Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
akisalimiana na Waziri Mkuu wa Mauritius, Pravind Kumar kabla ya
mazungumzo yao kwenye Ukumbi wa Maonyesho wa Pacifico Yokohama nchini
Japan, Agosti 28, 2019. Wote wawili wako Japan kuhudhuria Mkutano wa
Saba wa Tokyo International Conference on Africa Development -TICAD 7
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
akizungumza na Waziri Mkuu wa Mauritius, Pravind Kumar kwenye ukumbi wa
Maonyesho wa Pacifico Yokohama nchini Japan, Agosti 28, 2019. Wate
wawili wanahudhuria Mkutano wa Saba wa Tokyo International Conference on
Africa – TICAD 7.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
akizungumza na Waziri Mkuu wa Mauritius, Pravind Kumar kwenye ukumbi wa
Maonyesho wa Pacifico Yokohama nchini Japan, Agosti 28, 2019. Wate
wawili wanahudhuria Mkutano wa Saba wa Tokyo International Conference on
Africa – TICAD 7. Kushoto ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Afrika ya Mashariki, Profesa Palamagamba Kabudi
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki, Profesa
Palamagamba Kabudi (wa pili kulia) wakiwa katika picha ya pamoja na
maofisa kutoka Ubalozi wa Tanzania nchini Japan, Hifadhi za Taifa
Tanzania(TANAPA) na Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) wakati alipotembelea
banda la maonyesho la Tanzania kwenye Ukumbi wa Maonyesho wa Pacifico
Yokohama nchini Japan, Agosti 28, 2019.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
akizungumza na maofisa kutoka Ubalozi wa Tanzania nchini Japan, Hifadhi
za Taifa Tanzania (TANAPA) na Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) wakati
alipotembelea banda la maonyesho la Tanzania kwenye Ukumbi wa Maonyesho
wa Pacifico Yokohama nchini Japan, Agosti 28, 2019. (Picha na Ofisi ya
Waziri Mkuu)
…………………..
WAZIRI MKUU AWAKARIBISHA WAWEKEZAJI KUTOKA MAURITIUS
WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa
amewakaribisha wafanyabiashara na wawekezaji kutoka nchini Mauritius
waje washirikiane na Watanzania katika uwekezaji kwenye maeneo
mbalimbali yakiwemo ya utalii, viwanda vya sukari, nguo na bidhaa za
uvuvi.
Ametoa kauli hiyo leo, (Jumatano,
Agosti 28, 2019) wakati alipokutana na kufanya mazungumzo na Waziri Mkuu
wa Mauritius, Pravind Kumar katika Ukumbi wa Monyesho wa Pasfico
Yokohama nchini Japan.
Waziri Mkuu amesema nchi ya
Mauritius ina uwezo mkubwa sana katika uzalishaji wa sukari na wanayo
nafasi kubwa ya kushirikiana na Watanzania katika kilimo cha miwa na
ujenzi wa viwanda vya sukari na Tanzania ina ardhi nzuri na
kubwa inayofaa kwa kilimo hicho pamoja na soko kubwa ndani na nje ya
nchi.
Amesema uwekezaji katika sekta ya
sukari utasaidia kuunga mkono juhudi za Serikali ya Awamu ya Tano
inayoongozwa na Rais Dkt. John Magufuli za kuhakikisha inamaliza tatizo
la upungufu wa sukari nchini.
Akizungumzia kuhusu sekta ya
utalii, Waziri Mkuu amesema Mauritius imefanya vizuri sana katika utalii
na hasa ule wa kutumia fukwe za bahari. “Kwa vile Tanzania inazo fukwe
za bahari na maziwa naamini ushirkiano katika eneo hilo utatuletea
tija.”
Kuhusu usafiri wa anga, Waziri
Mkuu amesema kuwa wakati umefika sasa kwa Shirika la Ndege la Tanzania
(ATCL) kuanza safari za kwenda Mauritius ili kuvutia watalii wengi
wanaokwenda Mauritius kufanya utalii wa fukweni waje pia nchini.
Kuhusu viwanda vya nguo, Waziri
Mkuu amewahamasisha wafanyabiashara wa Mauritius kuwekeza nchini hasa
katika viwanda vya nyuzi za pamba na nguo kwani Tanzania hivi sasa
inazalisha pamba nyingi na yenye ubora wa juu.
“Watanzania wengi wameishia
kuwekeza kwenye viwanda vya kuchambua pamba hivyo wanalazimika kuuza
pamba yao nje ya nchi na wenzetu Mauritius wameenda mbali zaidi kwani
wana viwanda vya nguo na viwanda vya nyuzi. Kwa sasa Serikali ya
Tanzania imeweka mkakati wa kujenda viwanda vya nguo ili kuongeza tija.”
Amesema kwa sasa wamekuabaliana na
Waziri wa Mkuu huyo wa Mauritius kuwakutanisha Mawaziri wa viwanda na
Biashara wa Mauritius na Tanzania wakae pamoja kwa ajili ya kufanya
mazungumzo yenye lengo la kuwashawishi wafanyabiashara wa Mauritius waje
wawekeze katika viwanda vya nguo na nyuzi nchini.
Kadhalika,Waziri Mkuu amezungumzia
kuhusu sekta ya Uvuvi, ambapo amesema Tanzania ina eneo kubwa la bahari
na maziwa linalofaa kwa uvuvi wa kibiahara na lina samaki wengi lakini
wanavuliwa kwa kiwango kidogo sana kutokana na uwekezaji duni katika
sekta hiyo.
Amesema ingawa Serikali ya Awamu
ya Tano inaandaa mazingira ya kufufa kampuni za uvuvi nchini, bado
nafasi ipo kwa wawekezaji kutoka nje ya nchi hasa nchini Mauritius kuja
Tanzania kuwekeza kwenye uvuvi.
Kwa upande wake, Waziri Mkuu wa
Mauritius, Pravind ameihakikishia Serikali ya Tanzania kuwa nchi yake
iko tayari kufanya mazungumzo na Wizara na Taasisi zinazohusika na
masuala ya uwekezaji nchini ili kupata taarifa za kutosha
zitakazomwezesha kuwashawishi wafanyabiashara wa nchi yake waje wawekeze
nchini.
Mazungumzo hayo pia yalihudhuriwa
na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikikiano wa Afrika ya Mashariki,
Profesa Paramagamba Kabudi na viongozi kutoka Serikali ya Muungano wa
Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
No comments:
Post a Comment