**********************************
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa
amewakaribisha wawekezaji kutoka nchini Rwanda waje wawekeze katika
sekta mbalimbali na kwamba Serikali itawapa ushirikiano wa kutosha.
Ameyasema hayo leo (Jumanne, Juni
11, 2019) alipokutana na kufanya mazungumzo na Spika wa Bunge la Rwanda,
Donatille Mukabalisa, Ofisini kwake Bungeni jijini Dodoma.
Amesema Serikali ipo tayari
kuwapokea wawekezaji kutoka katika nchi hiyo ili waje kuwekeza katika
sekta mbalimbali zikiwemo za viwanda, kilimo, madini na utalii.
Kadhalika, Waziri Mkuu amesema
Tanzania na Rwanda ni nchi zenye uhusiano mzuri, hivyo amemwakikishia
Spika Donatille kwamba Serikali itauimarisha uhusiano huo.
Hata hivyo, Waziri Mkuu amesema
Serikali inatekeleza mradi wa ujenzi wa reli ya kisasa (SGR) ambao
utarajiwa kusaidia katika usafirishaji wa mizigo kwenda hadi nchini
Rwanda.
Naye, Spika Donatille ameishukuru
Serikali ya Tanzania kwa ushirikiano mkubwa inaoutoa kwa Serikali ya
Rwanda, hivyo amemuhakikishia Waziri Mkuu kwamba watauendeleza.
Spika huyo amesema ushirikiano wa
Tanzania na Rwanda ni muhimu katika uchumi kwa kuwa wanatumia bandari ya
Dar es Salaam katika kusafirisha asilimia kubwa ya mizigo yao.
Amesema wananchi nao wanatakiwa
wawe na ushirikiano katika nyanja mbalimbali kama za kibiashara.
Ametumia fursa hiyo kuwakaribisha Watanzania wakawekeze nchini Rwanda
No comments:
Post a Comment