Mkuu wa Wilaya ya
Songwe Samuel Jeremia Opulukwa (kulia) akisikiliza maelezo kuhusu chumba cha
upasuaji kutoka kwa Mganga Mkuu wa Mkoa
wa Songwe Dkt Kheri Kagya (katikati) wakati alipotembelea Kituo cha Afya Isansa
Wilaya ya Mbozi ili kujifunza kwa vitendo ukamilishaji wa Vituo vya Afya,
Kushoto ni Mganga Mkuu wa Wilaya ya Songwe Humphrey Masuki.
Mkuu wa Mkoa wa
Songwe Brigedia Jenerali Nicodemus Mwangela na Mkuu wa Wilaya ya Songwe Samuel
Jeremia Opulukwa wakisikiliza maelezo kuhusu chumba cha kuhifadhia maiti kutoka
kwa Mganga Mkuu wa Mkoa wa Songwe Dkt Kheri Kagya wakati wa ziara Katika Kituo
cha Afya Isansa.
.................
Mkuu wa Mkoa wa
Songwe Brigedia Jenerali Nicodemus Mwangela ameutaka Uongozi wa Wilaya ya
Songwe Kuongeza jitihada na nguvu Zaidi katika kukamilisha ujenzi wa Vituo vya
Afya vya Magamba na Mbuyuni pamoja na ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya hiyo.
Brigedia Jenerali
Mwangela ameyasema hayo leo mara baada ya kupokea taarifa ya mpango wa
ukamilishaji wa miradi hiyo kutoka kwa uongozi wa Wilaya ya Songwe na kisha
kuwapeleka katika Mradi uliokamilika wa Kituo cha Afya ya Isansa Wilaya ya
Mbozi na ujenzi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa ili waweze kujifunza kwa vitendo.
“Baada ya kupokea
taarifa yao ya ukamilishaji wa miradi ya ujenzi ya Wilaya ya Songwe, nimeona ni
vema waje wajifunze kwa vitendo kwakuwa ukamilishaji wa miradi yao ya ujenzi
umekuwa ukienda taratibu mno pia wajifunze kufanya kazi za serikali kwa
teamwork”, amesisitiza Brigedia Mwangela.
Brigedia Jenerali
Mwangela amesema miradi ya ujenzi ya Wilayani humo mingi bado haijakamilika na
muda umewaishia hivyo kwa ziara hiyo wajifunze kuwa wenzao wamekalisha miradi
hiyo na inahudumia wananchi na pia kazi
za serikali zinapaswa kukamilika kwa muda.
“Wao vituo
vimechelewa sana kukamilika wamekuja wajifunze na waongeze nguvu ili waweze
kukamilisha mapema, wameniambia wamejifunza kitu lakini pia wanapaswa kutambua
kuwa kazi za serikali unapewa fedha, vifaa na muda maalumu wa kukamilisha”,
ameeleza Brigedia Mwangela
Kwa upande wake Mkuu
wa Wilaya ya Songwe Samuel Jeremia Opulukwa amesema wamejifunza kuwa wenzao
wameweza kumalizia ujenzi wa Vituo vya Afya kwa viwango vizuri na wao watafanya
hivyo ili wananchi waanze kupata huduma.
“Tumeona wenzetu
wamekamilisha vizuri nasi tutajitahidi kukamilisha vizuri vituo vyetu ya Afya vya
Magamba na Mbuyuni pamoja na hospitali ya Wilaya ili tuweze kutoa huduma kwa
wananchi wetu ifikapo Julai 30, 2019”, amesema Opulukwa.
Naye Mganga Mkuu wa
Wilaya ya Songwe Humphrey Masuki amesema wamejionea namna nzuri ya umaliziaji
wa vituo vya Afya ili viwe na ubora na kutoa mfano kuwa wamejifunza namna nzuri
ya upangaji makabati katika chumba cha kuhifadhi maiti na upangaji wa makabati
na meza katika jengo la maabara.
No comments:
Post a Comment