Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan (kushoto) akikabidhi mfano wa hundi ya Mkopo uliotolewa na Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) yenye thamani ya Shilingi 1.28 bilioni kwa Mrajis Msaidizi wa Ushirika Mkoani Singida, Thomas Nyamba (wapili kulia) na Makamu Mwenyekiti wa Chama Kikuu cha Ushirika Singida, Yahya Ramadhan (kulia). Watatu kulia mwenye mawani ni mwakilishi wa Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Augustino Matutu Chacha. Hafla hii ilifanyika mjini Itigi, mkoani Singida mwishoni mwa wiki.
Baadhi ya wafanyakazi wa TADB wakiwa katika picha ya pamoja na Mrajis Msaidizi wa Ushirika Mkoani Singida, Thomas Nyamba (katikatia) na Makamu Mwenyekiti wa Chama Kikuu cha Ushirika Singida, Yahya Ramadhan (wapili kulia) mara baada ya kukadhiwa mfano wa hundi ya Mkopo na Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan.
Na Mwandishi wetu, Singida
Makamu wa Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu
Hassan amepongeza juhudi za Benki ya Maendeleo ya Kilimo
Tanzania (TADB) kwa kusaidia wakulima wadogo nchini hali inayoongeza uzalishaji
na kuwaongezea kipato wakulima hao.
Makamu wa Rais aliyasema
hayo wakati akikabidhi hundi ya mfano yenye thamani ya Shilingi 1.285
Billioni zilizotolewa na TADB kwa ajili ya miradi ya kilimo cha Alizeti kwa
wakulima 458 waliochini ya vyama vya ushirika (AMCOS) mkoani Singida.
Aliongeza kuwa wakulima
waliopatiwa mkopo huo hawana budi kuutumia katika kuongeza tija ya uzalishaji
ili kuweza kufikia malengo ya mkopo huo ambao umelenga kuchagiza kusaidia Sekta
ya Mbegu za Mafuta nchini ili kutanzua changamoto za ukosefu wa mafuta hapa
nchini.
Makamu wa Rais alitumia
fursa hiyo kuwaagiza viongozi wa ushirika mkoani Singida kusimamia kwa makini
mkopo huo ili utumike kwa malengo yaliyokusudiwa na kuhakikisha unarudi kwa
wakati ili uweze kusaidia wakulima wengine.
“Nawashi muwe waaminifu kwa
kuutumia mkopo huu vizuri na kuurudisha kwa wakati ili kuwawezesha wakulima
wengine nchini waweze kukopeshwa ili kuchagiza uzalishaji wa mazao ya kilimo,”
aliongeza.
Mapema akizungumza na
hadhara mjini Itigi ambapo mfano wa hundi hiyo ilipotolewa, Mkuu wa Mkoa wa Singida,
Dkt. Rehema Nchimbi alisema kuwa mkopo huo utachagiza hupatikanaji wa malighafi
kwa ajili ya viwanda 144 ya kusindika mafuta ya alizeti vilivyopo mkoani humo.
“Kwa kipekee tunaishukuru
TADB kwa kutoa mkopo kwa AMCOS hizi saba mkopo ambao umelenga kuongeza tija ya
uzalishaji wa alizeti hali itakayochangia hupatikanaji wa malighafi ya uhakika
ya viwanda vyetu,” alisema.
Kwa upande wake, mwakilishi
wa Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo ambaye ni Mkurugenzi wa Mikopo na
Biashara, Augustino Matutu Chacha, alisema kuwa kwa msimu huu wa mwaka
2018/2019, benki imeidhinisha mikopo ya jumla ya shilingi Bilioni 3.506 kwa
miradi ya Kilimo ya Mkoa wa Singida pekee, ambapo Shilingi 1.285 Billioni
zimetolewa kwa ajili ya miradi ya kilimo cha Alizeti kwa wakulima 458 waliochini
ya vyama vya ushirika (AMCOS) na Shilingi 2.221 Billioni kwa ajili ya ujenzi wa
Kiwanda cha kusindika mbegu za mafuta ya alizeti kitakachojengwa katika
Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni.
“Tunatambua Alizeti kama
mojawapo ya mazao ya kimkakati kwa uchumi wa taifa letu na hasa kwa wananchi wa
mikoa inayozalisha zao hili kwa wingi ikiwamo mkoa wa Singida. Zao hili la
Alizeti lina fursa kubwa ya kuliingizia taifa fedha za kigeni na pia ni chanzo
cha ajira kwa watu wapatao laki 3 na zaidi,” alisema.
Aliongeza kuwa Mkakati wa
benki hiyo ni kuendelea kusaidia wakulima kuongeza uzalishaji wa Alizeti zenye
ubora kwa ajili ya kusaidia viwanda vya ndani kupata malighafi.
Aliongeza kuwa benki
imefanya mazungumzo na inatarajia kukutana na wadau wasindikaji wa mafuta ya
kula kwa lengo la kuandaa mpango shirikishi wa kutoa huduma za pembejeo na
mafunzo ya kilimo bora kwa wakulima.
“Benki ina mkakati wa
kuwaunganisha wakulima na wasindikaji kwa ajili ya kupata huduma nafuu za
pembejeo za kilimo,” aliongeza.
Mmoja wa wanufaika wa mkopo
huo, amabaye ni Makamu Mwenyekiti wa Chama Kikuu cha Ushirika, Yahya Ramadhan
alisema kuwa ujio wa Benki ya Kilimo umerudisha ari ya wakulima wa zao la
alizeti mkoani Singida ambao kwa takribani miaka nane wameshindwa kulima kwa
tija kutokana na ukosefu wa fedha kwa ajili ya ununuzi wa pembejeo za kilimo.
“Kwa hakika mkopo huu
umerudisha ari ya wakulima kwani unatuhakikishia hupatikanaji wa pembejeo na
zana za kilimo kwa wakati hali itakayoongeza uzalishaji wa alizeti,” alisema.
No comments:
Post a Comment