Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
akiwa katika picha ya pamoja na viongozi waku wa Nchi za Afrika na Japan
katika ufunguzi wa Mkutano wa Saba wa Tokyo International Conference on
Africa Development (TCAD 7) uliofanyika kwenye Ukumbi wa hoteli ya
Pacifico Yokohama nchini Japan, Agosti 28, 2019.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na
Rais waTogo, Faure Gnassingbe (kulia) wakipiga makofi katika ufunguzi wa
Mkutano wa Saba wa Tokyo International Conference on Africa Development
(TCAD7) uliofunguliwa na Waziri Mkuu wa Japan, Shinzo Abe kwenye Ukumbi
wa hoteli ya Pacifico Yokohama nchini Japan, Agosti 28, 2019
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na
viongozi Wakuu wa Nchi za Afrika wakifuatilia hotuba ya ufunguzi wa
Mkutano wa Saba wa Tokyo International Conference on Africa Development
(TCAD7) uliofunguliwa na Waziri Mkuu wa Japan, Shinzo Abe kwenye Ukumbi
wa hoteli ya Pacifico Yokohama nchini Japan, Agosti 28, 2019.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki, Profesa
Palamagamba Kabudi (kushoto) wakisikiliza hotuba ya ufunguzi wa Mkutano
wa Saba wa Tokyo International Conference on Africa Development (TCAD7)
uliofunguliwa na Waziri Mkuu wa Japan, Shinzo Abe kwenye Ukumbi wa
hoteli ya Pacifico Yokohama nchini Japan, Agosti 28, 2019.
(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
.................
*Asema nchi inahitaji teknolojia ya uhakika kufanikisha uchumi wa viwanda
WAZIRI
MKUU, Kassim Majaliwa amesema Tanzania inahitaji kuwa na tekinolojia
mpya na ya uhakika ili kufanikisha mkakati wa Seikali ya Awamu ya Tano
inayoongozwa na Rais Dkt. John Magufuli wa kukuza uchumi na kufikia wa
kati ifikapo 2015 kupitia sekta ya viwanda.
Ameyasema
hayo leo (Jumatano, Agosti 28, 2019) katika Mkutano wa Saba wa Tokyo
International Conference on African Development (TCAD 7) uliofunguliwa
na Waziri Mkuu wa Japan, Shinzo Abe kwenye ukumbi wa hoteli ya Pacifico
Yokohama nchini Japan.
Waziri
Mkuu ambaye amemwakilisha Rais Dkt. John Magufuli katika mkutano huo
amesema kwamba ujenzi na uendeshaji wa uchumi wa viwanda unahitaji
sana teknolojia kutoka ndani na nje ya nchi.
Amesema
ujezi wa uchumi wa viwanda utajikita katika matumizi ya malighafi
yanayopatikana nchini kama vile mazao ya kilimo, uvuvi, mifugo na madini
kwani Tanzania imebarikiwa kuwa na ardhi nzuri na hali ya
hewa inayofaa kwa kilimo pamoja na kuwa mali asili nyingi.
Waziri
Mkuu amesema hivi sasa Tanzania inaandaa miundombinu na huduma
mbalimbali zitakazofanya uwekezaji katika sekta ya viwanda ufanyike
katika mazingira yanayokidhi matarajio ya wawekezaji na wateja wao.
Ametoa
mifano wa ujenzi wa bwawa la kufua umeme la Nyerere katika mto Rufiji,
ujenzi wa Reli ya kisasa ya SGR , ujenzi wa barabara za lami, ufufuaji
wa Shirika la Ndege la Tanzania na upanuzi wa Bandari za Dar es salaam,
Mtwara na Tanga kuwa ni baadhi ya mipango ya Serikali ya kuifanya nchi
iwe na sifa na viwango katika suala la uwekezaji wa viwanda.
“Utaratibu
wa Blue Print ulioandaliwa na Serikali kwa lengo la kuondoa kero
mbalimbali katika uwekezaji na biashara nchini Tanzania ni mfano hai
unaodhihirisha kamba Serikali ya Awamu ya Tano imedhamiria kushirikiana
na sekta binafsi kujenga uchumi wa viwanda.”
Awali,akifungua
mkutano huo, Waziri Mkuu wa Japan, Shinzo Abe amesema katika kipindi
cha miaka mitatu iliyopita, uwekezaja uliofanywa Barani Afrika na
wawekezaji binafsi kutoka nchini Japan umefikia Dola za Marekani bilioni
20. Ameahidi kuwa uwekezaji huo utaendelea kuengezeka.
Viongozi
mbali mbali kutoa nchi za Afrika wamehudhuria mkutano huo akiwemo Rais
wa Kenya, Uhuru Kenyatta, Rais wa Rwanda, Paul Kagame, Rais Uganda,
Yoweri Musseveni pamoja na Waziri Mkuu wa Mauritius, Pravini Kumar.
Waziri
Mkuu ameambatana na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika ya
Mashariki, Profesa Palamagamba Kabudi na viongozi mbalimbali kutoka
Serikali ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
No comments:
Post a Comment