ELIMU YA UFUNDI NI NYENZO KUELEKEA UCHUMI WA VIWANDA-NAIBU WAZIRI OLE NASHA
![](https://fullshangweblog.co.tz/wp-content/uploads/2019/05/1A-1.jpg)
Mwenyekiti wa baraza la elimu ya Ufundi
NACTE John Kondoro, kulia akimuelekeza jambo Naibu Waziri wa Elimu
Sayansi na Teknolojia Mhe.Wiliam Ole Nasha katikati, wakati akiwasili
kabla ya kufungwa kwa maonyesho hayo leo, kulia ni Naibu Katibu Mkuu
Averina Semakafu.
![](https://fullshangweblog.co.tz/wp-content/uploads/2019/05/1-79.jpg)
Mhadhiri wa chuo cha College of
Agriculture and Natural Resources, Deodatus Tibenda akitoa maelezo kwa
Naibu waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Mhe.Wiliam Ole Nasha, juu
ya shughuri zinazofanywa na chuo hicho kabla ya kufungwa kwa maadhimisho
hayo leo Jijini Dodoma.
![](https://fullshangweblog.co.tz/wp-content/uploads/2019/05/2-66.jpg)
Baadhi ya wawakilishi wa Taasisi
mbalimbali wakiwa katika hafla ya kufungwa kwa maonyesho ya kwanza ya
Elimu ya Ufundi yaliyofanyika Jijini Dodoma.
![](https://fullshangweblog.co.tz/wp-content/uploads/2019/05/3-58.jpg)
Mtendaji Mkuu wa Baraza la Elimu ya
Ufundi NACTE Adolph Rutayuga akizungumza wakati wa hafla ya kufungwa kwa
maonyesho ya kwanza ya Elimu ya Ufundi yaliyofanyika Jijini Dodoma.
![](https://fullshangweblog.co.tz/wp-content/uploads/2019/05/4-51.jpg)
Mwenyekiti wa Baraza la Elimu ya Ufundi
NACTE, John Kandoro, akizungumza wakati wa hafla ya kufungwa kwa
maonyesho ya kwanza ya Elimu ya Ufundi yaliyofanyika Jijini Dodoma.
![](https://fullshangweblog.co.tz/wp-content/uploads/2019/05/5B.jpg)
Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi a
Teknolojia Mhe.Wiliam Ole Nasha, akizungumza wakati wa hafla ya
kufungwa kwa maonyesho ya kwanza ya Elimu ya Ufundi yaliyofanyika
jijini Dodoma.
![](https://fullshangweblog.co.tz/wp-content/uploads/2019/05/6-27.jpg)
Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara,
Mhandisi Stella Manyanya, akiwapungia mikono wadau wa maonyesho ya Elimu
ya Ufundi, wakati wa hafla ya kufungwa kwa maonyesho ya kwanza ya
Elimu ya Ufundi yaliyofanyika Jijini Dodoma
![](https://fullshangweblog.co.tz/wp-content/uploads/2019/05/7C.jpg)
Naibu Waziri wa Elimu Sayansi na
Teknolojia Mhe.Wiliam Ole Nasha katikati waliokaa akiwa katika picha ya
pamoja na wadau na wamiliki wa taasisi zilizoshiriki katika maonyesho
ya kwanza ya Elimu ya Ufundi yaliyofanyika Jijini Dodoma.
Picha na Alex Sonna-Wazo-hurublog
………………
Na.Alex Mathias,Dodoma
Naibu Waziri wa Elimu Sayansi na
Teknolojia Mhe.Wiliam Ole Nasha, amesema elimu ya ufundi ni muhimu
katika maendeleo, kwa sababu inakuza taaluma hasa kipindi hiki cha
kutengeneza uchumi wa Viwanda.
Naibu Waziri Ole Nasha ametoa kauli hiyo
leo jijini Dodoma wakati akifunga maonyesho ya kwanza ya Elimu ya Ufundi
na Mafunzo yaliyofanyika uwanja wa Jamhuri Dodoma yenye lengo la
kukutanisha taasisi zote zilizochini ya NACTE.
Amesema kama Elimu ya Ufundi itasimamiwa
kikamilifu italeta tija hasa kipindi hiki tunajenga uchumi wa viwanda,
kwa sababu elimu ya ufundi inasaidia kukuza wataalamu ambao
watasaidia katika viwanda.
Aidha amefurahishwa katika maonyesho hayo
kuona vijana ambao ni mazao ya vyuo vya ufundi wakiwa na bidhaa
mbalimbali ambazo wamezitengeneza wenyewe na kujiajiri kupitia elimu ya
ufundi.
“Ndugu zangu nimepita kwenye mabanda
humo nimeona vijana ambao wametoka katika vyuo hivi na wamejiajiri na
wanafanya kazi nzuri sana, hii elimu ya ufundi ni muhimu sana inazalisha
wataalumu ambao watatusaidia katika viwanda na Nyanja mbalimbali
tunapojenga uchumi wa viwanda” amesema Ole Nasha.
Aidha amesema serikali itaendelea kuunga
mkono juhudi za wadau wa sekta binafsi ambao wanamalengo ya kuleta
mabadiliko kwa nchi hasa kipindi hiki cha ujenzi wa viwanda serikili
itakuwa bega kwa bega kuwaunga mkono kuhakikisha sekta hizo
zinasongambele.
Amesema serikali inathamini sana
uwekezaji wa sekta binafsi kwa sababu zinamchango mkubwa sana na hasa
katika kuinua elimu katika Nyanja mbalimbali hapa nchini.
“Ukiangalia hapa nchini kuna vyuo vya
ufundi mia tano arobaini(540) na vyuo binafsi ni mia tatu kumi na
tisa(319) vyote hivi ni vyuo vya watu binafsi vya serikali ni kama mia
mbili tu na kidogo, unaona sasa sekta binafsi ilivyo na mchango mkubwa”
amesema Ole Nasha.
Kwa upande wake Mtendaji mkuu wa baraza
la Elimu ya Ufundi nchini NACTE Adolph Rutayuga, amesema maonyesho hayo
yalikuwa na mafanikio makubwa, na wamedhamilia kuyafanya kuwa endelevu
na baraza litaendelea kuyaboresha ili kuwa bora zaidi.
Amesema lengo la maadhimisho hayo ni
kukuza taasisi hizo na kubadilishana uzoefu miongoni mwa taasisi hizo,
na ni fulsa kwa wanafunzi wa taasisi hizo kujiajiri na kubainisha kuwa
miongoni mwa waliokuwa wakitoa maelezo katika mabanda hayo ni wanafunzi
wa taasisi hizo.
“Mheshimiwa maadhimisho hayo yamekuwa ya
mafanikio sana na ili kuboresha zaidi kutekubaliana yawe ya kila mwaka
angalau mara moja kuzikutanisha taasisi hizi kukutana kwa pamoja,na
tumedhamilia katika maadhimisho yajayo kuongeza taasisi nyingi zaidi
katika maonyesho haya” amesema Rutayuga.
Maadhimisho haya yalianza tarehe 27 mwezi
huu nayamefungwa rasmi leo ambapo yamedumu kwa siku tano yaliyokuwa na
lengo la kukutanisha taasisi zote zilizopo chini ya NACTE ili
kuzitangaza taasisi hizo na maonyesho yalibebwa na kauli mbiu isemayo, “Elimu ya Ufundi na Mafunzo kwa Maendeleo ya Uchumi wa Viwanda Tanzania”.
No comments:
Post a Comment