Naibu
waziri Kilimo Mhe. Omari T. Mgumba (Mb)
akiwa ofisi ya mkuu wa mkoa wa arusha alipokutana na wataalamu wa kilimo
,ushirika na umwagiliaji kabla ya kuanza ziara ya kuzungukia maeneo
mbalmbali mkoani hapo.
Mwenyekiti
wa chama cha mapinduzi Mkoani Arusha
bwana Loata Erasto Sanare akieleza
jambao baada ya kutembelewa na Naibu
Waziri Kilimo Mhe. Omari T. Mgumba
katika ofisi ya chama hicho hivi karibuni.
Bashiri Salum, Wizara ya Kilimo - Arusha
Vyama
vya Ushirika vimeshauriwa kukopa fedha kwenye Mabenki kwa ajili ya wanachama wao kwa kuwa waliowengi
hawakopesheki hivyo kufanya shughuli za kilimo kuwa ngumu.
Akizungumza
katika kikao kilicho wakutanisha Maafisa Ushirika, umwagiliaji na afisa
kilimo Mkoani Arusha Naibu Waziri Kilimo
Mhe. Omari Mgumba amesema miundombinu mingi ya umwagiliaji inahitaji
marekebisho makubwa ili kuweza kutumiwa
na wakulima.
Aidha
miundombinu hiyo imekosa ukarabati kutokana na wakulima kutokuwa na mitaji ya
kutosha na kutoaminiwa na taasisi za fedha kusaidia ukarabati huo.
Ameshauri
tume ya Ushirika kuvisimia vyama vya ushirika ili viweze kukopa fedha Benki Kwa
ajili ya wanachama lengo likiwa ni kufanya ukarabati Wa miundombinu ya
umwagiliaji ambapo kila mwanachama atawajibika kuchangia huduma hiyo.
Hatuwezi
kufanya Kilimo cha kibiashara Kwa kutegemea mvua ambazo Nazo zimekuwa
haziyabiriki nawashauri tume ya Ushirika na tume umwagiliaji kusimamia vyama
hivyo kwenye skimu mbalimbali za umwagiliaji kukopa fedha ambazo zitatumika
kurekebisha miundombinu ya umwagiliaji badala ya kutegemea serikali .alisema
Mhe. Naibu Waziri
Naibu
Waziri aliwataka maafisa ugani kuwafikia wakulima na kuelimisha namna ya
kutumia na kutoa elimu juu ya matumizi bora ya viuatilifu vya mimea ili
kupambana na visumbufu vya mazao ambavyo vimekuwa vikimsababishia mkulima
hasara kubwa.
Naye
afisa Umwagiliaji wa kanda mhandisi Juma Mdete amesema katika ukanda huo eneo
ambalo linafaa kwa kilimo cha umwagiliaji ni hekta elfu 40 kati ya hilo
linalotumika ni hekta elifu 24 tu
Amesisitiza
kwamba pamoja na matumizi kidogo ya eneo la umwagiliaji lakini maeneo
yanayomwagiliwa yanasaidia upatikanaji wa chakula wakati wa ukame.
Akichangia
wakati wa mjadala huo Afisa Kilimo Mkoa wa Arusha Bwana Daniel Loiruck amethibitisha
kwamba ukiondoa Magonjwa ya mlipuko na uvamizi wa visumbufu vya mimea maafisa kilimo wamekuwa wakijitahidi
kuwafikia wakulima ili kutatua changamoto zinazowakabili.
Naye
mwenyekiti wa chama cha mapinduzi mkoani Arusha bwana Loata Erasto Sanare akamueleza Mhe. Naibu waziri kwamba hali ya
ukame mkoani humo ni kubwa hivyo kuishauri serikali kuanza kufikiri njia
mbadala ya kupambana na hali hiyo.
‘Msimu
wa kilimo upo katikati lakini mpaka sasa hakuna mvua na tumezunguka sehemu
mbalimbali hapa arusha mahindi yamekauka hata mvua ikinyesha haiwezi kuleta mabadiliko tunaishauri
serikali kufikiri mbinu za kukabiliana na hali hiyo’. Alisisitiza bwana Loata Sanare
No comments:
Post a Comment