Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiweka jiwe
la msingi la ujenzi wa Hospitali ya wilaya ya Geita ya Nzera, Novemba 27,
2018. Wapili kulia ni Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani na kulia ni Naibu
Waziri, Ofisi ya Rais TAMISEMI, Mwita Waitara . Watatu kulia ni Mbunge wa
Geita Vijijini, Joseph Msukuma na wapili kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa
Geita, Mhandisi Robert Gabriel. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwasalimia wanawake waliojifungua katika
Hospitali ya Wilaya ya Geita ya Nzera baada ya kuweka jiwe la Msingi la
Ujenzi wa Hospitali hiyo, Novemba 27, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akijadili jambo na Mbunge wa Geita
Vijijini, Jioseph Msukuma wakati alipotembelea Wodi ya Wazazi katika
Hospitali ya Wilaya ya Geita, Novemba 27, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
WAZIRI MKUU
Kassim Majaliwa amesema Serikali imepanga kumaliza tatizo la upatikanaji wa
huduma ya maji safi na salama kwa kuchimba visima virefu na vifupi pamoja na
kutumia maji ya maziwa na mito na kuyapeleka katika maeneo mbalimbali ya
wananchi nchini.
Pia, Waziri Mkuu amewaagiza
wakuu wa wilaya kusimamia uhifadhi wa maeneo ambayo yana vyanzo vya maji ili
kuyafanya yaendelee kuwa chepechepe, hivyo kuhakikisha vijiji vyote vinapata
maji ya uhakika. “Lazima maeneo hayo yatambuliwe na yahifadhiwe.”
Ameyasema hayo leo (Jumanne, Novemba 27, 2018) alipozungumza na wananchi kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika Uwanja wa shule Sekondari Bugando kata ya Nzera wilayani Geita, wakati akiwa katika ziara yake ya kikazi za siku nne mkoani Geita.
Waziri Mkuu amesemaSerikali kupitia Kampeni ya Rais Dkt. John Magufuli ya kumtua mama ndoo kichwani, itahakikisha wananchi katika maeneo yote nchini wanapata huduma ya maji safi na salama karibu na maeneo yao ya makazi.
Amesema Serikali imejipanga vizuri kuhakikisha kila kijiji kinapata huduma ya maji safi na salama, hivyo amewaagizawatendaji wote wa vijiji kuainisha maeneo yote yenye misitu na vyanzo vya maji na kuhakikisha yanalindwa.
Kadhalika, Waziri Mkuu amesema mbali na huduma ya maji, pia Serikali imedhamiria kusambaza umeme katika vijiji vyote ambavyo bado havijaunganishiwa nishati hiyo nchini vitaunganishiwa katika awamu ya tatu ya Mradi wa Nishati Vijijini (REA).
“Rais wetu Dkt. John Magufuli anataka kuona nyumba ya kila Mtanzania inapata umeme tena kwa gharama nafuu na ametenga fedha nyingi zitakazotosheleza kusambaza umeme katika vijiji vyote nchini. Gharama za kuunganishiwa umeme huo ni sh. 27,000 tu.”
Hata hivyo, Waziri Mkuu amesema wananchi hawatowajibika tena katika kulipia gharama za nguzo wala fomu za maombi ya kuunganishiwa umeme kwa sababu tayari gharama hizo zimeshabebwa na Serikali.
Naye, Mbunge wa jimbo la Geita Vijijini, Joseph Musukuma ameishukuru Serikali kwa utekelezaji wa miradi na ahadi zikiwemo na zile zilizotolewa za Rais Dkt. John Magufuli. “Nashukuru Serikali pia kwa kutuzindulia hospitali ya halmashauri ya wilaya ya Geita.”
Kuhusu suala la umeme, Mbunge huyo ameishukuru Serikali kwa kuwa vijiji vyake vyote vimeshaunganishiwa umeme isipokuwa vitongoji vichache, ambapo ameomba navyo viunganishiwe nishati hiyo muhimu kwa maendeleo ya wananchi.
Awali,Waziri Mkuu alikagua na kuzindua hospitali ya wilaya ya Geita inayojengwa katika kata ya Nzera na aliupongeza uogozi wa halmashauri ya wilaya ya Geita kwa hatua waliyofikia katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo.
No comments:
Post a Comment