Waziri wa Madini Doto Biteko akiweka Jiwe la Msingi katika Kituo Cha Pamoja Cha Biashara ya Madini. Pamoja naye ni Mbunge wa Simanjro, James Ole Millya , Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Prof.Simon Msanjila na Mkuu wa Wilaya ya Simanjiro, Mhandisi Zephania Chaula.
Waziri wa Madini Doto Biteko akifuatilia jambo baada ya kuweka Jiwe la Msingi Kituo cha Pamoja Cha Biashara, eneo la Mirerani. Wengine wa kwanza kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Alexander Mnyeti, Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, Dustan Kitandula. Kulia ni mwanzo ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini Prof. Simon Msanjila.
Waziri wa Madini Doto Biteko Sambamba na Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Alexander Mnyeti pamoja na wageni waloshiriki hafla ya uzinduzi wa Jengo la Biashara na Uthaminishaji Madini, wakielekea mahali kunakojengwa Kituo cha Pamoja Cha Biashara ya Madini.
Ø
ASEMA ATAKAYEKAMATWA NA TANZANITE
MARUFUKU KUINGIA TENA NDANI YA UKUTA.
Ø
ATAKA MINADA YA TANZANITE
ILIYOSIMAMISHWA SASA IANZE.
Ø SUMA JKT msitucheleweshe,
ifikapo Aprili mwaka huu jengo liwe limekamilika. Jengo hili la Kituo
cha Pamoja cha Biashara ya Madini litajengwa na SUMA JKT kwa gharama ya
shilingi 1,148, 259,500.
Ø Tunafunga CCTV camera kuzunguka
ukuta. Lengo la uwekaji wa mitambo hii ni kuimarisha ulinzi kwa ajili ya
rasilimali na watu waliomo na wanaoingia ndani ya ukuta. Tunataka tukiwa
Dar es Salaam na Dodoma tuwaone. Rai yangu kwenu ni kila mtu awe mlinzi wa
rasilimali madini na kwa upande wafanyabiashara wapende kununua katika mkondo
sahihi madini yao ili kuepuka usumbufu.
Ø
Tarehe 30
Januari 2019 nilisaini Kanuni za Mirerani Controlled Area. Nakuagiza Mkuu wa
Wilaya ya Simanjiro Kamati ianze kazi tuanze kusimamia Kanuni hizi.
Ø
Tumekuja
kumkabidhi mkandarasi site hakuna kulala mpaka madini yalinufaishe taifa.
Ø
Mkandarasi
wa CCTV nakukabidhi kazi hii nataka ufanye kazi yenye ubora na kumaliza ndani
ya Mkataba tuliokubaliana bila kuongeza hata sekunde.
Ø
Tulieni
tunakuja na utaratibu wa mashine. Wizi ni lazima tuutoe kwenye fikra
zenu.
Ø
Wakati
ukuta huu unajengwa kulikuwa na siasa nyingi. Wapo waliouita jela lakini
leo mapato yameongezeka mnalipa kodi vizuri. Tunakwenda kuondoa vikwazo kwenye
biashara ya madini. Mtalipa mrabaha usiozidi asilimia 7. Deni limebaki kwenu.
Ø
Suala
kujengwa ukuta lilikuwepo tangu mwaka 2002 lakini haukujengwa. Ametokea
mzalendo Rais Magufuli tumejenga. Asingekuwa yeye ingebaki hadithi nyingine.
Ø
Nitawashangaa
sana baada ya jitihada hizi tunazozifanya mapato yakishuka. Mkuu wa Mkoa
wasimamieni hawa huku mkiwalea.
Ø
Jengo la
biashara ya madini limejengwa mahususi ili kurahisisha uthaminishaji wa madini
pindi yanapovunwa hapa ndani.Ma broker tumewajengea nyumba hii hapa tuheshimu
taratibu.
Ø Jengo hili la biashara na
uthaminishaji litatumika kuwakutanisha wafanyabiashara wadogo na wenye madini
ili kuweza kufanya biashara sehemu salama na kwa uwazi. Kama alivyosema
Katibu Mkuu, jengo hili limegharimu shilingi milioni 85.
Ø
Tanzania
Tumegeuka kuwa darasa kwa jirani zetu na nchi nyingine kutokana na namna
tunavyosimamia Sekta ya madini. Watu wa mataifa wanakuja kujifunza lakini pia
Tunapata mialiko mingi kutoka nchi mbalimbali ili tuwaeleze namna
tunavyosimamia rasilimali hii.
Ø Tutumie madini yetu kubadilisha
maisha yetu. Tunataka siku moja watoto wa Simanjiro wasome kwenye shule nzuri,
watumie barabara nzuri, akina mama wapate huduma za afya sehemu nzuri. Haya
ndiyo mambo tunayoyataka. Siasa nyingine siyo agenda ya watanzania.
Ø Tanzania ni nchi ya 3 Afrika kwa
kuzalisha dhahabu, ya pili Afrka kwa madini ya vito na ya 18 duniani kwa
kuzalisha dhahabu lakini utajiri huu wa madini na maisha ya watanzania havifanani.
Ø Minada ya Tanzanite iliyosimamishwa
sasa ianze.
