Waziri wa Madini Doto Biteko (wa pili kushoto) akifuatilia hoja zilizotolewa na Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini na baadhi ya Wenyeviti wa kamati nyingine wakati wa semina ya wabunge iliyotolewa na wizara. Wa pili kulia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini Dustan Kitandula, wa kwanza kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Prof. Simon Msanjila na kwa kwanza kulia ni Katibu wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Nishati na Madini, Omary Magwinza.
Baadhi ya Watendaji na Wataalam kutoka Wizara na Taasisi zake wakifatilia uwasilishwaji mada uliotolewa na Wataalam wa Wizara ya Madini na taasisi zake.
Waziri wa Madini Doto Biteko na baadhi ya Watendaji na Wataalam wa Wizara na Taasisi zake wakijadiliana jambo baada ya kuhitimishwa kwa semina ya Wabunge wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madni na baadhi ya Wenyeviti wa kamati nyinginr iliyoandaliwa na wizara ya madini.
Imeelezwa
kuwa, Wizara ya Madini itaendelea kusimamia Uanzishwaji wa Masoko ya Madini
katika maeneo mbalimbali nchini huku ikiendelea kufanya marekebisho ya Kanuni za
Uanzishwaji wa masoko hayo.
Waziri
wa Madini Doto Biteko ameysema hayo Machi 31, 2019 wakati akifunga Semina ya
siku mbili iliyoandaliwa na wizara kwa Wabunge wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya
Nishati na Madini pamoja na baadhi ya Wenyeviti wa Kamati zenye uhusiano na
Sekta ya Madini.
Semina
hiyo ililenga kutoa elimu na kujenga uelewa wa pamoja kwa wabunge hao kuhusu
sekta ya madini ambapo mada mbalimbali ziliwasilishwa.
Mada
zilizowasilishwa ni pamoja na uanzishwaji wa masoko ya madini, mafanikio na
changamoto ya Shirika la Madini la Taifa STAMICO), elimu kuhusu majanga ya
asili (hasa matetemeko ya ardhi), ukaguzi migodini, biashara ya madini na
shughuli zinazofanywa na Taasisi ya Uwazi na uwajibikaji katika Rasiimali za
Madini, Mafuta na Gesi Asilia.
Waziri
Biteko aliongeza kuwa, Wizara itaendelea kuwaelea wadau wa madini huku
akiwataka kubadilika na kutenda matendo yenye manufaa kwa pande mbili na
kuwaomba wabunge hao kushirikiana na serikali katika kutoa elimu kwa wadau wa
madini ili waweze kuzingatia na kufuata taratibu zilizowekwa.
Pia,
alisema serikali itaendelea kufanya kaguzi migodini kwa lengo la kuhakikisha
wachimbaji wanachimba kwa usalama na kueleza kuwa, wizara imeomba kibali cha
kuongeza maeneo mengine ya ukaguzi wa madini na kusema,“ tumepanga kuongeza
vituo vingine 85”.
Aidha,
alizungumzia maeneo yenye wizi wa dhahabu katika maeneo ya kuchanjua madini
hayo na kuyataja kuwa ni Kahama na Chunya na kuwataka wahusika kuzingatia
sheria.
Akizungumzia
suala la kupunguza zaidi kodi kwa uchimbaji mdogo wa madini, alisema serikali
haitapunguza tena kodi hizo kwa sasa mpaka hapo itakapoona manufaa yake.
Ikumbukwe
kuwa, baada ya mkutano wa Kisekta uliofanyika Januari 22 mwaka huu chini ya
Uenyekiti wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli na
kuwashirikisha wadau mbalimbali wa madini baada ya wadau hao kuwasilisha kero
zao kubwa ikiwa kodi, serikali ilifanya mabadiliko na kuondoa kodi kwenye
uchimbaji mdogo wa madini kwa kuwafutia kodi ya ongezeko la thamani yaani
VAT (18%) na kodi ya zuio( withholding tax).
Mbali
na wajumbe wa kamati, wengine walioshiriki semina hiyo ni Wenyeviti wa Bodi za
Taasisi zilizo chini ya Wizara pamoja na Watendaji na Wataalam kutoka wizara na
taasisi zake.
No comments:
Post a Comment