Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akisisitiza jambo leo tarehe 22 Julai 2019 wakati wa kikao kazi kilichofanyika katika Ofisi ndogo ya Wizara ya Kilimo Jijini Dar es salaam kutoa maelekezo ya mgawanyo wa majukumu. Kulia kwake ni Naibu waziri wa Kilimo Mhe Hussein Bashe (Mb) na kushoto kwake ni Mhe Omary Mgumba. (PIcha Zote Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo)
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akisisitiza jambo leo tarehe 22 Julai 2019 wakati wa kikao kazi kilichofanyika katika Ofisi ndogo ya Wizara ya Kilimo Jijini Dar es salaam kutoa maelekezo ya mgawanyo wa majukumu. Kulia kwake ni Naibu waziri wa Kilimo Mhe Hussein Bashe (Mb), Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Mhandisi Mathew Mtigumwe na Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Omary Mgumba (Mb).
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akizungumza na Naibu waziri wa Kilimo Mhe Hussein Bashe (Mb) leo tarehe 22 Julai 2019 wakati wa kikao kazi kilichofanyika katika Ofisi ndogo ya Wizara ya Kilimo Jijini Dar es salaam kutoa maelekezo ya mgawanyo wa majukumu.
Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Dar es salaam
Waziri
wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) leo tarehe 22 Julai 2019 ameongoza kikao kazi
cha uongozi wa juu wa Wizara ya Kilimo ili kutoa taswira ya muelekeo wa Wizara
hiyo.
Kikao
hicho kilichotuama kwa masaa kadhaa katika Ofisi ndogo za Wizara ya Kilimo Jijini
Dar es salaam na kuongozwa na Mhe Hasunga, kimehudhuriwa pia Naibu Maziri wa
Kilimo Mhe Omary Mgumba (Mb) na Mhe Hussein Bashe kadhalika katibu Mkuu wa
Wizara hiyo Mhandisi Mathew Mtigumwe.
Katika
kikao hicho Waziri Hasunga amewataka Naibu Mawaziri hao kuhakikisha kuwa
wanafanya kazi kwa bidii na ushirikiano ili kutimiza adhma ya serikali ya awamu
ya tano inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt John
Pombe Magufuli akiwa na muktadha wa kuimarisha uchumi wa wananchi kadhalika
maendeleo kwa ujumla wake.
Waziri
wa Kilimo Mhe Hasunga ametoa taswira ya muelekeo wa wizara hiyo katika mipango
ya muda mfupi na muda mrefu ili kuwa na weledi na utendaji uliotukuka katika
utekelezaji wa ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ya mwaka 2015/2020.
Rais
Magufuli amemteua Naibu waziri wa Kilimo Mhe Hussein Bashe akishika nafasi ya
aliyekuwa Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Innocent Bashungwa ambaye sasa ni waziri
wa Viwanda na Biashara.
Moja
ya mambo aliyoyabainisha Mhe Hasunga ni pamoja na haja
ya kuanzishwa kwa Sheria ya Kilimo itakayotoa suluhisho la changamoto
zinazamkabili Mkulima na Sekta hiyo kwa ujumla.
“Kuna kila sababu ya kuanzishwa haraka sheria ya
kilimo na tayari tupo katika hatua za mwisho, kwa sababu hatuna Sheria ya
Kilimo na inayotumika sasa ni Sera ya Kilimo, iliyotungwa mwaka 2013 ambayo pia
inahitaji kupitiwa upya” amesema
Mhe. Hasunga ameongeza kuwa Sheria zinazotumika kwa
sasa ni za Bodi za Mazao mbalimbali, ambazo pia zinachangamoto zake na kuna
mazao ambayo hayana Bodi kiasi kwamba kuwatetea Wakulima wa mazao hayo inakuwa
vigumu.
Mazao yaliyo katika utaratibu wa Bodi ni pamoja na
zao la Pamba, Kahawa, Chai, Korosho, Pareto na Tumbaku kwa upande wa mazao ya
biashara, mazao ambayo hayana bodi ni yale ya chakula ambayo nayo yana mchango
mkubwa katika uchumi wa Taifa.
Kadhalika ameeleza kuhusu usajili wa wakulima wa mazao yote na ambapo Bodi hizo ziliagizwa
kuwapatia vitambulisho kwa ajili ya kuwatambua wakulima hao na wanapofanyika
kazi zao ili iwe rahisi kuwahuduma.
Pamoja na mambo mengine Mhe Hasunga ametaja umuhimu wa Wizara
ya Kilimo kuanzisha Bima ya Mazao itakayokuwa suluhisho kwa wakulima nchini
ambao kwa muda mrefu wamekosa utetezi pindi wanapopatwa na majanga kutokana na
uchache wa mvua ama vinginevyo, jambo linalopelekea kukoseka kwa mazao ya
kutosha.
MWISHO.
No comments:
Post a Comment