Waziri wa Kilimo, Mhe Japhet Hasunga (Mb) akisisitiza mpango wa serikali kusaini mikataba ya ubanguaji wa korosho wakati wa mkutano wake na waandishi wa habari uliofanyika katika ukumbi wa Bodi ya Korosho (CBT) Mkoani Mtwara, leo tarehe 8 Januari 2019. (Picha Zote Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo)
Waziri wa Kilimo, Mhe Japhet Hasunga (Mb) akisisitiza jambo wakati wa mkutano wake na waandishi wa habari uliofanyika katika ukumbi wa Bodi ya Korosho (CBT) Mkoani Mtwara, leo tarehe 8 Januari 2019.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Prof Siza Tumbo akifatilia mkutano wa Waziri wa Kilimo, Mhe Japhet Hasunga (Mb) wakati wa mkutano wake na waandishi wa habari uliofanyika katika ukumbi wa Bodi ya Korosho (CBT) Mkoani Mtwara, leo tarehe 8 Januari 2019.
Na Mathias
Canal, Wizara ya Kilimo-Mtwara
Serikali
imesema kuwa tarehe 10 Januari 2019 itasaini mikataba na wamiliki wa viwanda
vya ubanguaji wa korosho waliojitokeza kwa ajili ya kubangua korosho za
serikali za msimu wa mwaka 2018/2019 zilizonunuliwa na serikali kwa bei ya
Shilingi 3300 kwa kilo.
Waziri
wa Kilimo, Mhe Japhet Hasunga (Mb) ameyasema hayo leo tarehe 8 Januari 2019 wakati
wa mkutano wake na waandishi wa habari uliofanyika katika ukumbi wa Bodi ya
Korosho (CBT) Mkoani Mtwara.
Alisema
kuwa hivi karibuni serikali ilitangaza kuwa korosho ghafi zote zitabanguliwa
nchini hivyo utekelezaji wa jambo hilo umeanza, ambapo Bodi ya Nafaka na Mazao
mchanganyiko itaingia mikataba ya ubanguaji.
Pamoja
na wamiliki wa viwanda kupewa kazi ya kubangua korosho lakini pia serikali
imewakaribisha wananchi kujitokeza kubangua korosho za serikali kupitia vikundi
au mtu mmoja mmoja. “Wananchi wenye uwezo wa kubangua tunawaomba waende Shirika
la kuhudumia viwanda vidogo vidogo-SIDO) kwa ajili ya kujiandikisha ambapo
mpaka sasa watu 126 kwa ajili ya ubanguaji na Tani 29 zimechukuliwa kwa ajili
ya kuanza kubanguliwa” Alisisitiza Mhe Hasunga
Katika
mkutano huo Waziri huyo wa kilimo Mhe Japhet Hasunga amempongeza Mhe Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli kwa kushuhudia utiaji
wa saini mkataba wa mauziano ya mahindi kati ya Wakala wa Taifa wa hifadhi ya
Chakula (NFRA) na Shirika la Chakula Duniani (WFP) wa Bilioni 21
zitakazoiwezesha NFRA kunua mahindi kwa wakulima hivyo kuimarisha soko la
nafaka nchini.
Mhe
Hasunga alisema kuwa pamoja na kuanza ubanguaji kupitia SIDO lakini serikali
imeanza mchakato wa kukufua viwanda vya ubanguaji vya serikali na watu binafsi nchini
ili kuongeza ajira kwa wananchi ikiwa ni pamoja na kuanzisha vituo vya
wabanguaji wadogo wadogo.
Akizungumzia
kuhusu swala la malipo ya korosho na uhakiki wa wakulima alisema kuwa tayari
kiasi cha korosho ambayo imekusanywa kwenye maghala makuu ni Tani 203,938.3
wakati korosho iliyopo kwenye Vyama vikuu vya ushirika ni Tani 29,803.53
inayofanya jumla ya korosho yote iliyopokelewa kwenye vyama vya ushirika na
maghala makuu kuwa Tani 233,741.83 sawa na asilimia 84.7 ya lengo lililowekwa
la ukusanyaji katika Mikoa ya Mtwara, Lindi, Ruvuma na Pwani.
Kuhusu
malipo ya wakulima alisema kuwa miamala ya malipo ambayo imefanyika ni 261,458
yenye jumla ya watu 203,569. Aidha, vyama 490 vilimelipwa kati ya vyama 617, Alisema
Mkoa wa Mtwara jumla ya vyama 39 bado havijalipwa, Mkoa wa Lindi vyama vitano
na Ruvuma viwili hivyo serikali imejipanga ndani ya wiki mbili vyama hivyo kuwa
vimelipwa.
Waziri
Hasunga amesema kuwa mpaka kufikia jana tarehe 7 Januari 2019 fedha ambazo
zimeingizwa kwenye Account za wakulima ni zaidi ya Bilioni 257 huku ambazo
tayari zimeingia kwenye Account za wakulima ni Bilioni 226.2 ambapo Zaidi ya Bilioni
30.7 zilizohakikiwa bado hazijaingizwa kwenye Account za wakulima kutokana na taarifa
za baadhi ya wakulima hao kutofautiana majina ama vinginevyo. “Tunawaomba sana
wananchi kwenda Benki kujiridhisha kama Account zao zinafanya kazi kwani
serikali ina fedha za kuwalipa wakulima wote wa korosho” Alisema
“Tena
nisisitize kwa wale wanaofanya biashara ya korosho kinyume na utaratibu maarufu
kama (Kangomba) wajisalimishe na kuomba radhi wenyewe kuliko kusubiri serikali
iwabaini” Alisema
Vilevile,
Mhe Hasunga alisema kuwa wizara yake imeweka mikakati mbalimbali ambapo hadi kufikia
Januari 31 mwaka huu zoezi la uhakiki wa wakulima wanaostahili kulipwa liwe
limekamilika ambapo zaidi ya asilimia 80 ya wakulima wawe wamelipwa.
Pia
amewataka wananchi kupuuza taarifa mbalimbali zizotolewa na baadhi ya wananchi
wasiolitakia mema Taifa kupitia mitandao ya kijamii kuwa serikali hailipi
wakulima badala yake amesisitiza kuwa serikali ina fedha za kutosha kulipa
wakulima wa korosho isipokuwa kangomba wao hawatalipwa.
MWISHO
No comments:
Post a Comment