Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais
Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa anayeshughulikia afya Dkt. Dorothy
Gwajima akiwa katika kikao cha pamoja na Wenyeviti wa Mitaa na
vitongoji wakijadili masuala mbalimbali ya sekta ya afya leo, katika
kijiji cha Mkoyo, kata ya Hombolo Halmashauri ya Jiji la Dodoma.
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais
Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa anayeshughulikia afya Dkt. Dorothy
Gwajima akikagua kitabu cha kuingizia dawa katika Zahanati ya Ipala
kilichopo, katika kijiji cha cha Mwinyi , Halmashauri ya Jiji la Dodoma.
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais
Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa anayeshughulikia afya Dkt. Dorothy
Gwajima akikagua chumba cha dawa katika Zahanati ya Ipala iliyopo,
katika kijiji cha cha Mwinyi , Halmashauri ya Jiji la Dodoma
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais
Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa anayeshughulikia afya Dkt. Dorothy
Gwajima akionyesha mashine ya POSS inayotumika kwa ajili ya kukusanyia
mapato katika Zahanati ya Ihumwa, Halmashauri ya Jiji la Dodoma
……………………
Na. Angela Msimbira HOMBOLO
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais
Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa anayeshughulikia afya Dkt. Dorothy
Gwajima amewaagiza watumishi wa Sekta ya afya ngazi ya Msingi
kuhakikisha wanashirikisha Viongozi wa Mitaa, Vijiji na Kata mipango
yote ya afya inayohitaji ushirikishwaji wa wananchi.
Dkt. Gwajima ameyasema hayo leo
wakati alipokuwa kwenye ziara ya kutembelea vituo vya kutolea huduma kwa
lengo la kujionea maendeleo ya utoaji wa huduma za afya kwa jamii
pamoja na matayarisho ya vituo hivyo katika kushiriki huduma za afya ya
kinga katika kijiji cha Mkoyo, Kata ya Hombolo, Halmashauri ya Jiji la
Dodoma.
Amewataka watumishi hao
kuhakikisha wanawashirikisha viongozi wa dini na madhehebu mbalimbali
ili, somo la afya liweze kuwafikia wananchi wa makundi yote kokote
waliko kwa kuwa ushirikiano huo ni muhimu katika kujenga uelewa na
kufanyakazi kwa pamoja.
Dkt. Gwajima amefafanua kuwa,
watumishi wa sekta ya afya ngazi ya msingi wanatakiwa kuwasiliana na
Viongozi wa ngazi zote kuanzia Kitongoji, Mtaa, Kijiji, Kata hadi ngazi
ya juu katika Halmashauri na Mkoa kuhusu masuala yote ya afya
yanayohitaji ushiriki wa wananchi ili kuwezesha viongozi hawa kuibeba
vizuri ajenda ya afya na kuwaelewesha wananchi.
Amewahimiza watumishi wa sekta ya
afya ngazi ya msingi kuhakikisha nao wanagonga milango ya viongozi hawa
na kuwapa ajenda za afya zinazohitaji ushiriki wa wananchi kwa kuwa
viongozi hao ndiyo wenye dhamana ya kwanza kabisa ya uongozi wa wananchi
hivyo, ni fursa kubwa endapo tutaendelea kushirikiana nao kwa karibu
zaidi.
“kufanya kazi pamoja na viongozi
wa serikali katika ngazi ya kitongoji, mtaa, kijiji, kata na ngazi
zingine zote za uongozi wa serikali na jamii kutasaidia kuharakisha
uelewa wa wananchi juu ya ajenda za afya na juhudi za serikali na
hatimaye, kuwezesha wananchi wengi zaidi kushiriki shughuli za kijamii
zinazolenga kuboresha afya ya jamii kwa ujumla ili, kujenga taifa lenye
afya bora kwa gharama nafuu kabisa maana kinga ni bora kuliko tiba”
Amesema Dkt. Gwajima
Amesema kuwa, viongozi wa ngazi ya
kitongoji, mtaa, kijiji, kata na ngazi zingine zote wakielewa vizuri
sera, miongozo na mipango mbalimbali ya serikali kuhusu afya ya jamii
wataendelea kuwa mabalozi na wasimamizi wazuri wa kufikisha ujumbe kwa
jamii kwa haraka na kuwezesha kuhamasisha jamii husika kushiriki katika
masuala ya afya yanayohitaji wananchi.
Dkt. Gwajima amewashukuru viongozi
mbalimbali wa serikali na jamii ngazi zote kwa ushirikiano wao wakati
wote katika kuibeba ajenda ya afya na kufanikisha mambo mengi ikiwemo
ujenzi na ukarabati wa vituo vya kutolea huduma za afya unaoendelea nchi
nzima na masuala yote ya elimu ya afya kwa jamii na kuhamasisha
wananchi kupata huduma za afya ya kinga.
Naye Mwenyekiti wa Kijiji cha
Mkoyo katika Halmashauri ya Jiji la Dodoma Bw. Henry Kubesi amesema
kuwa, yeye na uongozi wote wa Kijiji hicho wanaishukuru Serikali ya
Awamu ya Tano chini ya Uongozi wa Dkt. John Pombe Magufuli kwa
kuhakikisha Uongozi wa Ngazi ya Msingi unatambuliwa, unaheshimiwa na
unashirikishwa katika masuala mbalimbali ya kimaendeleo.
Amesema kuwa, ngazi ya msingi ndio
nguzo muhimu katika jamii kwa kuwa wao ndio wanawafikia wananchi
kiurahisi zaidi hivyo, tunaishukuru Serikali kwa kulitambua hilo ili
kuweza kuongea lugha moja ya kuleta maendeleo kwa jamii. Aidha, Bw.
Kubesi ameahidi kuwa yeye akipewa ajenda ya afya huwa anahakikisha mara
moja anaanza utekelezaji kwa kuwashirikisha Wenyeviti wa Vitongoji vyote
8 vya Kijiji chake ili waelewe na kupeleka ujumbe husika kwa wananchi.
Naye mhamasishaji wa afya ngazi ya
jamii Bi. Anastazia Konyanza amesema kuwa yeye ni mtaalamu anayehusika
na eneo la uelimishaji na uhamishaji wa wananchi hivyo, atashirikiana na
wataalamu wengine wote kuhakikisha wanaendelea kuhamasisha na
kuelimisha jamii yote ya Kijiji cha Mkoyo, Halmashauri ya Jiji la Dodoma
kuhusu masuala yote muhimu ya afya kama ambavyo wamekuwa wakifanya na
kupata ufanisi mkubwa ikiwemo kwenye eneo la Bima ya Afya ya Jamii.
Aidha katika ziara hiyo Dkt.
Dorothy Gwajima aliambatana na wataalam wa afya kutoka Wizara, Mikoa na
Halmshauri ya Jiji la Dodoma.
No comments:
Post a Comment