JIJI LA DODOMA LAITIKIA KWA VITENDO KATAZO LA MATUMIZI YA MIFUKO YA PLASTIKI
Afisa Mazingira wa Jiji la Dodoma Ally
Mfinanga akizungumza na wananchi pamoja na wanafunzi wa Jamhuri
Sekondari baada ya zoezi la ukusanyaji wa mifuko ya plastiki katika
eneo linalizunguka Shule hiyo.
Diwani wa Kata ya Uhuru Jijini Dodoma,
Ally Kheri akizungumza baada ya tamati ya zoezi la ukusanyaji mifuko ya
plastiki kuzunguka shule ya sekondari Jamhuri zoezi lililoshirikisha
ofisi ya afisa mazingira na kampuni ya usafi ya Green West.
Meneja wa kampuni ya usafi ya Green West
Abdallah Mbena akizungumza baada ya tamati ya zoezi la ukusanyaji
mifuko ya plastiki kuzunguka shule ya sekondari Jamhuri.
Afisa mazingira wa kata ya Uhuru
akizungumza baada ya tamati ya zoezi la ukusanyaji mifuko ya plastiki
kuzunguka shule ya sekondari Jamhuri zoezi lililoshirikisha ofisi ya
afisa mazingira na kampuni ya usafi ya Green West.
Mwanafunzi wa kidato cha nne shule ya
sekondari Jamhuri Neema Leonard akizungumza baada ya tamati ya zoezi la
ukusanyaji mifuko ya plastiki kuzunguka shule ya sekondari Jamhuri zoezi
lililoshirikisha ofisi ya afisa mazingira na kampuni ya usafi ya Green
West.
Wafanya kazi wa kampuni ya usafi ya Green
West pamoja na wanafunzi wa shule ya Sekondari Jamhuri na baadhi ya
viongozi wakifanya usafi wa kuondoa mifuko kwa kutekeleza katazo la
Serikali kwa Mifuko ya Plastiki.
Sehemu ya picha ya pamoja baada ya kumaliza kufanya usafi kwa kukusanya mifuko.
Picha Zote na Alex Mathias-Wazo-huru blog
…………………
Na.Alex Mathias,Dodoma
Jiji la Dodoma katika kuunga mkono agizo
la serikali la kutokomeza matumizi ya mifuko ya plastiki ili kulinda
mazingira, limeanzisha mfumo wa kuwahamasisha wananchi kuondoa mifuko
hiyo katika mazingira yao, na kutoa elimu kuachana kabisa na matumizi
ya mifuko hiyo na kutumia mifuko mbadala.
Akizungumza wakati wa zoezi la hamasa
ilikuhamasisha wanachi kuondoa mifuko ya plastiki katika maeneo yao
afisa mazingira wa Jiji la Dodoma Ally Mfinanga, amesema wao kama jiji
wanaonyesha kwa vitendo kuitikia agizo hilo kwa kuwahamasisha wananchi
kuondoa mifuko hiyo ili kuacha mazingira yakiwa safi.
Sambamba na hilo amesema wanawaelimisha
wananchi kuacha na matumizi ya mifuko ya plastiki na kutumia mifuko
mbadala ili kuweka mazingira safi.
“ Tumeitikia kwa vitendo agizo la Waziri
mkuu la kuzuia matumizi ya mifuko ya plastiki, na sisi kama unavyoona
leo hii tupo shule ya sekondari jamhuri hapa, ni katika kutoa hamasa
kwa wananchi kuacha na matumizi ya mifuko ya Rambo ambayo inamadhara
makubwa katika ustwi wa mazingira”,
“Amesema wao kama jiji wanajitahidi
kuwafikia wananchi katika na kuwapa elimu ili watumie mifuko mbadala
tulinde mazingira yetu yawe na safi na sisi tuwe mfano kwa kuwa jiji
safi” amesema mfinanga.
Amesema endapo wananchi wote kwa pamoja
wakikubaliana kwa kauli moja kuachana matumizi ya mifuko ya plastiki
basi adhima ya serikali itafikiwa, amewakumbusha wanachi kuondoa mifuko
popote ilipo na atakaye kutwa anatumia mifuko hiyo faini ni shilingi
elfu therathini(30000).
Kwa upande wake Diwani wa kata ya Uhuru,
Ally Kheri ameshukuru wananchi kwa kujitikeza kwa wingi katika zoezi
hilo na kusema baada ya kusikia kampeni hiyo walikaa na kamati ya ODC na
kukubaliana kuanza na taasisi zilizopo katika kata hiyo.
Walianza na Shule ya Uhuru kasha
wakafuatia na sekondari ya Central na leo wamefika katika shule ya
Sekondari Jamhuri na kupata mwitikio mkubwa na zoezi kufanyika kwa
mafanikio mmakubwa sana.
“Kwanza nishukru kwa kufanikiwa kwa
zoezi hili na wanachi wameitikia kwa kiwango kikubwa sisi kama kata
baada ya kusikia kampeni hii tulikaa kamati ya ODC na tukakubaliana kuwa
tuanze na maeneo ya taasisi tulianza na shule ya Uhuru, Sekondari
Central na leo tupo hapa Jamhuri zoezi limefanikiwa kwa kiwango kikubwa
sana”
Kwa upande wake Meneja wa kampuni ya
usafi ya Green West Abdallah Mbena ameishukuru serikali kwa kupiga
marufuku matumizi ya mifuko ya plastiki kwani ilikuwa ikiletaufumbufu
katika kuweka mji safi lakini kwa sasa kazi yao itarahisishwa kwa
kiwango kikubwa.
No comments:
Post a Comment