Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akikagua maghala yaliyohifadhi korosho katika Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga wakati akiwa katika ziara ya kikazi mkoani Pwani Februari 19, 2019. (Picha Zote Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo)
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akikagua na madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga sambamba na wananchama wa Chama Cha Mapinduzi wakati akiwa katika ziara ya kikazi mkoani Pwani Februari 19, 2019.
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa Wilaya ya Kibiti mara baada ya kukagua maghala yaliyohifadhi korosho ya serikali wakati akiwa katika ziara ya kikazi mkoani Pwani Februari 19, 2019.
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akisalimiana na Afisa Kilimo wa Wilaya ya Mkuranga Bi Julitha Bulali alipotembelea Wilayani humo kwa ajili ya kukagua maghala yaliyohifadhi korosho wakati akiwa katika ziara ya kikazi mkoani Pwani Februari 19, 2019.
Na Mathias Canal,
Wizara ya Kilimo-Pwani
Sheria ya Korosho kifungu cha 12 hakimruhusu mtu yeyote
kufanya kazi ya korosho pasina kutambulika, wakati kifungu cha 15 cha sheria
hiyo katika kifungu kidogo cha nne kinawataka wahusika wote wa korosho wawe
wamesajiliwa na kuwa na leseni ya biashara hiyo.
Bila kuwa na usajili huo kwa mfanyabiashara yeyote wa korosho
ni kosa kisheria hivyo kwa atanayebainika anapaswa kuchukuliwa hatua kali za
kisheria.
Serikali imetilia msisitizo maagizo iliyoyatoa hivi karibuni
kuwa katika malipo ya wakulima wa korosho haitamlipa mfanyabiashara
asiyetambulika kisheria (Kangomba).
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) ameyasema hayo tarehe 19 Februari 2019 wakati akizungumza na
madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga wakati akiwa katika ziara ya
kikazi mkoani Pwani.
Mhe Hasunga amesema kuwa ni lazima sheria zifuatwe katika
utekelezaji wa majukumu yote ikiwemo biashara ya zao la korosho ili kuwanusuru
wakulima wanaotumia nguvu nyingi katika kilimo hicho huku wakipata matokeo duni
kutokana na baadhi ya wafanyabiashara wanaowahujumu (Kangomba).
Ameongeza kuwa wahujumu katika biashara za mazao mbalimbali
ya kilimo nchini katika kipindi kirefu wamekuwa wakiwanyanyasa wakulima kwa
kuwanyonya katika bei jambo ambalo serikali imelibaini hivyo kuingilia kati.
Aliongeza kuwa sababu ya wakulima kuchelewa kulipwa fedha za
korosho zao kutokana na uhakiki uliochukua muda mrefu umesababishwa na vyama
vya Ushirika kutofanya kazi yao ipasavyo kwa kuwasajili na kuwatambua wakulima.
“Vyama vya ushirika ndivyo vinapaswa kuwajua na kuwatambua
wakulima wake katika mazao yote yanayouzwa kupitia mfumo huo, vinginevyo
kutofanya kazi kwa weledi kumetuchelewesha kwa kiasi kikubwa” Alikaririwa Mhe
Hasunga na kuongeza kuwa
“Hata sheria yetu ya maghala haikufanya kazi vizuri, Vyama
vya msingi havikutekeleza majukumu yake”
Mhe Hasunga amesema kuwa serikali haitawavumilia wote wanaofanya
biashara hiyo kinyume na sheria badala yake watachukuliwa hatua za kisheria
ikiwemo kufunguliwa kesi za uhujumu uchumi.
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga ameanza ziara ya kikazi
mkoani Pwani, Lindi na Mtwara ambapo katika ziara hiyo atafuatilia mwenendo wa
malipo ya wakuli wa zao la korosho.
MWISHO.
No comments:
Post a Comment