KATIBU MKUU CHAMA CHA FLERIMO CHA MSUMBIJI AWASILI JIJINI DODOMA
Na.Alex Mathias,Dodoma
KATIBU
Mkuu wa Chama Cha Flerimo cha nchini Msumbiji Samwel Regue amewasili
jijini Dodoma na kulakiwa na mgeni wake Katibu Mkuu wa Chama Cha
Mapinduzi(CCM)dokta Bashiru Ally.
Akiwa
jijini humo pamoja na mambo mengine atafanya mazungumzo na Makamu
Mwenyekiti wa CCM Bara mzee Philip Mangula kabla ya kuelekea wilayani
Kibaha mkoani Pwani kuangalia maendeleo ya ujenzi wa Chuo Cha Uongozi.
Regue
mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Dodoma pamoja na
wenyeji wake walielekea ofisi za CCM Makao Makuu alipoandaliwa mapokezi
na hapo alivishwa mavazi rasmi ya kabila ya wagogo ikiwa ni namna ya
kukaribishwa.
Akizungumza
katika mapokezi hayo dokta Bashiru amemshukuru Regue kwa ujio wake na
kusema kuwa pamoja na kwenda Kibaha ataenda Zanzibar kwa ajili ya
kuonana na raia wa Msumbiji wanaoishi huko.
“Mgeni
wetu amewasili hapa,tumempokea na kwa mujibu wa ratiba atapata nafasi
kutembelea ujenzi wa Chuo chetu pale Kibaha ambao unaendelea vizuri,
“CCM,Frelimo,ANC
cha Afrika ya Kusini,NPLA cha Angola,SWAPO cha Namibia,ZANU PF cha
Zimbabwe ni vyama ambavyo vimeungana kujenga chuo hicho kwa kushirikiana
na chama cha Kikomunist cha nchini China”alisema dokta Bashiru.
No comments:
Post a Comment