Sunday, February 10, 2019

MAKAMU WA RAIS AONGOZA KIKAO CHA MASUALA YA MUUNGANO DODOMA

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiongoza Kikao cha Kamati ya Pamoja ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (SMT) na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ)  kujadili masuala ya Muungano. Kikao hicho kimefanyika leo Februari 9, 2019 katika ukumbi wa Kambarage, jengo la Hazina Square, Dodoma. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais).
 Sehemu ya Mawaziri kutoka Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) wakifuatilia kwa makini Kikao cha Kamati ya Pamoja ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (SMT) na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ)  kujadili masuala ya Muungano. Kikao hicho kimefanyika leo Februari 9, 2019 katika ukumbi wa Kambarage, jengo la Hazina Square, Dodoma. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais).
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimkabidhi Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif ali Iddi (kushoto) hati ya umiliki wa ardhi  yenye ukubwa wa hekari 30 kwenye mji wa Serikali Dodoma kwa ajili ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar wakati wa ufunguzi wa Kikao cha Kamati ya Pamoja ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (SMT) na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ)  kujadili masuala ya Muungano. Kikao hicho kimefanyika leo Februari 9, 2019 katika ukumbi wa Kambarage, jengo la Hazina Square, Dodoma. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais).

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba akihutubia wakati wa kikao cha Kamati ya Pamoja ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (SMT) na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ)  kujadili masuala ya Muungano. Kikao hicho kimefanyika leo Februari 9, 2019 katika ukumbi wa Kambarage, jengo la Hazina Square, Dodoma. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais).



Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amesema vikao vya masuala ya Muungano vinaendeshwa kirafiki kama ndugu wawili ambao wamekaa na kujadili mambo yao.

Makamu wa Rais ameyasema hayo wakati wa ufunguzi wa kikao cha Kamati ya Pamoja ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (SMT) na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) kujadili masuala ya Muungano kilichofanyika februari 9, 2019 katika ukumbi wa Kambarage, Jengo la Hazina Square, Dodoma.

“Vikao hivi vina mambo mengi mchanganyiko si sheria na katiba peke yake vinavyofanya kazi kuna mengine, consideration zingine zinabidi ziingie ili kupata njia sahihi” alisema Makamu wa Rais

Kwa upande wake Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi alikabidhi kiwanja chenye ukubwa wa hekari 30 kilichopo kwenye eneo la mji wa Serikali Dodoma kwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar bila gharama yeyote kama alivyoelekeza Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli.

“kiwanja ni kikubwa sawa na viwanja vilivyotolewa kwa Wizara 10 za bara” alisema Waziri Lukuvi.

Awali Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba alisema kikao hicho ni cha kawaida ambacho kimejadili masuala ya Muungano na kilitanguliwa na vikao vingine vilivyojumisha Makatibu Wakuu pamoja na Mawaziri.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan alikabidhi hati ya umilikiwa wa kiwanja hicho chenye ukubwa wa hekari 30 kilichopo mji wa Serikali Dodoma kwa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Iddi.

Kikao hicho cha Kamati ya Pamoja ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (SMT) na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) kujadili masuala ya Muungano kilihudhuriwa na Mawaziri wa Serikali zote mbili pamoja na Makatibu Wakuu na Timu ya Wataalamu.

No comments:

Post a Comment