Naibu Waziri wa
Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu akizungumza na Wadau wa
Utalii nchini wakati wa Kongamano la Utalii lililofanyika mkoani Arusha
Baadhi ya Wadau wa Utalii nchini waliokuwa wamehudhuria
Kongamano la Utalii wakimsikiliza kwa makini Naibu Waziri wa Maliasili
na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu wakati akijibu baadhi ya hoja ambazo
zilikuwa zimewasilishwa na wadau hao ili ziweze kutafutiwa ufumbuzi.
Katibu Mkuu wa Maliasili nan Utalii, Prof. Adolf Mkenda
akizungumza na Wadau wa Utalii nchini wakati wa Kongamano la Utalii
liliofanyika mkoai Arusha kabla ya kumkaribisha Naibu Waziri wa
Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu kwa ajili ya kuzungumza
nao.
Katibu Mkuu wa Maliasili na Utalii, Prof. Adolf Mkenda (katikati) akizungumza na baadhi ya Wadau wa Utalii nchini mara baada ya kumalizika kwa Kongamano la Utalii lililofanyika mkoani Arusha
Katibu Mkuu wa Maliasili na Utalii, Prof. Adolf Mkenda (katikati) akizungumza na baadhi ya Wadau wa Utalii nchini mara baada ya kumalizika kwa Kongamano la Utalii lililofanyika mkoani Arusha
Kamanda wa Polisi wa Arusha, Jonathan Shana akizungmza na
Wadau wa Utalii nchini wakati akiwasilisha maada ya kuhusu namna
walivyojipanga kutumia vituo maalum vya kusimamishia magari yenye
watalii barabarani kwa ajili ya ukaguzi ili kuzuia usumbufu kwa watalii
wasiweze kukaa muda mrefu barabarani
Mwenyekiti wa Chama cha Waongoza Watalii Tanzania (TATO),
Wilbard Chamburo akizungumza mbele ya Naibu Waziri wa Maliasili na
Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu wakati akieleza baadhi ya adha ambazo
Wadau wa Utalii nchini wamekuwa wakikumbana nazo ili ziweze kutafutiwa
ufumbuzi
( PICHA NA WIZARA YA MALIASILI NA UTALII)
……….
Serikali kupitia
Wizara ya Maliasili na Utalii imesema itaendelea kupunguza adha
mbalimbali zinazowakabili Wadau wa Utalii likiwemo suala la polisi wa
usalama barabarani kusimamisha magari yenye watalii mara kwa mara.
Hayo yamesemwa na
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu alipokuwa
akizungumza na Wadau wa Utalii nchini katika kongamano la Utalii
lililofanyika mkoani Arusha.
Amesema Serikali kwa
kushirikiana na wadau wa utalii nchini imejenga vituo vya ukaguzi wa
magari vya utalii ili kupunguza usumbufu kwa watalii barabarani.
Amesema vituo hivyo vitashughulikia masuala ya msingi likiwemo suala madereva wenye watalii kupimwa kilevi.
Amesema mbali na kilevi, Vituo hivyo vitashughulikia vitendo vyote ya uhalifu watakavyofanyiwa watalii.
Aidha, Mhe.Kanyasu amesema lengo la Serikali ni kupunguza kero kwa watalii ili wafikie milioni mbili mwaka 2019.
Akizungumza kwenye
kongamano hilo, Mhe.Kanyasu amesema licha ya kujengwa vituo hivyo vya
ukaguzi lakini bado kuna kero ambazo zinafanyiwa kazi lengo likiwa ni
kuboresha sekta ya utalii.
Kwa upande wake,
Kamanda wa polisi mkoa wa Arusha, Jonathan Shana amewataka wadau wa
utalii kufuata sheria lakini akataka kupewa taarifa za polisi
wanaowakwaza.
“Nipigieni simu hata saa nane za usiku kwa askari wanawaomba rushwa nishughulike nao” Alisisitiza Shana.
Naye Mkuu wa mkoa wa Arusha Mhe.Mrisho Gambo amesema lengo la Arusha kuanzisha vituo vya ukaguzi magari ni kupunguza kero.
Amesema uwepo wa vituo hivyo vitafanya mazingira bora kwa watalii na wafanyabiashara.
Mwenyekiti wa Chama
cha Wasafirishaji Watalii (TATO) Wilbard Chambulo amesema ujenzi wa
vituo hivyo ni hatua muhimu ya kuwahakikishia watalii usalama wao pindi
wakiwa barabani pamoja na mali zao.
Kwa upande wake,
Katibu Mkuu wa Maliasili na Utalii, Prof.Adolf Mkenda amesema mkoa wa
Arusha ni mfano wa kuigwa kwa mikoa mingine kwa kujenga vituo hivyo ili
kupunguza kero kwa watalii.
No comments:
Post a Comment