Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akikata utepe kufungua jengo jipya la
Taasisi ya Karume ya Sayansi na Teknolojia, iliyopo Mbweni Wilayani Magharibi
“B” - Unguja Januari 8, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiweka jiwe la msingi wa jengo jipya la
Taasisi ya Karume ya Sayansi na Teknolojia, iliyopo Mbweni Wilayani Magharibi
“B” - Unguja Januari 8, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiangalia kitabu kwenye maktaba ya jengo
jipya la Taasisi ya Karume ya Sayansi na Teknolojia, iliyopo Mbweni Wilayani
Magharibi “B” – Unguja baada ya kufungua jengo hilo Januari 8, 2019. (Picha na
Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu Kassim
Majaliwa akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Magharibi “B” Silima Haji Haji,
wakati akiwasili Zanzibar kwa ziara ya kikazi ya siku moja Januari 8, 2019.
(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amefungua
Jengo la Taasisi ya Karume ya Sayansi na Teknolojia (KIST), wilaya ya Magharibi
‘B’ lililojengwa kwa ghararama ya sh. bilioni 4.2.
Afungua
jengo hilo leo (Jumanne, Januari 8, 2019) ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya
sherehe za miaka 55 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar yaliyotokea Januari 12,
1964.
Waziri
Mkuu amesema kukamilika kwa Jengo la taasisi hiyo kuna manufaa makubwa kwa
jamii ikiwemo kutoa elimu ya ufundi itakayowasaidia vijana kujiajiri na
kuondokana na utegemezi.
“Kusaidia
azma ya Serikali ya kufikia uchumi wa kati ifikapo 2025 na msukumo katika sekta
ya viwanda kwa vijana kujiajiri na kuajiriwa katika sehemu mbalimbali pamoja na
Serikalini.”
Amesema
manufaa mengine ya KIST ni kutoa mafunzo ya fani mbalimbali zinazokwenda
sambamba na mabadiliko ya ulimwengu katika Nyanja za sayansi, teknolojia na
ualimu.
Kadhalika,
Waziri Mkuu ameutaka uongozi wa KIST ubuni mbinu mbalimbali na utafute miradi
mingine ya ujenzi itakayosaidia kuwa na miundombinu ya kisasa ya kutolea elimu.
Amesema
uongozi wa taasisi hiyo hauna budi kuweka mikakati ya kushirikiana na taasisi
nyingine zinazotoa mafunzo ya ufundi ndani na nje ya nchi ili kubadilishana
uzoefu.
Waziri
Mkuu amesema kulingana na maendeleo ya kiteknolojia na mahitaji ya soko uongozi
wa KIST ujipange kutoa mafunzi ya biomedical Engineering na kuimarisha mafunzo
ya matengenezo ya ndege na urubani katika ngazi ya stashahada.
Awali,
Waziri wa Elimu na Mafunzi ya Amali, Riziki Pembe Juma alisema Wizara yake
itaendeleza taasisi hiyo ili kuwaendeleza vijana na baadae waweze kujiajiri na
kuajiri.
Alisema
vijana wanaohitimu mafunzo ya fani mbalimbali katika taasisi hiyo wanapewa
mikopo ya masharti nafuu na Serikali baada ya kujiunga kwenye vikundi.
Waziri
Huyo, alisema wahitimu hao kabla ya kupewa mikopo wanaandika andiko la miradi
ambayo watakwenda kuitekeleza ambapo tayari vikundi zaidi ya 10 vya vijana
vimeshawezeshwa.
No comments:
Post a Comment