Mkuu wa
wilaya ya Iringa Richard Kasesela akiwa ameambatana na diwani wa kata ya Mwangata ndugu Nguvu Chengula pamoja na naibu meya wa manispaa ya Iringa Joseph Ryata wakiingia kufunga mafunzo ya ujasiliamali yaliyodhaminiwa na diwani wa kata hiyo
Mkuu wa
wilaya ya Iringa Richard Kasesela akiwapa vyeti wajasiliamali walioshiriki mafunzo yaliyodhamini na diwani wa kata ya Mwangata Nguvu Chengula
Baadhi ya wajasiliamali walioshiriki kwenye mafunzo ya kukuza ulewa wa utengenezaji wa bidhaa mpya,mafunzo yaliyodhamini na diwani wa kata ya Mwangata Nguvu Chengula
NA FREDY
MGUNDA,IRINGA.
Mkuu wa
wilaya ya Iringa Richard Kasesela amefunga mafunzo kwa vikundi vya
wajasiriamali vya wanawake,wazee na vijana manispaa ya Iringa yaliyolenga
kuwajengea uwezo wa namna ya kutumia vizuri fedha za mikopo walizopewa na
manispaa hiyo.
Mafunzo hayo ya siku mbili yamefanyika katika ukumbi wa Damu ya Yesu uliopo katika katika kata ya Mwangata na kuhudhuriwa na wanawake,wazee na vijana zaidi ya 351 wajasiriamali kutoka katika maeneo mbalimbali ya manispaa ya Iringa na nje ya mkoa wa Iringa
Akizungumza wakati wa kufunga mafunzo hayo Kasesela aliwataka vijana,wazee na wanawake hao kutumia fedha walizopewa kwa malengo waliyokusudia na kuhakikisha wanaanzisha viwanda vidogo vidogo vitakavyoinua uchumi wao.
Aidha Kasesela
aliwataka vijana,wazee na wanawake kujitokeza kwa wingi kuomba mikopo kwenye
halmashauri za wilaya ,mikopo ambayo haina masharti magumu wala ukilinganisha
na taasisi za kifedha (benki).“Msikubali kukata tamaa kwamba maisha ni
magumu,hata siku moja serikali haiwezi kugawa pesa kwa mtu mmoja
mmoja,anzisheni vikundi vya ujasiriamali,kisha ombeni mikopo kwenye
halmashauri,pesa zipo.
Kwa
upande wake diwani wa kata ya Mwangata Nguvu Chengula alisema kuwa lengo la
kutoa mafunzo hayo ni kuwaongezea njia za kupata ajira mbadala ambayo itawakuwa
suluhisho ya kupata ajira
“Leo
tumetoa mafunzo kwa wajasiliamalia zaidi ya 351 wa kutoka katika maeneo
mbalimbali ya mkoa wa Iringa na nje ya mkoa wa Iringa hivyo utaona namna
ambavyo mafunzo haya yamewaingia wajasiliamali hao” alisema Chengula
Chengula
alisema kuwa wajasiliamali wengi hawana elimu ya kutosha kuhusu ujasiliamali
ndio maana aliamua kufadhili mafunzo hayo ya siku mbili ili wapate elimu hiyo.
Lakini
pia Chengula aliwataka wananchi wa kata ya Mwangata kuyatumia vizuri mafunzo ya
ujasiliamali ambayo yamekuwa yanadhamini na diwawa wa kata hiyo kwa kuwa ndio
njia ya kujikomboa kimaisha
Nao washiriki
wa mafunzo hayo walisema kuwa baada ya kupata mafunzo hayo
wamesema kuwa mafunzo hayo yamekuwa yakiongezea ujuzi wa kufanya biashara na
kukuza mitaji yao.
walisema
kupitia mafunzo hayo ya siku mbili wamepata elimu kuhusu namna ya kuanzisha
biashara na kutafuta masoko,kutengeneza mnyororo wa thamani kutunza kumbukumbu
na vifungashio na umuhimu wa uwekaji lebo” walisema wajasiliamali hao
Aidha
wajasiliamali hao wamewaomba viongozi kuiga mfano wa diwani wa kata ya Mwangata
Nguvu Chengula kwa kutoa mafunzo kwa wananchi wao waliowapa dhamana.
Wajasiliamali
walisema pia wamejifunza taratibu za utoaji wa mikopo na urejeshaji wa
mikopo,wajibu wa kiongozi wa kikundi,ukweli kuhusu Ukimwi,ukatili dhidi ya
wanawake na watoto pamoja na elimu kuhusu mfuko wa bima ya afya (CHF
iliyoboreshwa.
No comments:
Post a Comment