Monday, November 19, 2018

WENGI WANUFAIKA NA SEMINA YA UFUGAJI WA KISASA WA KUKU KUTOKA KUKU PROJECT,JIJINI DAR ES SALAAM


Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Kuku Project Bw. Geofrey Kayenga akifungua Semina kwa ajili ya ufugaji wa kisasa wa kuku kwa wafugaji na ambao wanahitaji kuanza na wanaofuga  kuku,  alisema kuwa lengo kubwa la semina hiyo ilikuwa ni kuhamasishana na kubadilishana ujuzi wa ufugaji wa kuku kwa ujumla na kuwapa njia za kisasa za ufugaji wa kuku, Chuo cha Ustawi wa Jamii Jijini Dar es Salaam.
Bi. Beatrice Kanemba Meneja Mawasiliano wa Kuku Project, akielezea kwa ufupi juu ya Kuku Project ambapo ilianza mwaka 2014, alisema kuwa malengo yao yalikuwa ni kuona sekta ya ufugaji inakuwa rasmi,watu kufanya ufugaji kama biashara,kutumia teknolojia ya mitandao ya kijamii kutoa elimu ya ufugaji wa kuku ili kuwafikia watu wengi zaidi. aliongeza kuwa baadhi bidhaa walivyonavyo ni pamoja na Vifaa vya kisasa vya ufugaji na vifaranga wa iana zote ya kuroirer pamoja na ushauri wa ufugaji wenye tija na usimamizi wa mabanda na masoko ndani na nje ya nchi. 
Bw. Deusdedit Nestory, Mkuu wa Kitengo cha Kuku Manispaa ya Kinondoni akielezea mikakati ya Serikali kupitia Wizara ya Kilimo na Ufugaji ambapo pamoja na kuhimiza wananchi kufanya shughuli zao kwa vikundi ili kuwarahisishia kupata mikopo na kufanya kazi kwa urahisi lakini pia wanatoa elimu ya ufugaji wa kuku kwa wananchi kuanzia ngazi ya Kata lengo likiwa ni kuboresha sekta ya ufugaji wa kuku.
Daktari wa Mifugo wa Kuku Project  Dkt. Shukuru akielezea namna wanavyotatua shida mbalimbali hasa za magonjwa ya kuku lakini pia kutoa ushauri wa kitaalam ili mfugaji asiweze kupata hasara hasa katika ufugaji wake.
Baadhi ya watu mbalimbali walifika katika semina hiyo wakiendelea kufuatilia masomo mbalimbali juu ya ufugaji wa kuku wa kisasa.
 Mmoja wa wafugaji aliyefika katika Semina hiyo akielezea matarajio yake na namna atakavyo nufaika na Kuku Project.
Mmoja wa washiriki  katika Semina hiyo akielezea namna alivyoelewa kuhusiana na ufugaji wa kuku kwa kutumia vifaa vya kisasa na wenye tija kwa washiriki wengine. 
Mwendesha Semina hiyo Bi. Zainab Muharami kutoka Kuku Project akielezea zaidi baadhi ya mambo yanayohusiana na Kuku Project.
Afisa Mikopo wa Kuku Project Sigbeth Fraden  akielezea taratibu za kupata mkopo kupitia Platinum Credit ambapo kwa sasa wanatoa mikopo kwa ajili ya ufugaji wa kuku kwa watumishi wa umma na mipango ya kuanza kuwapa mikopo hiyo kwa watu binafsi bado inaendelea.
 Mfugaji wa mda mrefu Mama Anna Mfinanga akielezea namna Kuku Project ilivyomsaidia na alivyofaidika nayo kutoka katika ufugaji mpaka kutaftiwa masoko sehemu mbalimbali ikiwemo ya mayai. 
Meneja Utendaji  wa Kuku Project Bw. Goodluck Kilango, akielezea namna watu wanaweza kufanikiwa zaidi katika ufugaji wa kuku na pia kuwataka vijana waweze kuwa wafugaji kwa sababu ufugaji unalipa, mwisho aliwashukuru wadau wote waliofika katika semina hiyo ya ufugaji iliyoandaliwa na Kuku Project.
Wafanyakazi wa kuku Project pamoja na wananchi mbalimbali waliofika katika semina ya ufugaji wa kuku wakiwa katika picha ya pamoja.
(Picha zote na Fredy Njeje)

No comments:

Post a Comment