ALIYELAZWA MWAKA MMOJA MLOGANZILA APATIWA MASHINE YA KUPUMUA
Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya
Hospitali ya Taifa Muhimbili Prof. Charles Majinge (kushoto) akimpatia
msaada wa mashine ya kusaidia kupumua (Oxygen Concentrator) Bw. Hamad
Awadhi ambaye alilazwa kwa muda wa mwaka mmoja katika Hospitali ya
Mloganzila.
Mkurugenzi wa Huduma za Uuguzi MNH-
Mloganzila Redemptha Matindi (aliyevaa gauni la bluu) akitoa maelezo
namna mashine ya oxygen inavyounganishwa ili iweze kutumika kwa mgonjwa,
anayemfuatia ni Prof. Charles Majinge, kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa
Huduma za Tiba Dkt. Mohamed Mohamed, kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa
MNH Prof. Lawrence Museru.
Prof. Lawrence Museru (wa pili kushoto)
akitoa maelezo kwa Mwenyekiti wa bodi ya wadhamini MNH Prof. Majinge (wa
pili kuli) kuhusu ununuzi wa mashine ya kusaidia kupumua (Oxygen
Concentrator) ambayo imegharimu shilingi milioni tatu na nusu, kushoto
ni Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Mloganzila Dkt. Julieth
Magandi.
Dkt. Daktari Bingwa wa magonjwa ya ndani
MNH- Mloganzila Dkt. Patricia Munseri (kulia) akizungumzia kuhusu
matibabu aliyopatiwa Bw. Awadhi kwa kipindi chote alichokua amelazwa
hospitalini.
Bw. Hamadi Awadhi akitoa neno la shukrani
kwa uongozi wa Muhimbili-Mloganzila kwa huduma aliyoipata na kwa
kumpatia msaada ambao utamuwezesha kuendelea na shughuli zake za
kawaida.
Mashine ya kusaidia kupumua (Oxygen Concentrator) ambayo amepatiwa msaada Bw. Hamad Awadhi.
……………………..
Hospitali ya Taifa Muhimbili- Mloganzila,
imempatia msaada wa mashine ya kusaidia kupumua (Oxygen Concentrator)
Bw. Hamad Awadhi kutokana na matatizo yake ya afya ambayo yanamlazimu
kutumia mashine ya oxygen muda wote ili aweze kupumua.
Akikabidhi msaada huo Mwenyekiti wa Bodi
ya Wadhamini wa Hospitali ya Taifa Muhimbili-MNH-Prof. Charles Majinge
amesema hospitali imempatia msaada Bw. Awadhi kwa lengo la kuokoa maisha
yake sanjari na kuimarisha afya yake lakini pia kumuwezesha kuendelea
na shughuli zake za kawaida ili kutokua tegemezi kutokana na hali yake.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa
MNH Prof. Lawrence Museru ameeleza kwamba mashine hiyo inathamani ya
shilingi milioni tatu na nusu imenunuliwa na Hospitali ya Mloganzila
ambapo wataalam wamempatia mafunzo Bw. Awadhi namna ya kuitumia na
kuitunza ipasavyo.
Prof. Museru amemtaka Bwan. Awadhi
kuitunza na kuitumia vema mashine hiyo kama ambavyo ameelekezwa na
wataalam ili afya yake itakapoimarika iweze kusaidia watanzania wengine.
“Hospitali imekupatia msaada wa mashine
hii ya kukusaidia kupumua- kwa lengo la kuhakikisha afya yako inaimarika
zaidi hivyo tunaomba uitunze na utakapopona kabisa utairejesha
hospitali ilituwasaidie wengine” amesema Prof. Museru.
Naye Daktari Bingwa wa magonjwa ya ndani
MNH- Mloganzila Dkt. Patricia Munseri amesema, Bw. Awadhi kwa muda wote
aliokuwepo hospitalini ameishi kwa kutegemea mashine ya oxygen ambayo
inamsaidia kupumua ambapo kwa siku alikua akitumia gesi wastani wa lita
5,760.
Bw. Hamad Awadhi alifikishwa Hospitali ya
Taifa Muhimbili- Mloganzila Julai 9 mwaka 2018 na kuruhusiwa Julai 9
mwaka 2019 baada ya afya yake kuimarika.
No comments:
Post a Comment