Ø Chama Cha MAREMA unganeni,tukigundua
hamna msaada tutawaacha.
Ø Hatutaki kukwamishana,tunataka
kusimamia sekta..Wachimbaji acheni majungu, toeni taarifa za kweli.
Ø Hatutawatoza fedha nyingi lakini
mtatuonesha vitambulisho. Natoa maelekezo kuanzia leo tozo za kiingilio
zitatozwa kwa wale wanaofanya kazi. Ndani ya mgodi watalipa shilingi elfu
50,000 kwa mwaka, Mabroker watalipa shilingi elfu 30,000 kwa mwaka na wana
Appolo, wafanyabiashara wadogo kama wachekechaji, mama lishe watalipa shilingi
20,000 kwa mwaka.
Ø Naomba Wizara ya Kazi kupitia Mfuko
wa fidia kwa wafanyakazi ( WCF) na Mifuko ya Hifadhi ya Jamii kuja
kujifunza na kutengeneza muundo ambao unaendana na aina ya kundi hili ili
kuweza kulihudumia kundi hili la wachimbaji wadogo wa madini.
Ø
Katika
mkutano wa wadau wa tarehe 22 Januari, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Dkt. John Magufuli pamoja na mambo mengine alisisitiza kuimarisha
mazingira ya ufanyaji biashara ya Madini Tanzania na pia kuimairisha usalama.
Tuliagizwa kiualisia kuanza mara moja kuweka mifumo ya kidigitali kuzunguka
ukuta.
ALIYOYASEMA MKUU WA MKOA WA MANYARA ALEXANDER MNYETI
Ø Mkoa wa Manyara ni mkoa mkubwa wenye
Tanzanite ambayo haipo popote duniani. Unapokuwa Mkuu wa Mkoa kama huu
lazima uweze kudhibiti Tanzanite. Nataka nikamwambie Mhe. Waziri tuna
madini mengi zaidi ya Tanzanite.
Ø
Kwenye
madini lazima nibanane na wewe. Nisipodhibiti sina cha kumwambia Mhe. Rais.
Tutapambana mpaka dakika ya mwisho kuhakikisha kodi zinapatikana. Babati tuna
rubi ya kutosha. Nataka nikwambie ifanye Babati kuwa Makao Makuu ya Madini nchi
nzima.
Ø Mhe. Waziri kazi yetu ni kusimamia
mnayoyapitisha juu ili yasipotoshwe na yatekelezwe kwa Mujibu wa Sheria.
Ø Mhe. Rais alituelekeza tupitie na
kukubaliana kuweka mazingira mazuri ya kuboresha Tanzania kupitia sekta hii.
Tulikaa kujadili mabadiliko makubwa. Nina hakika mabadiliko makubwa yanakuja.
Ø Mhe. Waziri tumeshakubaliana na wadau
hawa mambo mengi. Tunataka kuona mengi kutoka kwao.
Ø Ni matarajio yangu kuwa shughuli
nyingi zitafanyika ndani ya jengo la Kituo cha Biashara.
Ø Nakipongeza Chama Cha Marema kwa
kufanya kazi nzuri. Ukipingana na Serikali hakuna unachoweza kufanya. Hakuna
aliye juu ya serikali.
ALIYOYASEMA MWENYEKITI WA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA
NISHATI NA MADINI, DUSTAN KITANDULA
Ø Mhe. Rais ameonesha uungwana, mpira
uko kwenu. Hisani pekee kwake ni ninyi kulipa kwa kuonesha kwa vitendo. Yale
yaliyokuwa yakiwakwaza yameondoka, mlipe kodi.
Ø Tumewaona mkiwa katika maandamano ya
kumuunga mkono Rais. Kikao cha Januari 22 kilionesha dhamira ya Rais na
aliahidi kutekeleza kero zenu ndani ya kipindi kifupi. Tuliletewa miswada
kufanya mabadiliko.
Ø Nampongeza Rais kwa kuondoa vikwazo
kwa wachimbaji wadogo. Serikali imedhamiria kuhakikisha sekta hii inalinufaisha
taifa.
ALIYOYASEMA MBUNGE WA SIMANJIRO JAMES OLLE MILLYA
Ø Kuwepo kwa ukuta huu hakumaanishi
hakuna majirani. Kwa mujibu wa Sheria na taratibu zake nakuomba
Mhe Waziri migodi hii isaidie jamii. Wanaofanya uchimbaji wakumbuke
vijiji vya jirani.
Ø Baada ya kujengwa ukuta bado
wanapanga mistari mirefu. Wanaongia ndani wakaguliwe mapema.
Ø Bado kuna changamoto kwako Mhe.
Waziri na Katibu Mkuu ikiwezekana muwaletee maji.
ALIYOYASEMA MWENYEKITI WA MAREMA, JUSTIN NYARI
Ø Mhe. Rais ameweka alama ambayo
haitapotea, alama ambayo itakumbukwa kwa vizazi na vizazi.
Ø Ujenzi wa kituo cha pamoja cha
biashara ni mwanzo mzuri kwetu na mkoa wetu na nchi yetu, wachimbaji wako
tayari kushirikiana na serikali.
No comments:
Post a Comment