Naibu
Waziri wa Kilimo Mhe. Omary Mgumba akipata amelezo ya ujenzi wa vihenge vya
kisasa kwa upande wa ndani kutoka kwa Mhandisi wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya
Chakula (NFRA) Makao Makuu Bwana Iman
Nzobonaliba kulia kwake na wengine ni Mkurugenzi wa Uhifadhi Bwana Mikalu
Mapunda na kushoto kwake ni Mhandisi Mgole Chambili Msimamizi kutoka Kampuni ya
Feruum.
Naibu
Waziri wa Kilimo Mhe. Omary Mgumba akipata amelezo ya ujenzi wa vihenge vya
kisasa kutoka Mhandisi wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) Makao
Makuu Bwana Iman Nzobonaliba kulia kwake na wengine ni Mtendaji Mkuu wa NFRA
Bwana Milton Lupa.
Mafunsi
wa Kampuni ya Feruum wakiendelea na kazi ya kuunganisha vyuma vya ujenzi wa
vihenge vya kisasa eneo la Kizota Jijini Dodoma wakati wa ziara ya Naibu Waziri
wa Kilimo Mhe. Omary Mgumba.
Naibu
Waziri wa Kilimo Mhe. Omary Mgumba amesema Serikali ya Tanzania imepokea maombi
mapya ya kuuza mahindi kwenda nchini Kenya yenye jumla ya Tani milioni 1.
Mhe.
Mgumba ameyasema hayo wakati alipofanya ziara ya gafla kwenye Ofisi za Wakala
wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA - Makao Makuu) Jijini, Dodoma
alipotembelea leo alasiri ili kujionea maendeleo ya ujenzi wa vihenge vya
kisasa vya kuhifadhia chakula katika eneo la Kizota, Jijini Dodoma.
Naibu
Waziri Mgumba amesema wakati Serikali ikiwa kwenye hatua ya kuiuzia Zimbabwe
kiasi cha mahindi Tani laki saba (700,000) na tani laki moja (100,000) kwa mazao
mengine ya nafaka, Serikali ya Kenya imewasilisha ombi rasmi la kununua kiasi
hicho kutoka Tanzania.
Naibu
Waziri Mgumba amesema huu ni wakati muhafaka kwa Wakulima wa Tanzania
kuchangamkia fursa ya kuuza chakula cha ziada nje ya nchi na kwa bei nzuri
ambayo italeta tija na maendeleo na uchumi wao.
Aidha
Mhe. Mgumba alidokeza kuwa amefanya ziara hiyo lengo lake likiwa ni kujionea
maendeleo ya ujenzi wa vihenge vya kisasa (Silos) vya kuhifadhia mazao kwa
lengo la kuongeza akiba ya taifa ya chakula kwa Kanda ya Kati yenye kuhudumia
mikoa ya Dodoma, Singida kutoka uwezo wake wa sasa wa kuhifadhi, tani elfu
thelasini na tisa (39,000) hadi kufikia tani elfu hamsini na tisa (59,000).
Mradi
wa ujenzi wa vihenge hivyo vya kisasa, ulizinduliwa rasmi tarehe 24 Aprili,
2018 na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa
Majaliwa na ulianza rasmi Mwezi Juni 2018 huku Kampuni ya Feruum kutoka nchini
Poland ndiyo iliyoshinda zabuni ya ujenzi huo.
Akijibu
swali la Mhe. Mgumba, Mhandisi wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) Bwana
Iman Nzobonaliba amesema Mradi unataraji kuisha kwa wakati mnamo Mwezi Disemba
2019.
Akijibu
swali la Naibu Waziri Mgumba ambaye alitaka kufaham namna Wakala ilivyojianda
kununua mazao ya Wakulima katika msimu wa kilimo wa 2019/2020 Mtendaji Mkuu wa
Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula Bwana Milton Lupa amemwambia Naibu Waziri
Mgumba kuwa NFRA imeanza zoezi la kununua chakula cha ziada kutoka kwa Wakulima
tangu tarehe 17 Juni 2019 katika Kanda ya Makambako na Sumbawanga na kwamba
kiasi cha shilingi bilioni 2.5 kitatumika kwa sasa.
Bwana
Lupa amesema NFRA imejipanga kutumia bajeti ya kiasi cha bilioni 15 pamoja na
kuomba mkopo kutoka Benki ya Kilimo wenye riba nafuu na kuongeza kuwa zaidi ya
shilingi bilioni 62.6 zitatumika kwa ununuzi wa nafaka kwa msimu wa kilimo wa
2019/2020.
Akizungumzia
bei ya kununulia mahindi kwa kilo, Mtendaji Mkuu amesema bei ya ununuzi itakuwa
ikitofautiana kutoka eneo moja na eneo linguine.
“Niseme
tu kuwa tutaanza na bei ya shilingi 400 hadi 500 kwa kila kilo moja ya mahindi
lakini bei hii pia itakuwa ikibadilika kutokana na sababu mbalimbali”
Amekaririwa Bwana Milton Lupa.
Naibu
Waziri Mgumba ameongeza kuwa NFRA ni Taasisi ya Serikali na imeaminiwa
kusimamia jukumu la uhifadhi wa chakula na kuwa Taifa linatarajia makubwa
katika kuhakikisha Taifa linakuwa na akiba ya chakula ya kutosha.
“Sisi
kama Viongozi wenu, hatuna shaka na uzoefu wenu na umahiri wenu katika nyanja
ya uhifadhi wa chakula hususan nafaka kama mahindi, endeleeni mbele na sisi
tutahakikisha mnapata mahitaji yenu, nawahakiki kuwa fedha za ununuzi mtazipata
kwa kuwa Wizara ya Fedha na Mipango imetuahidi kuwa zitakuja mapema kama
mlivyopanga” Amekaririwa Mhe. Mgumba
MWISHO.
No comments:
Post a Comment