Mkurugenzi mkuu wa Bohari ya Dawa
(MSD) Laurean Bwanakunu akitoa neno la utangulizi katika mkutano wa
tathmini ya utendaji kazi wa Bohari ya Dawa(MSD) unaofanyika Mjini
Bariadi mkoani Simiyu kwa siku tatu na lengo likiwa ni kujenga
ushirikiano na kufanya kazi kwa timu, Agosti 19, 2019.
Katibu Tawala wa mkoa wa Simiyu,
Bw. Jumanne Sagini akifungua mkutano wa tathmini ya utendaji kazi
wa Bohari ya Dawa(MSD) unaofanyika Mjini Bariadi mkoani Simiyu kwa siku
tatu na lengo likiwa ni kujenga ushirikiano na kufanya kazi kwa timu,
Agosti 19, 2019.
Katibu Tawala wa mkoa wa Simiyu,
Bw. Jumanne Sagini akifungua mkutano wa tathmini ya utendaji kazi
wa Bohari ya Dawa(MSD) unaofanyika Mjini Bariadi mkoani Simiyu kwa siku
tatu na lengo likiwa ni kujenga ushirikiano na kufanya kazi kwa timu,
Agosti 19, 2019.
Mkurugenzi wa Utawala na
Rasilimali watu wa Bohari ya Dawa(MSD), Victoria Mwanri Elangwa akitoa
taarifa katika mkutano wa tathimini ya utendaji kazi wa Bohari ya
Dawa(MSD) unaofanyika Mjini Bariadi mkoani Simiyu kwa siku tatu na
lengo likiwa ni kujenga ushirikiano na kufanya kazi kwa timu, Agosti
19, 2019.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu,
bw. Jumanne Sagini (wanne kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na
wakurugenzi wa idara mbalimbali na mameneja wa kanda wa Bohari ya Dawa
nchini(MSD) mara baada ya kufungua mkutano wao wa siku tatu, Agosti 19,
2019 ambao unafanyika kwa siku tatu Mjini Bariadi Mkoani Simiyu.
Baadhi ya wakurugenzi wa idara
mbalimbali na mameneja wa kanda wa Bohari ya Dawa nchini(MSD) wakiwa
katika mkutano wao wa siku tatu,uliofunguliwa na Katibu Tawala wa Mkoa
wa Simiyu, bw. Jumanne Sagini Agosti 19, 2019 ambao unafanyika Mjini
Bariadi Mkoani Simiyu.
Baadhi ya wakurugenzi wa idara
mbalimbali na mameneja wa kanda wa Bohari ya Dawa nchini(MSD) wakiwa
katika mkutano wao wa siku tatu,uliofunguliwa na Katibu Tawala wa Mkoa
wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini Agosti 19, 2019 ambao unafanyika Mjini
Bariadi Mkoani Simiyu.
Baadhi ya wakurugenzi wa idara
mbalimbali na mameneja wa kanda wa Bohari ya Dawa nchini(MSD) wakiwa
katika mkutano wao wa siku tatu,uliofunguliwa na Katibu Tawala wa Mkoa
wa Simiyu, bw. Jumanne Sagini Agosti 19, 2019 ambao unafanyika Mjini
Bariadi Mkoani Simiyu..
……………………..
Na Stella Kalinga, Simiyu RS
Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya dawa
(MSD) Laurean Bwanakunu amesema Bohari ya dawa inatarajia kuanza ujenzi
wa kituo cha mauzo na usambazaji dawa mkoani Simiyu ili kurahisisha
utoaji wa huduma kwa mkoa wa Simiyu na mikoa jirani.
Bwanakunu ameyasema hayo
Agosti 19,2019 katika ufunguzi wa mkutano wa tathmini ya utendaji kazi
wa menejimenti na mameneja wa kanda wa bohari ya dawa nchini.
lengo likiwa ni kujenga ushirikiano na kufanya kazi kwa timu.
Bwanakunu amesema wameamua
kufanyia mkutano wa tathimini mkoani Simiyu ili kuweza kujionea eneo la
ujenzi wa kituo cha mauzo ya dawa ikiwa ni moja ya kuongeza wigo mpana
wa utoaji huduma.
“Tutakuwa na mkutano wa siku tatu
hapa Simiyu kwa ajili kufanya tathmini ya utendaji kazi ulivyokuwa kwa
mwaka mzima, tutawafanyia tathmini wakurugenzi wote na wenyewe
watamfanyia Mkurugenzi Mkuu; lakini pia tutatumia fursa hii kutembelea
mahali tulipoamua kujenga bohari kwa kuwa tunatarajia kujenga bohari
hapa Simiyu”alisema Bwanakunu.
Akifungua mkutano huu, Katibu
Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini amesema maboresho ya
usambazaji wa dawa yaliyofanywa na Bohari ya Dawa (MSD) yameongeza
upatikanaji wa dawa mkoani Simiyu ambapo kwa sasa upatikananji wa dawa
ni zaidi ya asilimi 88.
Aidha, Sagini ametoa wito kwa
Taasisi zote za Umma zinazohitaji maeneo kwa ajili ya kujenga Ofisi zao
kufika mkoani Simiyu, ambapo amewahakikishia upatikanaji wa maeneo lengo
likiwa ni kuendelea kusogeza huduma mbalimbali karibu na wananchi.
Mkurugenzi wa Rasilimali watu wa
Bohari ya Dawa(MSD), Bibi. Victoria Elangwa amesema uwepo wa kituo cha
kusambaza dawa Simiyu kutapunguza umbali kwa Mkoa wa Simiyu na mikoa ya
Mara na Shinyanga kupata huduma za Bohari ambazo kwa sasa zinapatikana
Mwanza.
Ameongeza kuwa ujenzi wa Kituo
hicho unatarajia kuanza mara moja kwa kuwa tayari wataalam wameshaanza
kushughulikia masuala ya ukamilifu wa mazingira na baada kukamilisha
kazi hiyo atatafutwa mkandarasi kwa ajili ya kuanza ujenzi.
No comments:
Post a Comment