Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo akiwa katika picha pamoja na makundi mbalimbali yaliyoshiriki mkutano wa wizara na hafla ya kuwaaga wastaafu kutoka Chuo Cha Madini (MRI) na Wizara ya Madini Makao Makuu
Naibu
Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo amewataka watumishi wa wizara kuhakikisha
wanatoa huduma stahiki kwa watanzania ili kuendana na kasi ya Serikali ya Awamu
ya Tano ya Rais John Pombe Joseph Magufuli.
Aidha,
amewataka watumishi hao, kila mmoja kulingana na majukumu yake kujipima utendaji wake binafsi kabla ya
kungoja vipimo vilivyopo kwa kuzingatia miongozo na taratibu za Utumishi wa
Umma.
Naibu
Waziri Nyongo, ametoa kauli hiyo leo alipokuwa akifungua Mkutano wa Wafanyakazi
wa Wizara kwa niaba ya Waziri wa Madini, Doto Biteko aliyekuwa katika
utekelezaji wa majukumu mengine ya kitaifa.
Aidha,
Nyongo amewaeleza watumishi hao kuwa wanao wajibu wa kuzingatia dhana nzima ya
kuongeza ufanisi na tija katika utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku kwa
manufaa ya Taifa na watanzania kwa ujumla.
Pamoja
na rai ya kila mtumishi kujipima utendaji wake, Nyongo amewakumbusha kuzingatia
matumizi ya Opras katika kutekeleza na kujipima namna kila mmoja anavyotekeleza
majukumu yake.
Amesema Opras ni hitaji la kisheria kila mmoja hanabudi
kulizingatia.
“Wote
tnafahamu kuwa ipo miongozo mbalimbali inayotumika katika utendaji wetu wa kila
siku hivyo ni rai yangu kuwa tuizingatie ili kutoa huduma stahiki kwa
watanzania kwa ufanisi na viwango vinavyotakiwa.” Alisisitiza .
Aidha,
Nyongo alieleza wajibu wa Wizara kwa kuzingatia miongozo iliyopo ikiwa ni
pamoja na kuweka mazingira mazuri ya kazi yatakayowawezesha watumishi wake
kutekeleza majukumu yao ipasavyo.
Pamoja
na hilo, alikazia suala la kuwaendeleza watumishi, kuwajengea uwezo katika kazi
zao pamoja na kushughulikia na kutatua changamoto zinazowakabili katika maeneo
yao ya kazi.
Zaidi
ya hapo, Nyongo alisisitiza suala la kuimarisha mawasiliano baina ya watumishi
wa wizara lakini pia mawasiliano baina ya wizara na taasisi zilizo chini ya
wizara na wadau wote wa sekta ya madini ili kuongeza ufanisi hatimaye kuongeza
tija katika utendaji wa wizara.
Kuhusu
kuzingatia suala la afya za watumishi, Nyongo ameipongeza wizara kwa kuratibu
mara kwa mara suala la upimaji wa afya kwa hiari kwa watumishi wake na kutoa
rai kwa kila mmoja kutumia fursa hiyo na kujitokeza kupima afya zao kwa hiari.
Akihitimisha
hotuba yake, Nyongo amewasihi watumishi wa wizara kuongeza juhudi na
kuelekeza fikra zao katika kupelekea serikali ya viwanda kutokana na ukweli
kwamba sekta ya madini ni mojawapo ya nguzo ya uchumi wa viwanda na kuwa
itasaidia katika kuifikisha Tanzania kuwa miongoni mwa nchi zenye uchumi wa
kati ifikapo 2025.
Kutokana
na uwepo wa wastaafu katika mkutano huo, Nyongo alitumia fursa hiyo kuwapongeza
sana wastaafu watano walijumuika katika mkutano na hafla fupi ya kuwaaga na
kuwatakia maisha mema katika hatua nyingine ya maisha.
Kwa
uande wake, Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Utawala na Rasilimali Watu Nsajigwa
Kabigi kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Prof. Simon Msanjila
alisema mkutano huo umelenga katika kujadili masuala mbalimbali ya kiutendaji
ya wizara ili kupata mwelekeo wa namna bora ya kuleta ufanisi katika kutekeleza
majukumu na shughuli za kila siku za wizara pamoja na kubadilishana mawazo,
kufurahi pamoja na kuwaaga wastaafu.
No comments:
Post a Comment