Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi
akimkabidhi jarida la Nchi Yetu Tanzania, Nahodha wa Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars)
anayekipiga katika Klabu ya KRC Genk ya Nchini Ublegiji Mbwana Samatta amara baada ya
mazungumzo baina yao katika Ofisi za Idara ya Habari (MAELEZO) jana Jumanne (Mei 28, 2019)
Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) na Msemaji Mkuu wa Serikali, (wa tatu kulia) Dkt.
Hassan Abbasi akiwa katika picha ya pamoja na Nahodha wa Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa
Stars) na Mshambuaji wa Klabu ya KRC Genk ya Ubelgiji (katikati) mara baada ya kumalizika kwa
mazungumzo baina yao katika Ofisi za Idara ya Habari (MAELEZO jana Jumanne (Mei 28, 2019)
Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) na Msemaji Mkuu wa Serikali, (wa tatu kulia) Dkt.
Hassan Abbasi akizungumza na Nahodha wa Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) na
Mshambuliaji wa Timu ya KRC Genk ya Ubelgiji Mbwana Samatta wakati wa mazungumzo baina
yao katika Ofisi za Idara ya Habari (MAELEZO) jana Jumanne (Mei 28, 2019) Jijini Dar es Salaam.
Nahodha wa Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) na Mshambuaji wa Kalbu ya KRC Genk ya
Ubelgiji akifafanua jambo ka Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) na Msemaji Mkuu wa
Serikali, (wa tatu kulia) Dkt. Hassan Abbasi wakati wa mazungumzo baina yao katika Ofisi za
Idara ya Habari (MAELEZO) jana Jumanne (Mei 28, 2019) Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Utalii ya Samatta Tours, Hamisi Waziri akifafanua jambo kwa
Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Dkt. Hassan Abbasi wakati wa mazungumzo baina
yao katika Ofisi za Idara ya Habari (MAELEZO) jana Jumanne (Mei 28, 2019) Jijini Dar es Salaam.
Katikati ni Nahodha wa Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) Mbwana Samatta.
SERIKALI
imesema itaendelea kumsaidia kwa hali na mali Nahodha wa Timu ya Taifa
ya Tanzania, Taifa Stars, anayechezea Klabu ya Genk ya Nchini Ubelgiji
Mbwana Samatta ili kuhakikisha kuwa anafungua milango ya uwekezaji na
kuiweka juu ramani ya Soka la Tanzania katika anga la kimataifa.
Akizungumza
jana Jumanne (Mei 28, 2019) Ofisini kwake Jijini Dar es Salaam na
Nahodha huyo waTaifa Stars, Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) na
Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbasi alisema Samatta ameonyesha
njia iliyoshindwa kufikiwa na wachezaji wengi wa miaka ya nyuma
waliojaribu kucheza Soka la kulipwa katika vilabu mbalimbali vya Nchi za
Nje hususani Bara la Ulaya.
Dkt.
Abbasi alisema Serikali ilimteua Sammatta kuwa Balozi wake wa Utalii
kutokana na sifa kubwa zilizoletwa na mchezaji huyo nje ya mipaka ya
Tanzania kwa kuwa Serikali ina Imani naye kubwa katika kufungua milango
ya fursa za uwekezaji hususani katika miradi ya maendeleo inayotekelezwa
na Serikali ya Awamu ya Tano hapa nchini.
“Mbwana
Samatta ameonyesha njia ambayo ilikuwa ndoto iliyoshindwa kutimizwa na
wachezaji wengi wa zamani, hatua hii aliyofikia ni kubwa na imetokana na
sifa kubwa ya nidhamu na kipaji cha mchezo huu hili ni funzo kwa
wachezaji wetu chipukizi” alisema Dkt. Abbasi.
Kwa
mujibu wa Dkt. Abbasi alisema kwa sasa yapo mambo makubwa na mazuri
hususani vivutio vya sekta ya utalii, hivyo kupitia nafasi yake ya
Ubalozi Serikali itatoa msaada wowote unaohitajiwa na mchezaji huyo ili
kuhakikisha kuwa vivutio vya Tanzania vinabainishwa na hivyo kutangaza
mambo mazuri ya Tanzania.
Aidha
Dkt. Abbasi alisema Ofisi yake imeandaa mikakati mbalimbali ya
mawasiliano ya kitaifa katika kuisema nchi katika maeneo mbalimbali
hivyo kumtaka mchezaji huyo kutumia majukwaa hayo kwa ajili ya kuona
namna bora ya kutumia fursa hizo ili kuitangaza Tanzania nje ya mipaka
yake.
Kwa
mujibu wa Dkt. Abbasi alimtaka mchezaji huyo kuwasiliana naye iwapo
kutakuwepo na changamoto yoyote anayoweza kuipata katika kutekeleza
majukumu yake ya nafasi ya Ubalozi kwani kwa sasa Serikali ya Awamu ya
Tano imefungua milango ya ushirikiano na wawekezaji wa ndani na nje ya
nchi ili kuhakikisha kuwa Tanzania inapiga hatua katika kuwaletea
maendeleo wananchi wake.
Kwa
upande wake, Nahodha huyo wa Taifa Stars, Mbwana Samatta alisema akiwa
nchini Ubelgiji tayari amefanya juhudi kubwa katika kutangaza vivutio
mbalimbali vya utalii vilivyopo nchini, ambapo mwanzoni mwa mwezi ujao
madaktari 5 wa timu hiyo wanatarajia kuja nchini kwa ajili ya kutembelea
maeneo mbalimbali ya utalii nchini.
Samatta
alisema raia wengi wa kigeni wana shauku ya kutembelea Tanzania
kutokana kusikia na kuona uzuri wa vivutio mbalimbali vya utalii ikiwemo
Wanyama, hivyo akiwa Balozi wa Utalii afanya kila liwezekanalo kukaa
karibu na viongozi na wachezaji wa klabu yake ya KRC Genk kuwaeleza
uzuri wa Tanzania ili na wao waonesha nia ya kuitembelea Tanzania.
“Wachezaji
wengi hususani wale wa kiafrika waliopo nje hususani Bara la Ulaya
wanaipenda sana Tanzania, na hi inatokana na sifa tuliyonayo, na hivyo
kwa kutumia nafasi yangu ya Ubalozi nitaendelea kushawishi waitembelee
Tanzania” alisema Samatta.
Kwa
upande wake, Mkurugenzi wa Kampuni ya Utalii ya Samatta Tours, Hamis
Waziri aliishukuru Serikali kutokana na jitihada mbalimbali inazofanya
kwa ajili ya kuhamasisha sekta ya utalii nchini na kusema taasisi hiyo
itakuwa tayari kutangaza matukio mbalimbali kwa ajili ya kulitangaza
jina la Tanzania.
No comments:
Post a Comment