Kaimu Mkurugenzi wa Uchaguzi Giveness Aswile
SUBIRA
KASWAGA – AFISA HABARI NEC
Tume
ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imesema kuwa jumla ya wagombea 13 walichukua fomu za kuomba kuteuliwa kugombea nafasi
ya Ubunge katika Majimbo ya Babati Mjini, Ukerewe, Simanjiro na Serengeti.
Akizungumza
ofisini kwake jijini Dar es Salaam, kuhusu
uteuzi huo Kaimu Mkurugenzi wa Uchaguzi Giveness Aswile amesema kuwa, wagombea
hao wanatoka katika vyama sita vya siasa ambavyo ni AFP, CCM, CUF, NCCR
Mageuzi, NRA na UDP.
Amesema
kuwa, hadi muda wa mwisho wa uteuzi Novemba 03, mwaka huu saa 10:00 jioni,
jumla ya wagombea wane wa Ubunge kutoka CCM, waliteuliwa na hivyo kutangazwa
kuwa wamepita bila kupingwa kwa mujibu wa kifungu cha 44 cha Sheria ya Taifa ya
Uchaguzi.
Wagombea
hao walitangazwa kupita bila kupinga baada ya wanachama wengine kutoka vyama
vilivyochukua fomu za uteuzi, kukosa sifa kutokana na sababu mbalimbali
zikiwemo kushindwa kurudisha fomu hizo kwa wakati na wengine kutojaza fomu hizo
kikamilifu ikiwa ni pamoja na kutojaza fomu ya kuheshimu na kuyazingatia
maaadili ya uchaguzi
Aidha
kwa upande wa udiwani katika kata 47 za Tanzania Bara, Aswile ameeleza kuwa, vyama
14 vya siasa vilishiriki ambapo wanachama 102 kutoka vyama hicvyo walichukua
fomu za uteuzi.
“Vyama
vilivyoshiriki ni AAFP, ACT – WAZALENDO, ADC, CCK, CCM, CHADEMA, CUF,
DEMOKRASIA MAKINI, NCCR – Mageuzi, NRA, SAU, TLP, UDP na UPDP” alisema Aswile
na kufafanua kuwa,
Hadi
Novemba 03, 2018 saa 10:00 jioni wanachama 73 tu ndio waliorejesha fomu na
kuteuliwa kuwa wagombea Udiwani.
Wanachama
wengine 29 hawakuteuliwa kuwa wagombea kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo
kushindwa kurejesha fomu za uteuzi, kutojaza fomu za uteuzi kwa usahihi,
kutosaini fomu za kuheshimu na kuzingatia maadili ya uchaguzi na kukosa sifa za
kugombea udiwani kwa mujibu wa sheria.
Aidha,
Aswile amefafanua kuwa wagombea 15 wa nafasi ya Udiwani waliwekewa pingamizi
kwa Msimamizi wa Uchaguzi na kupelekea wagombea 9 kuenguliwa kutoka katika
orodha ya wagombea wa nafasi ya udiwani.
Tume
ya Taifa ya Uchaguzi ilipokea rufaa mbili kutoka kwa Wagombea Udiwani wa Kata
ya Muhinda iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Buhigwe na Kata ya Mnyamani iliyopo
katika Halmashauri ya Manispaa ya Ilala wakipinga maamuzi ya Wasimamizi wa
Uchaguzi kuwaondoa katika kugombea udiwani.
Aidha,
katika kikao cha Tume kilichofanyika Novemba 09, 2018 kimeridhia rufaa moja ya
mgombea Udiwani wa CUF katika kata ya Muhinda Halmashauri ya Wilaya ya Buhigwe
na hivyo kumrudisha mgombea katika nafasi hiyo.
“Tume
imekubaliana na maamuzi ya Msimamizi wa Uchaguzi katika kata ya Mnyamani
Halmashauri ya Manispaa ya Ilala ya kumuondoa mgombea wa CUF katika orodha ya
wagombea na hivyo mgombea kuendelea kuenguliwa kugombea udiwani” alisema Aswile.
Aidha,
katika kata 47 jumla ya wagombea udiwani katika kata 41 wamepita bila kupingwa
na hivyo ni kata sita tu ndizo zitakazofanya uchaguzi Mdogo tarehe 02, Desemba mwaka huu.
Amezitaja
kata hizo kuwa ni Nkoanekoli iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Meru,
Kivinje/Singino, Mteja, Somanga, Mitole zote katika Halmashauri ya Kilwa na
kata ya Butimba iliyopo Halmashauri ya wilaya ya Bunda.
Kampeni
za uchaguzi zimeanza tarehe 04 Novemba 2018 na zitakamilika tarehe 01 Desemba
siku moja kabla ya uchaguzi.
Aswile
amevikumbusha vyama vya siasa na wagombea kuheshimu Maadili ya Uchaguzi wa
Rais, Wabunge na Madiwani ya mwaka 2015 wakati wote wa kampeni na hata siku ya
uchaguzi.
No comments:
Post a Comment