Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisoma hotuba ya
kuahirisha Bunge jijini Dodoma, Februari 9, 2019. (Picha na Ofisi ya
Waziri Mkuu)
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ametoa siku
21 kwa viwanda vyote vinavyozalisha
vileo nchini viwe vimefunga mfumo ukusanyaji kodi kwa kutumia stempu za
kielektroniki.
Pia
ameziagiza Wizara na Taasisi zote za Umma ziwe zimejiunga na
Mfumo wa Serikali wa Kielektroniki wa ukusanyaji na usimamizi wa maduhuli
(GePG) kabla ya Juni mwaka huu.
Ametoa
maagizo hayo leo (Jumamosi, Februari 9, 2019) , wakati
akiahirisha mkutano wa kumi na nne wa Bunge la kumi na moja, Bungeni jijini
Dodoma.
Waziri Mkuu amesema Mamlaka ya Mapato
Tanzania (TRA) isimamie uwekaji wa mifumo hiyo na ifikapo februari
28, 2019 kila kiwanda kiwe kimefunga mfumo huo.
“Naielekeza
TRA kusimamia uwekaji wa mifumo ya kukusanya kodi za vileo kwa kutumia stempu
za kielektroniki kwa viwanda vyote vinavyozalisha vinywaji hivyo.”
Pia,
Waziri Mkuu amesema Serikali
inaendelea kuchukua hatua za kuongeza mapato na kuimarisha usimamizi wa
matumizi ya fedha na rasilimali za umma ili kufikia malengo.
Miongoni mwa mikakati hiyo ni kutumia mfumo wa
kielektroniki wa stempu za kodi kwenye viwanda vinavyozalisha bidhaa
zinazotozwa ushuru wa bidhaa na zile zinazoingizwa nchini.
Waziri
Mkuu amesema mfumo huo utasaidia Serikali katika kupata taarifa sahihi za
uzalishaji na kupunguza uvujaji wa mapato ya Serikali.
Wakati huo huo, Waziri Mkuu amesema
Serikali imeendelea kutekeleza maelekezo ya Rais Dkt. John Magufuli aliyoyatoa
Januari 22, 2019, alipokutana na wadau wa sekta ya madini.
AmesemaSerikali imefutaKodi
ya Ongezeko la Thamani (VAT) na Kodi ya Zuio ya asilimia tano ya
mwisho inayotozwa kwenye bei ya kuuzia madini ya aina zote kwa wachimbaji
hao.
Waziri
Mkuu amesema hatua hiyo inatarajiwa kupunguza utoroshwaji wa madini; kuwatambua
wachimbaji wadogo kupitia masoko ya madini yatakayoanzishwa.
Pia
itasaidia kuwapunguzia gharama wachimbaji wadogo na hivyo kuendesha shughuli
zao kwa ufanisi pamoja na kuongeza wigo wa mapato kwa kuwa madini yatauzwa
ndani ya nchi.
“Nitoe
rai kwa wachimbaji wote wadogo kushirikiana na Mamlaka mbalimbali za Serikali
kutekeleza maazimio yaliyofikiwa katika kikao na Mheshimiwa Rais.”
Amesema siku zote Watanzania wanamuenzi
Rais Dkt. John Magufuli, kwa hatua za makusudi anazochukua katika kuhakikisha
anaimarisha mifumo ya ukusanyaji wa mapato.
Waziri Mkuu amesema Rais Dkt. Magufuli
anafanya hayo yote kwa lengo la kuona Tanzania inapunguza utegemezi wa misaada
kutoka katika mataifa mengine.
“Mifano maelekezo aliyoyatoa kwa
Mawaziri, Wakuu wa Mikoa wawasilishe mapendekezo kuhusu namna bora ya kuongeza
ukusanyaji wa mapato ya ndani katika maeneo yao.”
Waziri Mkuu amesema tayari Serikali
imeshapokea mapendekezo hayo na imetoa maagizo mahsusi kwa TRA na TAMISEMI
zishirikiane katika ukusanyaji wa kodi za majengo.
Akizungumzia
kuhusu hali ya uchumi, Waziri Mkuu amesema imeendelea kuimarika, ambapo kati ya
Januari hadi Septemba 2018, pato la Taifa lilikua kwa wastani wa asilimia 6.7
ikilinganishwa na asilimia 6.2 katika kipindi kama hicho mwaka 2017.
AmesemaOngezeko hilo la ukuaji wa
uchumi limechochewa zaidi na uwekezaji mkubwa kwenye miundombinu hususan ujenzi
wa barabara, reli na viwanja vya ndege.
Waziri Mkuu amesema masuala mengine yaliyochangia ukuaji
mzuri wa uchumi ni kutengemaa kwa upatikanaji wa nishati na hali nzuri ya
hewa kwa upande wa kilimo.
“Shughuli za kiuchumi zilizoendelea
kutoa mchango mkubwa katika pato la Taifa kwa kipindi hicho ni kilimo (asilimia
33.4), ujenzi (asilimia 15.7) na biashara (asilimia 10.2).”
Amesema kutokana na umuhimu wa sekta ya
kilimo, Serikali itaendelea kuboresha miundombinu ya umwagiliaji, kuhakikisha
pembejeo za kilimo zinapatikana kwa wakati.
Pia kuhakikisha huduma za ugani
zinaimarishwa katika maeneo yote nchini pamoja na kuboresha
upatikanaji wa miundombinu ya hifadhi na masoko.
Lengo la Serikali ni kuongeza tija
kwenye uzalishaji wa mazao ya kilimo na hivyo kumwongezea kipato mkulima
kitakachomwezesha kujikimu na kujikwamua na umaskini.
No comments:
Post a Comment