**************
Na.Alex Sonna,Dodoma
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais
TAMISEMI, Mhe Selemani Jafo ametangaza matokeo ya uchaguzi wa wanafunzi
kujiunga na kidato cha tano awamu ya pili.
Zoezi la uchaguzi wa wanafunzi hao
waliopangwa kidato cha tano limefanyika kwa kuzingatia jumla ya
wanafunzi wavulana 1,861 waliokua wamebaki kwenye uchaguzi wa awamu ya
kwanza.
Kati ya wanafunzi 1,861
waliochaguliwa ni wanafunzi 1,674 na wanafunzi 187 wamekosa tahasusi
hivyo hawajachaguliwa. Kati ya wanafunzi waliochaguliwa 178 wamepangiwa
tahasusi za Sayansi na Hisabati na 1,496 wamepangiwa Sanaa na Biashara.
” Niwashauri waliokosa nafasi
waombe kozi mbalimbali katika vyuo vya elimu ya ufundi vinavyotambulika
na NACTE, lakini pia waliochaguliwa wanapaswa kuripoti Septemba 2 hadi
16 mwaka huu watakaochelewa watakua wamepoteza nafasi, ” amesema Waziri
Jafo.
No comments:
Post a Comment