Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa ikiongozwa na Mkuu wa Mkoa pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga na Mkurugenzi wa manispaa ya Sumbawanga walipotembelea moja ya maduka ya wauzaji wa mbolea yaliyopo mjini Sumbawanga.
Mkuu wa Mkoa
wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo ametembela ghala la kuhifadhia mbolea la Kampuni
ya Mbolea Tanzania (Tanzania Fertilizer Company – TFC) na
kutokuta hata mfuko mmoja wa mbolea huku wakulima wakijiandaa na msimu wa
kilimo wa mwaka 2018/2019 huku mvua zikitarajiwa kuanza hivi karibuni.
Mh. Wangabo
amefanya ziara fupi katika maghala kadhaa ya wafanyabiashara binafsi pamoja na
makampuni yaliyopo mjini sumbawanga na kukuta shughuli za uletaji wa mbolea
ukiendelea kwa maandalizi yam simu wa kilimo huku Kampuni ya Mboleaa Tanzania
(TFC) ikikosa hata mfuko mmoja katika ghala lao jambo lililowashanga
walioambatana na Mkuu wa Mkoa katika ziara hiyo.
“Tutawasiliana
na viongozi wa TFC ili tuweze kujua kwanini hawaleti mbolea ya kutosha wakati
hii ni kampuni ya serikali inaweza ikaleta mbolea nyingi kuliko hata hao
wengine lakini badala yake “godown” (ghala) kubwa lakini hakuna kitu, nini
manufaa ya TFC sasa,” Alihoji.
Awali akisoma
taarifa ya kampuni hiyo msimamizi wa ghala hilo Jelio Mahenge alisema kuwa
msimu wa kilimo wa mwaka 207/2018 kampuni ilifanikiwa kusambaza tani 1082 na
kuwa msimu wa kilimo wa mwaka 2018/2019 kampuni imejipanga kuleta jumla ya tani
2500 kwa awamu ya kwanza.
“Mheshimiwa
Mkuu wa Mkoa kampuni inafanya jitihada zote za hali na mali kuhakikisha uletaji
wa mbolea unatekelezeka ndani ya mwezi huu wa kumi na moja ili kuendana na
msimu wa kilimo na kuleta tija kwa wakulima na nchi kwa ujumla,”
Msimu wa
Kilimo wa mwaka 2017/2018 Mkoa ulitumia zaidi ya tani 24,000 za Mbolea ya
kupandia (DAP) na mbolea ya kukuzia (UREA) na msimu wa kilimo wa mwaka
2018/2019 mkoa unatarajiwa kutumia zaidi ya tani 34,000 na mpaka mwanzoni mwa
mwezi huu Mkoa umepokea tani 363.75 ambazo tayari zikiwa ndani ya maghala ya
wafanyabiashara wa mbolea na nyingine zikiwa njiani.
No comments:
Post a Comment