SERIKALI YAKARIBISHA WAWEKEZAJI WA VIWANDA VYA NGOZI
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa
amewakaribisha wawekezaji na wafanyabiashara mbalimbali kutoka Misri
ikiwemo kampuni ya Cairo for Investment and Development inayoshughulika
na usimamizi wa kiwanda cha ngozi waje kuwekeza nchini Tanzania.
Ametoa kauli hiyo jana (Jumanne, Julai 9,
2019) alipotembelea kiwanda kikubwa cha ngozi cha Robbiki kilichoko
katika mkoa wa Sharkianchini Misri, ambapo alitumia fursa hiyo
kuwakaribisha wawekezaji hao waje wawekeze nchini kwani kuna malighafi
za kutosha.
Waziri Mkuu ambaje jana alikuwa katika
siku ya pili ya ziara yake ya kikazi nchini Misri alisema Tanzania
inamifugo mingi hivyo inahitaji wawekezaji watakaojenga viwanda vya
kuchakata bidhaa mbalimbali zitokanazo na mifugo hiyo ikiwemo ngozi.
Alisema Serikali ya Awamu ya Tano
inayoongozwa na Rais Dkt. John Magufuli imeboresha mazingira ya biashara
na ya uwekezaji pamoja na kusimamia uwajibikaji kwa watumishi wa umma,
hivyo Tanzania ni mahali bora na salama kwa wawekezaji na
wafanyabiashara.
Kwa upande wake,Mwenyekiti
wa Kampuni ya Cairo for Investment and Development ya nchini Misri,
ambayo inasimamia kiwanda cha ngozi cha Robbiki, Yasser Mohamed Ahmed Al
Maghraby alisema kiwanda hicho kinauhitaji mkubwa wa ngozi kutoka
Tanzania.
Awali, Waziri Mkuu
alitembelea mradi mkubwa wa mabwawa ya kufugia samaki, mradi wa upanuzi
wa awamu ya pili ya mfereji wa suez canal, ambapo aliipongeza Serikali
ya Misri kwa ujenzi wa mradi huo mkubwa kwa kutumia fedha za ndani (Dola
bilioni 8.2).
No comments:
Post a Comment