MAGARI YAGONGANA NA KUSABABISHA VIFO VYA WATU 4 ,MAJERUHI 12 KAHAMA
Watu wanne wamefariki dunia na wengine 12
wamejeruhiwa katika ajali iliyotokea jana majira ya saa mmoja usiku
katika eneo la nyambula kata ya Ngogwa Wilayani Kahama mkoani Shinyanga
baada ya gari aina ya Totoya hice yenye namba za usajili T 710 AZZ na
Gari aina ya Land cruiser yenye namba za usajili T 477 ATC.
Mpekuzi Blog imezungumza na kamanda wa
polisi mkoa wa Shinyanga (ACP) Richard Abwao ambaye alikuwa katika
hospitali ya Halmashauri ya Mji wa Kahama kuhusiana na tukio hilo na
kusema kuwa chanzo cha ajali hiyo ni mwendo kasi wa dereva wa hice
iliyokuwa na abiria ikitokea kakola kwenda kahama.
Amesema barabara ya kakola kahama imekuwa
na vumbi nyingi kutokana na kutumika na magari mengi baada ya kuibuka
kwa machimbo mapya ya kakola namba 9 na kuwataka madereva wote kuchukua
tahadhari kwa kutoendesha kwa mwendo kasi ili kuzuia ajali.
Amefafanua kuwa leo RTO atakuwa na
operation maalum katika barabara hiyo ili kubaini madereva wanaokiuka
sheria za usalama barabarani pamoja na kuyaondoa magari mabovu yote
barabarani.
Kamanda Abwao Amesema leo atatoa taarifa
rasmi za ajili hiyo ikiwemo majina ya watu waliopoteza maisha katika
ajali hiyo iliyotokea usiku wa kuamkia leo.
Boniface Makoye shuhuda wa tukio hilo
amesema baada ya ajali hiyo kutokea abiria wengi walijeruhiwa na aliweza
kuwaokoa baadhi yao ambao walikuwa wamenaswa na vyuma katika hice hiyo.
Taarifa kamili zaidi kuhusiana na ajali hii endelea kufuatilia
Wazo-huru blog
No comments:
Post a Comment