SERIKALI YAZIDI KUPAMBANA NA RUSHWA NCHINI
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani na
Ushirikiano Afrika Mashariki, Dkt Damas Ndumbaro, akizungumza wakati wa
kongamano la kujadili maswala ya rushwa ikiwa ni siku ya mapambano dhidi
ya rushwa kwa nchi za umoja wa Afrika uliofanyika jijini Dodoma.
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais,
Menejimenti yaUtumishi wa Umma, Dkt Merry Mwanjelwa, akizungumza wakati
wa kongamano la kujadili maswala ya rushwa ikiwa ni siku ya mapambano
dhidi ya rushwa kwa nchi za umoja wa Afrika uliofanyika jijini Dodoma.
Katibu Mtendaji wa Bodi ya Umoja wa
Afrika ya Mapambano dhidi ya Rushwa, Cherity Nchimunya, akizungumza
wakati wa kongamano la kujadili maswala ya rushwa ikiwa ni siku ya
mapambano dhidi ya rushwa kwa nchi za umoja wa Afrika uliofanyika jijini
Dodoma.
Mkaguzi na Mdhibiti wa hesabu za
Serikali(CAG) Profesa Mussa Assad, akifuatilia mawasilisho ya mtoa mada
wakati wa mjadala wa namna ya kupambana na rushwa nchini Tanzania,
kongamano lililofanyika jijini Dodoma.
…………………….
Na EZEKIEL NASHON, DODOMA.
SERIKALI imesema imeweka nguvu na
msisitizo mkubwa katika kupambana na rushwa, kwani rushwa imekuwa
ikirudisha sana juhudi za kupambana na umasikini jikomboa kiuchumi na
kupoteza haki za watu wengi katika jamii.
Hayo yamebainishwa Jijini Dodoma, na
naibu waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt
Damasi Ndumbaro, wakati akizungumza kwenye kongamano la siku maalumu ya
mapambano dhidi rushwa kwa nchi za umoja wa Afrika(AU).
Ambapo umefanyika jijini Dodoma, na
kutumia siku hiyo kama ni siku ya kuhamasisha, kuwapa elimu, na
kuwajengea uwezo vijana namna ya kupambana na rushwa, ambapo kongamano
hilo limehusisha wanafunzi wa vyuo vikuu, na wanafunzi wa sekondari na
waandishi wa habari.
Dkt Ndumbaro amesema kama nchi wameweka
mkazo mkubwa kuhakikisha wanapambana na rushwa, na kwa kuhakikisha hayo
yanafanikiwa Tanzania imejiunga na kusaini mikataba na itifaki za
kupambana na rushwa kimataifa na kikanda.
“Tanzania kwa kutambua umuhimu wa
ushirikiano katika kupambana na rushwa imesaini na kuridhia mikataba na
itifaki za kupambana na rushwa kimataifa na kikanda, hii ni pamoja na
mikataba ya umoja wa kimataifa wa kupambana na rushwa” amesema dkt
Ndumbaro.
Ametaja baadhi ya mikataba hiyo ni
mkataba wa umoja wa kimataifa wa kupambana na rushwa(UNCAC,2003),
itifaki ya nchi za kusini mwa bara la Afrika ya kupambana na rushwa(SADC
Protocol Against Corruption, 2001, na mkataba wa mapambano dhidi ya
rushwa kwa nchi za afrika(AU Convention on preventing and Combating
Corruption, 2003).
Nyingine ni mwanachama wa shirikisho la
taasisi za mapambano dhidi ya rushwa barani Afrika(AAACA) jumuiya ya
madola(CAACA) pamoja na Afrika mashariki( EAAACA) amesema Tanzania pia
ni mwenyeji wa bodi ya umoja Afrika ya ushauri kuhusu maswala ya rushwa
ambapo makao makuu yake yapo Arusha.
Amesema kwa mkazo huo tafiti zinaonyesha kuongezeka kwa kiwango cha utawala bora kwa kupata asilimia 58.5/100.
“Tanzania imeonekana kuongeza kiwango cha
utawala bora kwa kupata alama 58.5/100,na kuwa nchi ya kumi na moja11
kati ya nchi 54 kwa mwaka 2018 ikilinganishwa na 2017 ambapo ilipata
alama 57.5/100 na kuwa nchi ya 17 katika bara la Afrika kwa mujibu wa Mo
Ibrahim Index of African Governance” amesema.
Aidha amewataka TAKUKURU kuhakikisha
wanafanya kazi kwa uwazi na waminifu ili kukomesha vitendo vya rushwa
hapa nchini na kuwa na utawala bora.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa mkuu wa
TAKUKURU CP, Diwani Athumani, amesema wao wamekuwa wakifanya kazi na
kuhakikisha wanakomesha vitendo vya rushwa hapa nchini.
Amesema wamekuwa wakifanya kazi na
kuhakikisha taarifa zinazopatikana zinawafikia wananchi ili waweze
kujifunza kuhusu maswala ya rushwa na kuhakikisha mali ambazo
hazikupatikana kwa halali zinarudishwa serikalini kwa mujibu wa sheria.
Aidha amesema moja ya changamoto ambazo
zinaikabili taasisi hiyo katika utendaji wa kazi ni pamoja na
kukosekana kwa ushahidi pindi kesi zinapokuwa mahakamani pamoja na
ufinyu wa bajeti katika taasisi hiyo.
“Moja ya changamoto ambazo zinaikabili
taasisi hii ni pamoja na mashahidi kushindwa kufika kutoa ushahidi pindi
kesi zinapokuwa mahakamani kesi nyingi zinafutwa kutokanna na kukosa
ushahidi, pamoja na ufinyu wa bajeti katika kutekeleza majukumu yetu”
amesema.
No comments:
Post a Comment