Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu akiwa na
Mwakilishi kutoka Ubalozi wa Austria nchini Tanzania (sehemu ya biashara), Kurt
Mullauer (kushoto) katika Ofisi ya Naibu Waziri jijini Dodoma.
Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu (katikati) akiwa na Mwakilishi kutoka Ubalozi wa Austria nchini Tanzania (sehemu ya biashara), Kurt Mullauer (kushoto) katika Ofisi ya Naibu Waziri jijini Dodoma.Kulia ni Kaimu Kamishna wa Umeme na Nishati Jadidifu, Mhandisi Innocent Luoga.
Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu amefanya
mazungumzo na Mwakilishi kutoka Ubalozi wa Austria Nairobi-Kenya, (sehemu ya
biashara), Kurt Mullauer aliyefika wizarani ili kumweleza kuhusu
Ujumbe wa Kibiashara kutoka Austria unaotarajiwa kuwasili nchini mwezi
Januari, 2019.
Mazungumzo hayo yamefanyika katika Ofisi za Wizara
ya Nishati jijini Dodoma na kuhudhuriwa na Kaimu Kamishna wa Umeme na Nishati
Jadidifu, Eng.Innocent Luoga na Mwakilishi wa Kaimu Kamishna wa Petroli na
Gesi, Ebenezer Mollel.
Kurt Mullauer amemweleza Naibu Waziri kuwa, ujumbe
huo wa kibishara utajumuisha makampuni 8 ambayo yanajishughulisha masuala ya
afya, usafirishaji na nishati na utawasili jijini Dodoma mwishoni mwa
mwezi Januari kwa ajili ya kukutana na viongozi na watendaji wa Serikali.
Mullauer ameongeza kuwa, nchi hiyo imekuwa ikiunga
mkono uendelezaji wa miradi ya umeme nchini na hadi sasa wameshatoa mikopo ya
masharti nafuu kwa baadhi ya miradi ya umeme iliyo nje ya gridi.
Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Nishati,
aliushukuru ubalozi wa Austria kwa uamuzi waliouchukua wa kuyaleta makampuni
hayo nchini ambapo Tanzania itapata fursa ya kueleza maeneo yanayohitaji
uwekezaji hasa katika miradi ya uzalishaji umeme ili kuweza kufikia lengo la
kuwa na megawati 5000 ifikapo mwaka 2020.
Naibu Waziri pia amemweleza Mullauer kuhusu maeneo
yote yanayohitaji ushirikiano na wawekezaji hasa ya uzalishaji umeme kwa
kutumia maji, gesi asilia na nishati jadidifu na usambazaji umeme vijijini.
No comments:
Post a Comment