MHE.AWESO ATOA MAELEKEZO MRADI WA MAJI MASANGE WILAYANI KONDOA
Naibu Waziri wa Maji Mhe Jumaa
Aweso,akizungumza na wananchi wa kijiji cha Masange wilayani Kondoa
baada ya kufanya ziara ya kukagua na kujionea mradi wa maji.
Mbunge wa Jimbo la Kondoa vijijini ambaye
pia ni Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dokta.Ashatu Kijaji,akizungumza
na wananchi wa kijiji cha Masange wilayani Kondoa wakati wa ziara ya
Naibu Waziri wa Maji Mhe.Juma Aweso alipofanya ziara ya kukagua na
kujionea mradi wa maji.
Mwenyekiti wa Maji Kijiji cha Masange
Bw.Bakari Mnyoti ,akitoa kero yake kwa Naibu Waziri wa Maji Mhe.Juma
Aweso (hayupo pichani) ambapo alifanya ziara ya kukagua na kujionea
mradi wa maji.
Mkazi wa Kijiji cha Masange Bi.Mariam
Isaka ,akizungumza mbele ya Naibu Waziri wa Maji Mhe.Juma Aweso (hayupo
pichani) ambapo alifanya ziara ya kukagua na kujionea mradi wa maji.
Sehemu ya wanakijiji wa Masange
wakimsikiliza Naibu wa Maji Mhe.Juma Aweso (hayupo pichani) akizungumza
mara baada ya kufanya ziara ya kukagua na kujionea mradi wa Maji uliopo
wilayani Kondoa.
Naibu Waziri wa Maji Mhe.Juma
Aweso,akiongozana na baadhi ya wanakijiji na viongozi kupanda mlima
kwenda kujionea Taki la Maji ambalo hutumika kusambaza maji katika
kijiji cha Masange wilayani Kondoa.
Naibu Waziri wa Maji Mhe.Juma Aweso
,akiwa amepanda juu ya Taki la Maji akikagua na kujionea hali halisi ya
maji ya usambazajwi katika kijiji cha Masange.
Mbunge wa Jimbo la Kondoa vijijini ambaye
pia ni Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dokta.Ashatu Kijaji,akiongozana
na Naibu Waziri wa Maji Mhe.Juma Aweso kupanda juu ya Taki la maji
kujionea jinsi maji yanayotumika kusambazwa kwa wanakijiji wa Masange
wilayani Kondoa.
…………………………
Na.Alex Sonna,Dodoma
Naibu Waziri wa Maji Mhe Jumaa Aweso
amesema Wizara yake itashirikiana na TAKUKURU ili kujiridhisha katika
utekelezaji mradi wa Maji katika kijiji cha Masange Wilayani Kondoa
mkoani Dodoma.
Naibu Waziri Aweso ameyasema hayo wakati
akizungumza na wananchi wa eneo hilo alipofanya ziara ya kukagua na
kujionea mradi wa Maji kijiji cha Masange uliogharimu kiasi cha
Sh.Milioni 433 baada ya kupewa majibu yasiyojitosheleza na Mkandarasi wa
Mradi huo.
“Haiwezekani tukauziwa mbuzi kwenye
gunia,lazima kukagua na kujionea,baada ya kupewa majibu ya kusuasua
hivyo TAKUKURU tutashirikiana nao kubaini ubadhilifu,na mkandarasi
asilipwe mpaka tufanye uchunguzi tujiridhishe”amesema Aweso
Hali hiyo imekuja baada ya Mkandarasi wa
mradi huo wa Maji kampuni ya Best One kwa kushirikiana na wataalam wa
sekta ya Maji wa halmashauri ya Wilaya ya Kondoa kutoa majibu
yasiyoridhisha kuhusu matumizi ya fedha zilizotumika katika mradi huo .
Akijibu kero ya wananchi hao kuhusu Maji
Mhe Aweso amepiga simu mbele ya wananchi kwa wataalamu wa Wizara
kuulizia taratibu za upatikanaji wa Gari la kuchimba visima katika
kijiji hicho ambapo ameahidi kuchimbwa visima viwili kwenye Kijiji hicho
ndani ya kipindi cha muda mfupi.
Katika kujiridhisha na mradi huo Mhe
Aweso alilazimika kupanda kwenye mlima ambao chanzo cha maji
kinapatikana ambapo alikiri kuwepo kwa changamoto Na kuahidi kuzimaliza
ili wananchi wa Masange waweze kupata maji na kwenda sawa na kauli mbiu
ya kumtua mama ndoo.
Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Kondoa
vijijini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dokta.Ashatu
Kijaji amesema yupo tayari kufanya kazi hata saa sita usiku na
walichomwagiza wananchi wake ni kutatua kero ya Maji .
Dkt.Kijaji amesema kuwa wananchi wa Mtaa
wa Masange wamesema adha kubwa inayowakabili ni maji hivyo ni vyema
serikali ikafanya mchakato haraka kutatua kero hiyo.
Awali ,akisoma taarifa ya Mradi wa Maji
wa Masange mbele ya Naibu Waziri wa Maji Jumaa Aweso,Kaimu Meneja wa
Wakala wa Maji vijijini[RUWASA]Wilaya ya Kondoa Mhandisi Falaura Seleman
Kikusa amesema mradi wa Maji Masange ulianza tangu tarehe
15,Disemba,2014 na kuzinduliwa rasmi tarehe 13,Septemba ,2016 kupitia
mbio za Mwenge wa Uhuru huku ukigharimu zaidi ya Tsh.Milioni 433 .
Aidha amebainisha kuwa muda wa
utekelezaji wa Mradi huo kwa mujibu wa Mkataba ni kipindi cha miezi mine
kuanzia tarehe 15,Disemba,2014,hadi 15,Machi,2015 hivyo kutokana na
changamoto mbalimbali hususan kuchelewa kwa malipo ya madai ya
mkandarasi,mradi uliongezewa muda wa utekelezaji na kukamilika rasmi
mnamo tarehe 7,Juni,2018.
Mhandisi Kikusa ameendelea kufafanua kuwa
upatikanaji wa Maji katika kijiji cha Masange haukidhi mahitaji halisi
ya maji kwa wakazi wa kijiji hicho kwani huduma ya maji imekuwa
ikipatikana kwa mgao kwa vitongoji kwa masaa manne hadi matano.
Amesema chanzo cha kuwepo kwa hali hiyo
unatokana na changamoto kadhaa ikiwemo kuongezeka kwa wakazi pamoja na
kukua kwa mji wa Masange ,Uwezo wa chanzo cha Maji [lita 119,577.6 kwa
siku]kuwa mdogo ikilinganisha na mahitaji halisi ya Maji ya sasa [zaidi
ya lita 141,560 kwa siku] na changamoto nyingine ni usimamizi usio mzuri
kutoka kwa timu ya mhandisi.
Hata hivyo mkandarasi wa mradi hadi
kufikia sasa alishalipwa kiasi cha sh.347,421,000 kati ya gharama
433,288,548 na zilizobaki kwa mujibu ya makubaliano ya mkataba ni
Tsh.120,609,648.
No comments:
Post a Comment