Baadhi ya viongozi wa dini, ,
viongozi wa asasi zisizosa Kiserikali na wawakilishi wa vijna , wanawake
na watu wenye ulemavu wakifuatilia hotuba ya Mwenyekiti wa Tume ya
Taifa ya Uchaguzi, Mhe Jaji wa Mahakama ya Rufaa, Semistocles
Kaijage(hayupo pichani) wakati akifungua Mkutano wa wadau wa Uchaguzi
Mkoani Simiyu, Julai 20, 2019 Mjini Bariadi.
Baadhi ya viongozi wa dini, , viongozi wa asasi zisizosa Kiserikali na
wawakilishi wa vijna , wanawake na watu wenye ulemavu wakifuatilia
hotuba ya Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe Jaji wa Mahakama
ya Rufaa, Semistocles Kaijage(hayupo pichani) wakati akifungua Mkutano
wa wadau wa Uchaguzi Mkoani Simiyu, Julai 20, 2019 Mjini Bariadi.
Baadhi
ya viongozi wa Vyama vya siasa wakifuatilia hotuba ya Mwenyekiti wa
Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe Jaji wa Mahakama ya Rufaa, Semistocles
Kaijage(hayupo pichani) wakati akifungua Mkutano wa wadau wa Uchaguzi
Mkoani Simiyu, Julai 20, 2019 Mjini Bariadi.
Afisa
TEHAMA Mwandamizi kutoka Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Bw. Frank Mhando
akiwasilisha mada katika mkutano wa wadau wa uchaguzi Mkoani Simiyu,
uliofanyika julai 20, 2019 Mjini Bariadi.
Mwenyekiti
wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe Jaji wa Mahakama ya Rufaa,
Semistocles Kaijage akifungua Mkutano wa wadau wa Uchaguzi Mkoani
Simiyu, uliofanyika Julai 20, 2019 Mjini Bariadi,(kulia) Mratibu wa
Zoezi la Uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura Mkoani Simiyu,
Bw. Maganga Simon
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya
Uchaguzi, Mhe Jaji wa Mahakama ya Rufaa, Semistocles Kaijage(katikati
walioketi) akiwa katika picha ya pamoja viongozi wa dini mkoani Simiyu
mara baada ya kufungua Mkutano wa wadau wa Uchaguzi Mkoani humo,
uliofanyika Julai 20, 2019 Mjini Bariadi.
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya
Uchaguzi, Mhe Jaji wa Mahakama ya Rufaa, Semistocles Kaijage akifungua
Mkutano wa wadau wa Uchaguzi Mkoani Simiyu, uliofanyika julai 20, 2019
Mjini Bariadi.
*************
|
Na Stella Kalinga, Simiyu
Tume ya Taifa ya Uchaguzi
inatarajia kuanza rasmi zoezi la Uboreshaji wa Daftari la kudumu la
wapiga kura mkoani Simiyu kuanzia Julai 31, 2019 hadi Agosti 06, 2019.
Akifungua mkutano wa wadau wa
Uchaguzi mkoani Simiyu, Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe
Jaji wa Mahakama ya Rufaa, Semistocles Kaijage amesema Tume
imekamilisha maandalizi ya uboreshaji daftari ambayo ni pamoja na
kuhakiki vituo vya kujiandikisha, uandikishaji wa majaribio, maandalizi
ya vifaa vya uboreshaji daftari, mkakati wa elimu kwa mpiga kura na
uzinduzi wa uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura.
Amesema uboreshaji huu
hautawahusisha wapiga kura wote walioandikishwa kwenye daftari la kudumu
la wapiga kura mwaka 2015 bali utawahusu wapiga kura wapya ambao
wametimiza miaka 18, wale ambao watatimmiza.umri wa miaka 18 siku ya
uchaguzi Mkuu mwaka 2020, ambao wamehama katika maeneo ya awali ya
uchaguzi na wale ambao kadi zao zimeharibika
Katika hatua nyingine Jaji
Kaijage ametoa rai kwa wananchi wote wenye sifa kujitokeza kwa wingi ili
kuboresha taarifa zao, huku akitoa wito kwa viongozi wa vyama vya
siasa, kuzingatia sheria za uchaguzi na kanuni zake katika zoezi hili
la uboreshaji na maelekezo kwa Vyama vya Siasa kuhusu uboreshaji.
Kwa upande wake Afisa TEHAMA
Mwandamizi kutoka Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Bw. Frank Mhando amesema
Tume imefanya uhakiki wa vituo vya uandikishaji ambavyo vimeongezeka
kutoka 36,549 mwaka 2015 hadi 37,407 mwaka 2018 (Tanzania Bara), upande
wa Tanzania Zanzibar vimeongezeka kutoka 380 mwaka 2015 hadi 407 mwaka
2018; huku akifafanua kuwa katika uandishaji huu kila Kijiji au Mtaa
utakuwa na angalau Kituo kimoja cha kujiandikisha.
Naye Mratibu wa Zoezi la
Uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura Mkoani Simiyu, Bw.
Maganga Simon amesema mkoa umejiandaa vizuri ili kufanikisha zoezi
ambapo wananchi wenye sifa zaidi ya 700,000 wanatarajia kuandikishwa
katika daftari hilo huku akiwasisitiza viongozi wote mkoani hapo
kuwahamasisha wananchi wenye sifa kujitokeza kujiandikisha.
“Mkoa wetu ni mwenyeji wa
Maonesho ya Nanenane Kitaifa mwaka2019, tutatumia fursa hiyo
kuhamasisha, kutakuwa na bango kubwa litakaloonesha kuwa kuanza Julai
31 hadi Agosti 6 2019 mkoa wetu utashiriki kikamilifu kwenye zoezi la
uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura na Simiyu tumejipanga
kufanikisha zoezi hili ambalo linasimamiwa na Tume ya Taifa ya uchaguzi”
alisema
Akizungumza kwa niaba ya watu
wenye ulemavu, Katibu wa Chama cha Viziwi (CHAVITA) Mkoa wa Simiyu,
Alex Benson amewaomba viongozi wa vyama vya siasa kuwapa fursa watu
wenye ulemavu kuwania nafasi mbalimbali, huku akisisitiza wasimamizi
kupewa mafunzo ya lugha ya alama ili kurahisisha mawasiliano na watu
wenye ulemavu pindi wanapoenda kujiandikisha na kupiga kura.
Naye Dora Stephano kutoka
katika ASASI za kiraia amesema Tume ione uwezekano wa kuongeza
ushirikishwaji wa asasi za kiraia nyingi zaidi, ili kuongeza wigo wa
kutoa elimu kwa wapiga kura juu ya masuala mbalimbali ya uandikishaji na
uchaguzi.
Mkutano wa wadau wa uchaguzi
mkoani Simiyu, umewahusisha Mratibu wa Uandikishaji wa Mkoa, Viongozi
wa Vyama vya siasa Viongozi wa dini, wawakilishi wa watu wenye ulemavu,
wawakilishi wa vijana, wawakilishi wa wanawake, wawakilishi wa asasi za
kiraia, watendaji wa Tume na waandishi wa habari.
No comments:
Post a Comment