![](https://fullshangweblog.co.tz/wp-content/uploads/2019/06/PMO_6475-720x1024.jpg)
Mshambuliaji wa Azam, Obey Chirwa
akimtoka Mlinzi wa Lipuli N. Lufunga katika mechi ya fainali ya ubingwa
wa mashindano ya Shirikisho la Azam iliyochezwa kwenye uwanja wa Ilulu
mjini Lindi Juni 1, 2019. Azam ilishinda 1-0. (Picha na ofisi ya Waziri
Mkuu)
![](https://fullshangweblog.co.tz/wp-content/uploads/2019/06/PMO_6444-1024x756.jpg)
Mshambuliaji wa Azam, Donald Ngoma
akichanja mbuga kuelekea lango la Lipuli huku akizongwa na mlinzi wa
Lipuli Haruna Shamte katika mechi ya fainali ya mashindano ya Shirkisho
la Azam kwenye uwaja wa Ilulu mjini Lindi Juni 1, 2019. Azam ilioshinda
1-0. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkiuu)
![](https://fullshangweblog.co.tz/wp-content/uploads/2019/06/61525306_1362254307274140_4665949889375502336_n.png)
****************************************
Klabu ya Lipuli fc imepokea
kichapo cha goli 1:0 kutoka kwa wanalambalamba Azam fc ambapo mchezo huo
ulikuwa fainali na Azam kutangazwa kuwa Mabingwa wa Michuano ya Kombe
la Shirikisho.
Baada ya kwenda mapumziko kwa timu
zote mbili Azam walikuja katika kipindi cha pili kuonesha kweli
wanahitaji kombe hilo hivyo mpaka kufikia dakika ya 65 Obray Chirwa
kufanikiwa kuingia kambani na kufanikisha timu yake kuchukua taji hilo
Katika matokeo hayo timu ya Lipuli FC ambayo ni mshindi wa pili imeibuka na kitita cha sh million 25.
No comments:
Post a Comment