Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na
Umeme (TEMESA) Mhandisi Japhet Y. Maselle kushoto, Mhandisi Jairos
Nkoroka (wa tatu kulia) pamoja na wafanyakazi wakikagua propella za
vivuko vilivyohifadhiwa katika karakana ya mji wa Ifakara baada ya
daraja la mto Kilombero kukamililika. Vivuko hivyo, MV.Kilombero I na II
vitaanza kukarabatiwa na kuunganishwa hivi karibuni tayari kwa hatua ya
kupelekwa katika eneo la Kikove Malinyi kwa ajili ya kutoa huduma.
Mhandisi Jairos Nkoroka kushoto
akimuonyesha Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA)
Mhandisi Japhet Y. Maselle mashine ya kugandamiza vipuri vya magari
(press machine) wakati alipotembelea kukagua utendaji kazi wa karakana
hiyo mpya ya TEMESA iliyoanza kutoa huduma mwezi Juni mwaka huu katika
Halmashauri ya mji wa Ifakara wilayani Kilombero mkoani Morogoro.
Karakana hiyo sasa itahudumia wilaya zote za karibu ikiwemo wilaya ya
Ulanga na Malinyi ambazo awali zilikuwa zikitegemea kupata huduma
Morogoro mjini.
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na
Umeme (TEMESA) Mhandisi Japhet Y. Maselle kulia akikagua mashine ya
kupimia uwiano wa matairi ya magari (wheel balance) iliyopo katika
karakana ya TEMESA katika Halmashauri ya mji wa Ifakara wakati
alipoitembelea kujionea utendaji kazi wake mara baada ya kuanza kutoa
huduma Juni mosi mwaka huu. Karakana hiyo sasa itahudumia wilaya zote za
karibu ikiwemo wilaya ya Ulanga na Malinyi ambazo awali zilikuwa
zikitegemea kupata huduma za matengenezo ya magari na mitambo kutoka
Morogoro mjini.
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na
Umeme (TEMESA) Mhandisi Japhet Y. Maselle (wa pili kushoto) akifurahia
jambo na wafanyakazi mara baada ya kumaliza kukagua mipaka ya karakana
ya TEMESA Ifakara iliyoanza kutoa huduma Juni mosi mwaka huu katika
Halmashauri ya mji wa Ifakara wilayani Kilombero mkoani Morogoro.
Karakana hiyo sasa itahudumia wilaya zote za karibu ikiwemo wilaya ya
Ulanga na Malinyi ambazo awali zilikuwa zikitegemea kupata huduma za
matengenezo ya magari na mitambo kutoka Morogoro mjini.
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na
Umeme (TEMESA) Mhandisi Japhet Y. Maselle kulia akikagua kivuko cha MV.
Kilombero I kilichohifadhiwa katika karakana ya mji wa Ifakara baada ya
daraja la mto Kilombero kukamililika. Kivuko hicho pamoja na kivuko cha
MV. Kilombero II vitaanza kukarabatiwa na kuunganishwa hivi karibuni
tayari kwa hatua ya kupelekwa katika eneo la Kikove Malinyi kwa ajili ya
kutoa huduma.
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na
Umeme (TEMESA) Mhandisi Japhet Y. Maselle kushoto akikagua kivuko cha
MV Kilombero II ambacho kimehifadhiwa katika karakana hiyo baada ya
huduma za kivuko kufungwa katika mto Kilombero kutokana na kukamilika
kwa daraja. Kivuko hicho pamoja na kivuko cha MV. Kilombero I
vinatarajiwa kuanza kufanyiwa ukarabati tayari kwa hatua ya kupelekwa
katika eneo la Kikove Malinyi kwa ajili ya kutoa huduma katika maeneo
hayo.
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na
Umeme (TEMESA) Mhandisi Japhet Y. Maselle katikati akiwa katika picha ya
pamoja na wafanyakazi wa karakana mpya ya TEMESA iliyopo katika
Halmashauri ya mji wa Ifakara wilayani Kilombero mara baada ya kumaliza
kukagua karakana hiyo.
No comments:
Post a Comment