Sunday, June 16, 2019

MAJALIWA AKABIDHI VIKOMBE BONANZA LA CRDB NA WABUNGE

Mshambuliaji wa timu ya Soka ya Benki ya CRDB ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo, Abdulmajid Nsekela akimtoka mlinzi wa timu ya Soka ya Bunge, Rajab Kapira katika mechi ya kirafiki iliyochezwa kwenye uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma June 16, 2019. CRDB ilishinda 3-1. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Mke wa Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne, Mama Salma Kikwete akijiandaa kurusha mpira katika mechi ya kirafiki kati ya timu ya Mpira wa Pete ya Bunge na timu ya Benki ya CRDB kwenye uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma, Juni 16, 2019. Bunge ilishinda 35-2. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu Mkuu,Kassim Majaliwa akimkabidhi nahodha wa Timu ya Soka ya Benki ya CRDB ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo, Abdulmajid Nsekela, kikombe cha ushindi wa mechi ya soka ya kirafiki kati ya timu hiyo na timu ya Bunge iliyochezwa kwenye uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma, Juni 16, 2019. CRDB ilishinda 3-1. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Wachezaji na mashabiki wa timu ya soka ya benki ya CRDB wakishangilia baada ya kukabidhiwa kikombe cha ushindi baada ya kuitandika timu ya Bunge 3-1 katika mechi ya kirafiki ilichezwa kwenye uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma, Juni 16, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na mchezaji nyota wa timu ya mpira wa pete ya Bunge, Mke wa Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne, Mama Salma Kikwete kabla ya kuanza kwa mechi ya kirafiki kati ya Bunge na CRDB iliyochezwa kwenye uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma Juni 16, 2019. Bunge ilishinda 35-2. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

No comments:

Post a Comment