Tuesday, September 17, 2019

WAZIRI HASUNGA: WATENDAJI WIZARA YA KILIMO JIPANGENI KUFIKIA MALENGO



Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga akisisitiza akisisitiza jambo wakati akifungua kikao kazi kilichowakutananisha Wenyeviti wa Bodi na Taasisi za Wizara hiyo, Wakurugenzi na Watendaji wakuu wa Bodi na Taasisi kwenye ukumbi wa Ofisi ndogo ya wizara ya Kilimo Jijini Dodoma ili kujadili utekelezaji wa mikakati waliyojiwekea, tarehe 17 Septemba 2019. (Picha Zote Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo)
Naibu waziri wa Kilimo Mhe Hussein Bashe akizungumza wakati wa kikao kazi kilichowakutananisha Wenyeviti wa Bodi na Taasisi za Wizara hiyo, Wakurugenzi na Watendaji wakuu wa Bodi na Taasisi kwenye ukumbi wa Ofisi ndogo ya wizara ya Kilimo Jijini Dodoma ili kujadili utekelezaji wa mikakati waliyojiwekea, tarehe 17 Septemba 2019.
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga akisisitiza jambo wakati akifungua kikao kazi kilichowakutananisha Wenyeviti wa Bodi na Taasisi za Wizara hiyo, Wakurugenzi na Watendaji wakuu wa Bodi na Taasisi kwenye ukumbi wa Ofisi ndogo ya wizara ya Kilimo Jijini Dodoma ili kujadili utekelezaji wa mikakati waliyojiwekea, tarehe 17 Septemba 2019.


Revocatus Kassimba, Wizara ya Kilimo-Dodoma
                                                         
Watendaji wa wizara ya kilimo na taasisi zake wameagizwa kufanya kazi kwa weledi na maarifa ili kuweza kufikia malengo ya uzalishaji mazao nchini.

Agizo hili limetolewa leo (17.09.2019) jijini Dodoma na Waziri wa Kilimo Japhet Hasunga wakati wa kikao kazi cha watendaji wa wizara ,taasisi na bodi za mazao kujadili taarifa za utekelezaji wa malengo ya mwaka 2018/2019

Waziri Hasunga amewajulisha watendaji hao kuwa bado wizara na taasisi zake hazijafanikiwa kufikia lengo ya uzalishaji wenye kuzingatia tija na kuwezesha kilimo kiwe cha kibiashara

“Takwimu zinaonyesha hatujafanya vizuri kwenye kusaidia upatikanaji wa masoko ya mazao ya wakulima nchini kwa kipindi cha mwaka 2018/2019” Waziri Hasunga alieleza

Aliongeza  jukumu la wizara ni kuhamasisha uzalishaji na kuhakikisha mazao ya wakulima yanaongezwa thamani  ili kuwa na soko la uhakika.

Waziri Hasunga alisema changamoto ya masoko kwa mazao ya wakulima inahitaji kuwekewa mfumo mahsusi wa utatuzi ,hivyo ni jukumu la wataalam kuja na mipango mizuri ya utekelezaji.

‘Wizara yetu inasimamia aina 85 za mazao nchini  “ hii inafanya wizara kuhitaji weledi na utaalamu kupata ufumbuzi wa haraka wa  changamoto za mazao haya, alisisitiza Waziri Hasunga

Waziri wa kilimo ametaja  malengo sita (6)  ambayo serikali ya awamu ya tano inatumia kupima utendaji kazi wa wizara hiyo kwa mwaka 2019/2020, kwanza ni kuhakikisha nchi inazalisha chakula cha kutosha na kuwa na usalama wa chakula.

Pili,kilimo kinachangia upatikanaji wa fedha za kigeni, na tatu kilimo kinatoa mchango mkubwa katika pato la taifa zaidi ya asilimia 30 ya sasa.

Kigezo cha nne ni malighafi kiasi gani inapatikana kwa matumizi ya viwandani,tano kiasi gani cha ajira zimezalishwa katika sekta ya kilimo na sita namna gani wizara inasimamia ushirika nchini kuwa na tija na kuondoa kero.

Katika hatua nyingine Waziri Hasunga amewapongeza watendaji wote waliopo chini ya wizara hiyo kwa utendaji mzuri uliofanikisha Tanzania kuongoza kwa uzalishaji wa mazao ya chakula kati ya nchi za Afrika Mashariki mwaka 2019

“Nawapongeza wote waliosaidia nchi yetu kuzalisha mahindi kwa asilimia 103 na kuongoza Afrika Mashariki hali iliyofanya nchi kuwa una utoshelevu wa chakula wa asilimia 119” alipongeza Waziri Hasunga.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Bodi ya Pamba nchini Marco Mtunga ameelezea mafanikio ya zao  hilo kuwa  hadi kufikia mwezi huu Septemba tani 301,132 za pamba zimekusanywa toka kwa wakulima ikilinganishwa na tani 222,039 mwaka 2018

Aidha,Bodi ya Pamba nchini imefanikiwa kusambaza chupa milioni sita za viuatilifu kwa wakulima katika msimu huu 2019/2020 ili kudhibiti magonjwa kwenye zao hili.

Hata hivyo,Mtunga ameeleza kuwa zao la pamba linakabiliwa na changamoto kubwa ya soko kutokana na ukosefu wa wanunuzi wa uhakika.

“Tunaiomba serikali iingilie kati suala la upatikanaji wa soko la uhakika la pamba hususani katika mkoa wa Katavi ambako mvua sasa imeanza kunyesha na wakulima bado hawajauza pamba yao” alisema Mtunga

Mwisho.

No comments:

Post a Comment