OFISI YA MAKAMU WA RAIS MAZINGIRA YAAHIDI KUTAFUTIA UFUMBUZI UPATIKANAJI MIFUKO MBADALA
![](https://fullshangweblog.co.tz/wp-content/uploads/2019/06/1-4.jpg)
Afisa Mazingira Halmashauri jiji la
Dodoma Bw.Ally Mfinanga, akizungumza na wananchi pamoja na
wafanyabiashara wa soko la Majengo liliko jijini Dodoma Leo baada ya
kutembelea na kujionea hali halisi ya utekelezaji pamoja na kuzindua
kikosi kazi maalumu cha katazo la Mifuko ya Plastiki ambapo June Mosi
ndo mwisho wa matumizi yake.
![](https://fullshangweblog.co.tz/wp-content/uploads/2019/06/2-2.jpg)
Katibu Tawala wilaya ya Dodoma Bw.Edward
Mpongolo akiongea na wafanyabiashara wa soko la Majengo liliko jijini
Dodoma baada ya kutembelea na kujionea hali halisi ya utekelezaji
pamoja na kuzindua kikosi kazi maalumu cha katazo la Mifuko ya Plastiki
ambapo leo June Mosi ndo mwisho wa matumizi yake.
![](https://fullshangweblog.co.tz/wp-content/uploads/2019/06/3-2.jpg)
Meneja wa Kanda ya Kati kutoka Baraza la
Taifa la Mazingira (NEMC) Bw.Carlos Mbuta,akizungumza na wafanyabiashara
wa soko la Majengo liliko jijini Dodoma baada ya kutembelea na
kujionea hali halisi ya utekelezaji pamoja na kuzindua kikosi kazi
maalumu cha katazo la Mifuko ya Plastiki ambapo leo June Mosi ndo mwisho
wa matumizi yake.
![](https://fullshangweblog.co.tz/wp-content/uploads/2019/06/4-2.jpg)
Katibu Tawala wa Nkoa wa Dodoma Bw.Maduka
Kessy,akizungumza na wafanyabiashara wa soko la Majengo liliko jijini
Dodoma baada ya kutembelea na kujionea hali halisi ya utekelezaji
pamoja na kuzindua kikosi kazi maalumu cha katazo la Mifuko ya Plastiki
ambapo leo June Mosi ndo mwisho wa matumizi yake.
![](https://fullshangweblog.co.tz/wp-content/uploads/2019/06/5-1.jpg)
Katibu Mkuu ofisi ya Makamu wa Rais
Muungano na Mazingira Mhandisi Joseph Malongo,akizungumza na
wafanyabiashara wa soko la Majengo liliko jijini Dodoma baada ya
kutembelea na kujionea hali halisi ya utekelezaji pamoja na kuzindua
kikosi kazi maalumu cha katazo la Mifuko ya Plastiki ambapo leo June
Mosi ndo mwisho wa matumizi yake.
![](https://fullshangweblog.co.tz/wp-content/uploads/2019/06/6-2.jpg)
Mkurugenzi wa Idara ya Mazingira Ofisi ya
Makamu wa Rais Prof.William Mwegoha,akizungumza na wafanyabiashara wa
soko la Majengo liliko jijini Dodoma baada ya kutembelea na kujionea
hali halisi ya utekelezaji pamoja na kuzindua kikosi kazi maalumu cha
katazo la Mifuko ya Plastiki ambapo leo June Mosi ndo mwisho wa matumizi
yake.
![](https://fullshangweblog.co.tz/wp-content/uploads/2019/06/7-2.jpg)
![](https://fullshangweblog.co.tz/wp-content/uploads/2019/06/8-2.jpg)
Mkuu wa wilaya ya Dodoma Mhe.Patrobas
Katambi,akizungumza na wafanyabiashara wa soko la Majengo baada ya
kufanya oporesheni ya kukagua huku akizindua kikosi kazi maalumu cha
katazo la Mifuko ya Plastiki ambapo leo June Mosi ndo mwisho wa matumizi
yake.
![](https://fullshangweblog.co.tz/wp-content/uploads/2019/06/9-2.jpg)
Mkuu wa wilaya ya Dodoma Mhe.Patrobas
Katambi,akiongea na mfanyabiashara wa mifuko mipya baada ya kufanya
oporesheni ya kukagua huku akizindua kikosi kazi maalumu cha katazo la
Mifuko ya Plastiki ambapo leo June Mosi ndo mwisho wa matumizi yake.
![](https://fullshangweblog.co.tz/wp-content/uploads/2019/06/10-2.jpg)
Katibu Mkuu ofisi ya Makamu wa Rais
Muungano na Mazingira Mhandisi Joseph Malongo,akiangalia mifuko mipya
ambayo imeanza kutumika nchi nzima mara baada ya kufanya oparesheni
pamoja na uzinduzi kikosi kazi maalumu cha katazo la Mifuko ya Plastiki
ambapo leo June Mosi ndo mwisho wa matumizi yake.
![](https://fullshangweblog.co.tz/wp-content/uploads/2019/06/11A.jpg)
Sehemu ya mifuko mipya ambayo imeanza kutumika leo kwa nchi nzima katika soko la Majengo na Sabasaba.
![](https://fullshangweblog.co.tz/wp-content/uploads/2019/06/12-2.jpg)
Katibu Mkuu ofisi ya Makamu wa Rais
Muungano na Mazingira Mhandisi Joseph Malongo akiwa na Mkuu wa Wilaya ya
Dodoma Mhe.Patrobas Katambi,wakifanya oparesheni katika masoko ya
majengo na sabasaba huku wakizindiua kikosi kazi maalumu cha katazo la
Mifuko ya Plastiki ambapo leo June Mosi ndo mwisho wa matumizi yake.
