Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo akimkabdhi fedha 'mwalimu' wa kujitolea katika kitongoji cha Senje, Kijiji cha Samazi anaewafundisha watoto wa kitongoji hicho ambao wapo mbali na shule ya msingi jambo lililowapelekea wazazi wa watoto wa kitongoji hicho kumlipa mwanafunzi huyo aliyemaliza kidato cha nne kuwafundisha watoto.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo akiongea na wananchi wa kitongoji cha Senje, Kijiji cha Samazi, Wilayani kalambo mara baada ya msafara wake kuzuiwa na wananchi hao wakidai kujengewa shule.
Wananchi wa kitongoji cha Senje, kijiji cha Samazi
Wilayani Kalambo wamefanikiwa kuuzui msafara wa mkuu wa mkoa wa Rukwa Mh.
Joachim Wangabo na kumuomba kuwawezesha wapate ushirikiano wa kujenga shule ili
watoto wao waweze kusoma.
Wananchi hao wameeleza kuwa shule ya msingi iliyopo
karibu ni kilomita saba kutoka katika kitongoji hicho ambapo shule hiyo ipo
katika kijiji cha Samazi huku watoto hao wengi wadogo wakishindwa kufika katika
shule hiyo kutokana na umbali.
Kitongoji hicho cha Senje ambacho ni kipya kimeanza
kukaliwa na wananchi na kuonesha maendeleo baada ya kuanza kujenga vyumba
viwili vya madarasa, kuchimba shimo la choo pamoja na kuwa na mabati kwaajili
ya kuezeka majengo hayo huku wakiwa na suluhisho la dharura kwa kumlipa posho
mwanafunzi aliyemaliza kidato cha nne ili aweze kuwafundisha watoto wao.
Kwa upande wake Mh. Wangabo alisema kuwa shule hiyo
inayojengwa katika kitongoji hicho itaanza kuwa shule shikizi ya shule ya
msingi samazi hivyo watoto hao wataanza kusoma shule ya awali, darasa la kwanza
hadi la tatu kasha watahamia katika shule ya msingi samazi wakati taratibu
nyingine zikiendelea.
Aliongeza kuwa ili vyuma hivyo vianze kutumika ni
muhimu kuwa na ofisi ya mwalimu na nyumba ya mwalimu ili halmashauri iweze
kuunga mkono kwa kumleta mwaalimu na watoto waanze kusoma na kuwashauri
kuongeza kasi ya ujenzi wa majengo hayo ili waweze kupewa mwaalimu haraka
iwezekanvyo kwakuwa serikali ya wamu ya tano isingependa kuwaona watoto
hawaendi shule.
“Kata pamoja na kijiji watasimamia hii, mkurugenzi
utafuatilia kuhakikisha kwamba mtendaji wa kijiji na kata watasimamia ujenzi
ule unaoendelea pale, lazima nyumba ya mwalimu isimame na ofisi ya mwali
isimame na wakati huo muendelee kujipanga kuna swala la madawati watoto wasije
wakakaa chini, vyoo ni uhimu ili wanafunzi watumie vyoo sio kwenda kwenye
vichaka, shule haiwezi kuanza bila ya vyoo, tutaneza milipuko,” Alisisitiza.
Katika kuhakikisha jambo hilo linafanikiwa Mkuu wa
mkoa alimuagiza mkurugenzi wa halmashauri ya Wilaya ya kalambo kuhakikisha
wanaunga mkono kwa kununua mbao za kupaulia huku ofisi yake ikichangia bati za
ofisi ya mwalimu pindi itakapokamilika.
Katika msafara huo ambao aliwepo mkuu wa Wilaya ya
Kalambo Mh. Julieth Binyura nae aliwataka kuhakikisha ujenzi wa shule hiyo
hauishii kwenye madarasa mawili tu na hatimae kuiachia serikali mzigo wa kuendelea
kujenga shule hiyo wakati kitongoji hicho hakikuwahi kuwepo.
“Serikali sasa hivi ina utaratibu wa kusajili, kama
hujatimiza vigezo huwezi kusajiliwa shule, hata mkiwa mmejenga vyumba viwili
lazima mujenge ili mtoto akimaliza la kwanza, la pili, la tatu anaendelea,
lakini wengine wakijenga vyumab wanaishia viwili tu halafu watoto wanaanza
kusomea chini ya miti hatutaki,” Alibainisha.
No comments:
Post a Comment