kwa kupitisha sheria ya kupiga
marufuku utumiaji wa mifuko ya plastiki na kuongeza kuwa, nchini kwao
jimbo la Shengai wanajiandaa kupitisha sheria ambayo inahitaji
utenganishi wa aina za takataka za majumbani. kwamba takataka za nyanya
zisichanganywe na makopo. Dkt. Tulia aliongezea kuwa Tanzania inaangalia
namna itakavyoitumia hiyo sheria ili kujifunza.
Naibu Spika aliwashukuru jinsi
China wanavyoisaidia Tanzania kwa upande wa ufadhili wa masomo ya nje
wanafunzi wanaotoka Tanzania, ambapo alisema ufadhili wao ni tofauti na
ufadhili wa nchi nyingine, kwamba China huomba wanafunzi kwenda kusoma
China wakati mataifa mengine wanafunzi huomba moja kwa moja katika nchi
wanazopenda kusoma, pia katika vyuo vya VETA wataangalia ni kwa namna
gani wanaweza kushirikiana na Tanzania ikiwemo kusaidia vifaa vya
kufundishia kama vile kompyuta.
Mwisho walizungumzia namna ya
Tanzania kutunza raslimali zilizopo nchini ambapo ni pamoja na
wanyamapori na uoto wa asili, na kuahidi kuwa bega kwa bega na Tanzania
ili kukuza na kuendeleza rasilimali za nchi.
No comments:
Post a Comment