Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi,Ajira na Wenye Ulemavu anayeshughulikia walemavu, Mhe. Stella Ikupa( katikati kwa walioketi) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa Mkoa wa Simiyu na watumishi wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii Mkoani Simiyu(NSSF na PSSSF) mara baada ya kutembelea ofisi za mifuko hiyo wakati wa ziara yake mkoani Simiyu , Februari 25, 2019.
Na
Stella Kalinga, Simiyu
Naibu
Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya watu wenye
ulemavu, Mhe.Stella Ikupa ametoa wito kwa viongozi wa vyama vya watu
wenye ulemavu, kuwahamasisha wanachama wao kujiunga na mfuko
wa afya ya jamii (CHF )ulioboreshwa ili waweze kupata uhakika wa matibabu.
IKUPA
ametoa wito huo wilayani Itilima katika ziara yake wakati
akizungumza na viongozi wa Wilaya, Viongozi wa Vyama vya wenye ulemavu na
baadhi ya wenye ulemavu wenyewe wakati wa ziara yake wilayani humo
Februari 25, 2019, ambayo ililenga kukagua utekelezaji wa maelekezo ya Serikali
ikiwa ni pamoja na mradi wa Kitalu nyumba na masuala mbalimbali yahusuyo wenye
walemavu.
Amesema
ni vema viongozi wa vyama na wenye ulemavu wakapena taarifa na kuhamasishani
kujiunga na mfuko wa Afya ya Jamii(CHF) ulioboreshwa, ili wapewe vitambulisho
waweze kutibiwa kirahisi.
“Mkijiunga
na CHF iliyoboreshwa mkapata kadi mtakuwa na uwezo wa kutibiwa muda wowote, kwa
hiyo peaneni hizo taarifa mjiunge watu mnaofahamiana muweze kupewa hivyo vitambulisho
mpate kutibiwa kirahisi wakati tukiwa tunasubiri ile bima ya afya kwa kila
Mtanzania” alisema Mhe. Ikupa.
Katika
hatua nyingine amewaagiza maafisa Ustawi wa jamii na maendeleo ya jamii kutoa
elimu vijijini kwa watu wenye ulemavu kuhusiana na uundwaji
wa vikundi na namna ya kutekeleza miradi mbalimbali.
Mkuu wa Wilaya ya Itilima,Mhe.
Benson Kilangi akizungumzia utekelezaji wa mradi wa kitalu nyumba amesema
katika awamu ya kwanza jumla ya vijana 20 wamepata mafunzo ya utengenezaji wa
vitalu nyumba na kufundishwa stadi mbalimbali za kuendesha kilimo biashara na
kuongeza mnyororo wa thamani.
Naye Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,
Mhe. Festo Kiswaga amesema miradi ya vitalu katika Mkoa wa Simiyu
itatekelezwa kwa viwango na kwa malengo yaliyokusudiwa, huku akibainisha kuwa
vitasaidia kuongeza kipato kwa wananchi katika mkoa na kuwa sehemu ya
wananchi kujifunza kilimo bora.
Kwa upande wao viongozi pamoja na
watu wenye ulemavu walioshiriki katika ziara hiyo wamemwomba Mhe. Naibu Waziri
kushughulikia baadhi ya changamoto zinazowakabili katika maeneo yao.
“Ninaomba Serikali itusaidie tuweze
kupata wakalimani wa lugha ya alama ili na sisi walemavu wa kusikia tuweze
kupata ujumbe unaokuwa unawasilishwa na viongozi wetu kwenye mikutano na ziara
kama hii ya leo hii itatusaidia sana” alisema Mhandi Ntobi Mwenyekiti wa Chama
cha Walemavu wasiosikia Mkoa wa Simiyu.
“NaombaWataalam waje watutembelee
kwenye vijiji vyetu na kwenye vyama vyetu watusaidie kutupa elimu ya namna ya
kuunda vikundi na namna ya kufanya shughuli zinazoweza kutuongezea kipato” Bw.
Seni Jitabo mlemavu wa viungo Mkazi wa Zagayu wilayani Itilima.
Naibu Waziri Ikupa, anaendelea na
ziara yake Mkoani Simiyu ambayo itahitimishwa 27 Februari 2019, akiwa wilayani
Itilima Naibu waziri ametembelea kitalu nyumba kilichopo Lagangabilili na kituo
cha maarifa ya jamii Kanadi, ambako amejionea shughuli mbalimbali za uzalishaji
zinazofanywa na vijana.
MWISHO
No comments:
Post a Comment