Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania, Hamza Johari akifungua mkutano wa wadau kujadili Usalama wa Anga (CAPSCA) katika viwanja vya ndege uliofanyika ofisi za Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) jijini Dar yes Salaam. Picha zote na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG.
Wadau wanaounda Kamati ya Kitaifa ya Usalama wa Anga katika viwanja vya ndege (CAPSCA) wakimsikiliza mkurugenzi wa TCAA wakati akifanya ufunguzi.
Mkurugenzi wa huduma za kinga Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Leonard Subi akizunguza na wanahabari wakati akitoa ufafanuzi jinsi serikali iliyojipanga kukabiliana na magonjwa ya kuambukiza katika viwanja vya ndege na maeneo yote ya mpakani ikiwemo maeneo ya Bandari.
Na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG.
Serikali imejipanga kukabiliana na magonjwa yanayoambukiza katika viwanja vya ndege nchini.
Imenunua mashine za kupima joto (Thermo Scanner) 115 ambapo 15 zile zinaweza kupima abiria wengi wanaoingia kwa mpigo katika viwanja vya ndege vya kimataifa.
Hayo yamezungumzwa na Mkurugenzi wa huduma za kinga Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt.Leonard Subi wakati akitoa tathimini wakati wa mkutano wa wadau kujadili Usalama wa Anga (CAPSCA) katika viwanja vya ndege uliofanyika ofisi za Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) jijini Dar yes Salaam.
Dkt. Leonard Subi amesema kwasasa wameshafanya ukaguzi kwa Kushirikiana na Shirika la Afya Duniani (WHO) katika viwanja vya ndege vya kitaifa na kubaini mapungufu kadhaa yanayotakiwa kufanyiwa kazi ili kukidhi vigezo waliojiwekea.
"Tulifanya tathimini ya kwanza 2015 na kubaini viwanja vya kitaifa vipo chini ya kiwango walipata alama 50, ila ukaguzi tuliofanya tena 2018 umeonyesha matokeo chanya ya alama 73 katika masuala ya kiafya kwa wasafiri na watoa huduma japo bado tunasisitiza usimamizi uongezeke," amesema Dkt. Subi.
Ameongeza kuwa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imejipanga vyema kukabilia na magonjwa hayo kwa vile uwanja mpya umefungwa vifaa vya kisasa ambavyo unaweza kutamua kwa haraka wagonjwa wenye magonjwa ya kuambukiza.
Ameongeza kuwa wamejengea uwezo wafanyakazi wanaofanyakazi katika viwanja vya ndege na wameweza kujenga kituo katika hospitali ya Temeke na Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa ajili ya kukabilia na magonjwa ya kuambukiza na mlipuko pindi mgonjwa anapobaika.
Amemaliza kwa kuomba ushirikiano kwa wafanyakazo wote wanaofanyakazi katika uwanja wa ndege ili kuweza kukabiliana na magonjwa ya maambukizi katika viwanja vya kimataifa pia ameiomba jamii kuacha kuwahifadhi wahamiaji haramu ili kuweze kulinda afya zao maana unaweza kumuhifadhi akawa amekuja na magonjwa ya kuambukiza akaiathiri familia yako.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania, Hamza Johari amesema mpaka sasa wameshaweza kufanya tathimini katika viwanja vitatu vya kimataifa ikiwemo Uwanja vya Kitaifa ni Juliusi Kambarage Nyerere, Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume wa Zanzibar, Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere wa Dar es Salaam na Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro na vile visivyo vya kitaifa ikiwemo Uwanja wa Ndege wa Mwanza na Songwe, Mbeya.
Ameomba wadau wote wanaounda kamati ya Kitaifa ya Usalama wa Anga ikiwemo Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Wizara ya Maliasili na Utalii, Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi na Ofisi ya Waziri Mkuu Kitengo cha Maafa na wadau wengine wote wanaohusika na masuala ya usalama.anga na afya kuendelea kushirikiana ili kuweza kupambana na viwanja vya ndege na mipaka ya nchi ili kuzuia magonjwa ya kuambukiza yanayoweza tokea kutokana na wageni au wahamiaji haramu.
"Najua mnatambua lililotpkea mwaka 2018 lililotokea kule DRC Kongo ambapo aliuwawa dokta ambaye alikuwa akishughukia wagonjwa wa Ebola najua linauma ila ni vyema tusivunjike moyo tuendelee kupambana zaidi," amesema.
No comments:
Post a Comment