Mateso Juma( kulia) mwenye ulemavu wa ngozi ,
mkazi wa kijiji cha Kijiji cha Ifucha katika Halmashauri ya Tabora mjini, akiwa
ameshikilia kifaa cha umeme tayari( UMETA) baada ya kukabidhiwa na Naibu Waziri
wa Nishati, Subira Mgalu( kulia). Serikali iliagiza kuwa licha ya UMETA kugaiwa
bure kwa wateja 250 wa mwanzo watakaounganishiwa umeme,kipaumbele kiwe kwa
wazee wasiojiweza, wajane, na walemavu.
Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu akizungumza
na wakazi wa kijiji cha Itundaukulu wilayani Uyui, mkoani Tabora (hawapo
pichani) Naibu Waziri yupo mkoani Tabora kwa ziara ya kikazi ya kukagua
utekelezaji wa mradi wa usambazaji umeme vijijini REA.
Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu(kutoka
kulia)akipokea barafu(ice cream) na soda baridi kutoka kwa mama mjasiriamali (kushoto)
anayefanya biashara hiyo baada ya kufungiwa umeme wa REA katika kijiji cha
Simbo wilayani Uyui, mkoani Tabora.
.......................
Zuena
Msuya, Tabora,
Naibu wa Waziri wa Nishati, Subira Mgalu amewataka
wakandarasi ambao wanadhani hawatakamilisha ama kuchelewesha kazi ya usambazaji
wa umeme vijijini kutokana na changamoto mbalimbali , ni vyema
kazi hizo wakapatia wakandarasi wenye uwezo ili miradi hiyo ikamilike kwa
wakati.
Akizungumzia kazi ya kusambaza umeme vijijini
katika maeneo aliyotembelea mkoani Tabora, Julai 16, 2019, Mgalu alisema kuwa
kuna baadhi ya wakandarasi wamekuwa
hawaendani na kasi inayotakiwa katika kutekeleza mradi huo,na kwamba
wamekuwa na sababu nyingi za kujitetea licha ya awali kuonyesha kuwa na uwezo
wa kufanya kazi hizo.
Aliweka bayana kuwa kasi ndogo ya utekelezaji
mradi huo ikilinganishwa na kipindi kilichowekwa kuukamilisha, inaonyesha wazi
kabisa kuwa wakandarasi hao hawatamaliza kazi hiyo kwa wakati uliopangwa na
hivyo kurudisha nyuma juhudi za serikali katika kutimizma yake ya kuwapatia
umeme wananchi wote .
“Kuna wakandarasi ambao walianza vizuri lakini
sasa wanasuasua kutokana na changamoto mbalimbali, usikumbatie kazi igawe kwa
wenye uwezo, usisubiri jumba bovu likuangukie,Serikali wala Wizara ya Nishati
hatutakubali kurudishwa nyuma, ukishindwa ama kuchelewesha sheria itachukuwa
mkondo wake kwa kuwa fedha nyingi zimetengwa kwa ajili ya kuwapatia wananchi
umeme,”alisisitiza Mgalu.
Katika ziara hiyo, Naibu Waziri Mgalu aliwasha
umeme katika baadhi ya nyumba za kijiji cha Itundaukulu pamoja na Zahati ya
kijiji hicho, pia katika shule ya msingi ya Simbo pamoja na kuwasha umeme
katika baadhi ya nyumba katika Kijiji cha Simbo wilayani Uyui, Tabora.
Aidha alikemea tabia ya baadhi ya wakandarasi
wanaondoka katika eneo la mradi mara baada ya kijiji husika kuwashwa umeme,
badala ya kubaki na kuendelea na kazi ya kuwaunganishia wananchi wengine
waliokwisha lipitia huduma hiyo, jambo ambalo limekuwa likilalamikiwa sana na
wananchi.
Aliwagiza viongozi wa Serikali za mitaa na vijiji
kuwa walinzi wa wakandarasi hao, na wahakikishe kazi ya uunganishwaji wa
wananchi inaendelea, na endapo mkandarasi atalazimika kuondoka eneo la mradi, basi kuwepo na sababu maalum na watoe taarifa kwa uongozi wa
Vijiji.
“Nasikitishwa sana na baadhi ya wakandarasi,
wakiona umeme umeshawashwa katika kijiji na wao wanaondoka eneo hilo, nawaeleza
ukweli wakadarasi timizeni wajibu wenu kulinga na makubalino ya mikataba na
kutekeleza maagizo mbalimbali mnayopewa, tabia hii hatutaivumilia, fanyeni kazi
kwa mujibu wa mikataba muwatendee haki watanzania na taifa kwa ujumla,” alisisitiza Mgalu.
Aidha amefafanua kuwa bei ya kuwaunganishia
wananchi umeme vijijini ni shilingi 27,000 tu,
bei hii itandelea kutumika hata pale Mradi wa REA utapokamilika na kazi
hiyo wakapewa Shirika la Umeme nchini (TANESCO) kuendelea na kazi hiyo, hivyo
wanachi wote waendee kuunganishwa lengo ni kuwafikia wananchi wote.
“Hapo awali ilikuwa ,mara baada ya mradi wa REA
kukamilika katika eneo husika kazi ya uunganishaji wananchi inakabidhiwa kwa
Tanesco, na bei ya kulipia gharama hiyo ilikuwa ni zaidi ya 170,000/=, sasa
serikali imesema hapana bei ibaki ileile shilingi 27,000 kwa wananchi wote wa
vijijini,” alisema Mgalu
Vilevile aliwatoa hofu wananchi kuwa, mara baada
ya mradi wa REA kukamilika, serikali imeanzisha mradi mwingine wa ujazilizi
ambao utakuwa ukiendelea na kazi ya kusambaza umeme kwa wananchi ambao
hawakuweza kufukiwa na REA, na mradi huyo utahusisha mikoa mbalimbali.
No comments:
Post a Comment