![](https://fullshangweblog.co.tz/wp-content/uploads/2019/06/13-2.jpg)
Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mhe.Patrobas
Katambi akimuonesha jambo Katibu Mkuu ofisi ya Makamu wa Rais Muungano
na Mazingira Mhandisi Joseph Malongo,mara baada ya kufanya ziara ya
Oparesheni na kuzindua kikosi kazi maalumu cha katazo la Mifuko ya
Plastiki ambapo leo June Mosi ndo mwisho wa matumizi yake.
![](https://fullshangweblog.co.tz/wp-content/uploads/2019/06/15-1.jpg)
Sehemu ya wafanya biashara wa soko la Sabasaba wakifanya biashara zao za kuuza nyanya na baadhi ya bidhaa.
![](https://fullshangweblog.co.tz/wp-content/uploads/2019/06/16-1.jpg)
Katibu Mkuu ofisi ya Makamu wa Rais
Muungano na Mazingira Mhandisi Joseph Malongo,akinunua kikapu katika
soko la Sabasaba mara baada ya kufanya ziara ya Oparesheni na kuzindua
kikosi kazi maalumu cha katazo la Mifuko ya Plastiki ambapo leo June
Mosi ndo mwisho wa matumizi yake.
![](https://fullshangweblog.co.tz/wp-content/uploads/2019/06/17A.jpg)
Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mhe.Patrobas
Katambi akinunua kikapu katika soko la Sabasba akiwa na Katibu Mkuu
ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhandisi Joseph
Malongo,mara baada ya kufanya ziara ya Oparesheni na kuzindua kikosi
kazi maalumu cha katazo la Mifuko ya Plastiki ambapo leo June Mosi ndo
mwisho wa matumizi yake.
Picha na Alex Mathias-Wazohuru blog
………………….
Na ALEX MATHIAS, DODOMA.
Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais
Mhandisi Joseph Malongo, amewahakikishia wananchi kuwa ofisi yake
inashughulia kwa ukaribu swala la bei ya mifuko mbadala ili kila mwana
nchi aweze kuimudu.
Ameyasema hayo leo Jijini Dodoma, wakati
uzinduzi wa kikosi kazi maalumu cha kupambana na uharibifu wa
mazingira kitaifa, amesema ofisi yake inafanya jitihada za kuhakikisha
kila mwananchi anamudu garama za mifuko hiyo.
Amesema kumekuwa na malalamiko kuwa na
uhaba wa mifuko mbadala na wengine wamekuwa wakilalamika kuwa bei ya
mifuko hiyo sio rafiki, amebainisha kuwa wamekuwa wakihamasisha
kuzalishwa kwa wingi mifuko hiyo.
“Kumekuwa na malalamiko kidogo kuhusu
upatikanaji wa mifuko hii, na wengine wamelalamika kutokumudu garama
sisi kama ofisi ya makamu wa raisi mazingira tunalitafutia ufumbuzi
suala hili ili mifuko ipatikane kwa wingi na kwa garama nafuu” amesema
Malongo.
Amewataka wananchi kutokupuuzia sheria
hiyo kwani sheria hiyo imetungwa kwa mujibu wa sheria za nchi, hivyo
atakayepuuzia atachukuliwa sheria kali ambapo amesema kwa watengenezaji
faini milioni ishirini hadi bilioni moja.
Na kwa muuzaji ni faini ya shilingi laki
moja ana isiyozidi laki tano au kifungo jela kisichozidi miazi 3 au
vyote kwa pamoja, na kwa mtumiaji ni faini ya shilingi elfu
therathini(30,000) au kifungo siku saba jela au vyote kwa pamoja.
Amesema kuanzia sasa ni marufuku mahala
popote kutupa uchafu wa aina yoyote ikiwa ni pamoja na kutumia mifuko
ya plastiki, amebainisha kuwa kwa yeyote atakayekutwa na kikosi kazi
anatupa uchafu mahala masipotakiwa faini ni shilingi elfu hamsini.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya
Dodoma, Patrobus Katambi, amesema kuwa tangu katazo hilo lilipotangazwa
na serikali wamekuwa wakizungukia maeneo mbalimbali wakitoa elimu na
wananchi wamekuwa na mapokeo mazuri ya kampeni hiyo.
Amesema operation hiyo itakua endelevu na
ametangaza kuwa ni marufuku kwa abiria yeyote kupanda kwenye daladala
au pikipiki akiwa na mfuko wa plastiki, na amewataka makonda na madereva
kuwa makini na abiria wanaopanda kwenye vyombo vyao.
Amesema kuanzia sasa kila mtu katika
nyumba yake ahakikishe anafanya usafi ndani ya mita 5 – 10, na
kusipatikane mfuko wa plastiki katika maeneo yao na yeyote
atakayekutwa hajafanya usafi atachukuliwa hatua za kisheria.
Aidha amewaonya wenye maduka ambao
wamekuwa na tabia ya kutofanya usafi katika maeneo yao watachukuliwa
hatua za kisheria, na atakaye kutwa na taka katika nyumba atachukuliwa
hatua za kisheria.
“Kwa suala hili tumefanya vizuri
tulipopokea tu taarifa ya katazo tulizunguka sehemu nyingi kutoa elimu
ya masuala ya kutumia mifuko mbadala na mapokea yalikuw ni makubwa
sana, lakini wiito wangu ni kuhakikisha kila mtu kwenye nyumba yake
ahakikishe ndani ya mita 5- 10 anafanyya usafi na kuondoa mifuko hiyo”,
amesema katambi.
No comments:
Post a Comment