Na Asha Said, DAR ES SALAAM
MSHAMBULIAJI wa timu ya Simba, Meddie Kagere amechaguliwa kuwa
Mchezaji Bora wa mwezi Agosti wa Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) msimu wa
2019/20, huku Salum Mayanga wa timu ya Ruvu Shooting akichaguliwa Kocha
Bora wa mwezi huo.
Kagere na Mayanga walitwaa tuzo hiyo baada ya kuwashinda wenzao
walioingia nao fainali, katika uchambuzi uliofanywa Dar es Salaam wiki
hii na Kamati ya Tuzo ya VPL inayotolewa na Shirikisho la Mpira wa Miguu
Tanzania (TFF), kutokana na mapendekezo kutoka kwa makocha waliopo
viwanja mbalimbali, ambavyo ligi hiyo inachezwa msimu huu.
Kwa mwezi huo wa Agosti kila timu ilicheza mchezo mmoja, ambapo
Kagere aliiongoza Simba kuibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya JKT
Ruvu, huku mshambuliaji huyo raia wa Rwanda akifunga mabao mawili na
kutoa pasi moja ya goli.
Kagere aliwashinda Lucas Kikoti wa Namungo FC aliyefunga pia
mabao mawili kwa timu yake katika ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Ndanda
na Seif Karihe wa Lipuli aliyeiongoza timu yake kupata ushindi wa mabao
3-1 dhidi ya Mtibwa Sugar, ambapo Karihe alitoa mchango mkubwa katika
mchezo huo ikiwa ni pamoja na kufunga bao 1. Kagere na Karihe hawakupata
kadi yoyote, wakati Kikoti alipata kadi ya njano.
Kwa upande wa Mayanga aliwashinda Mecky Mexime wa Kagera Sugar
na Hitimana Thiery wa Namungo, ambapo aliiongoza Ruvu Shooting kuibuka
na ushindi wa bao 1-0 ugenini dhidi ya Yanga moja ya timu vigogo hapa
nchini na yenye wachezaji nyota wa ndani na nje ya Tanzania.
Mayanga aliwashinda Mecky Mexime wa Kagera Sugar aliyeiongoza
pia timu yake kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 ugenini dhidi ya Biashara
United, huku Hitimana Thiery ambaye aliyeipandisha daraja Namungo FC na
kucheza Ligi Kuu kwa mara ya kwanza, ambapo katika mchezo wake wa kwanza
wa ligi iliibuka na ushindi wa mabao 2-1 nyumbani dhidi ya Ndanda FC
No comments:
Post a Comment